Nani aliidangaya CHADEMA iitose vita dhidi ya ufisadi?

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
MPAKA sasa kila nikitafakari nashindwa kuelewa nini hasa kilikuwa kinaendelea katika vichwa vya viongozi wa juu wa Chadema hadi kukubaliana kuitosa ajenda ya ufisadi katika uchaguzi mkuu wa safari hii na kumchukua Edward Lowassa kuwa mgombea urais wake. Mbali ya kumteua Lowassa kuwa mgombea urais wake, Chadema kilikwenda mbali zaidi hivi karibuni kwa kuiondoa kwenye tovuti yake ile orodha yake ya ‘mafisadi papa' (list of shame) ambayo huko nyuma kilikuwa kikiitumia kujenga hoja kuwa CCM ni chama cha mafisadi. Kwenye orodha hiyo Lowassa alikuwa Na. 9.

Hatua hiyo ya kuiondoa orodha ya ‘mafisadi papa' katika tovuti yake inathibitisha, pasipo shaka yoyote, kwamba vita dhidi ya ufisadi sasa siyo tena ajenda kuu ya chama hicho kikuu cha Upinzani nchini. Vyovyote vile; imani yangu ni kwamba baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 kufahamika, Chadema kitaishi na majuto. Kitajutia kosa hilo kubwa la kiuongozi kililofanya ikiwa ni pamoja na lile la kuwapokea watuhumiwa wa ufisadi kutoka CCM na kuwapa nafasi za kugombea ubunge huku kikiwatosa baadhi ya makada wake wa miaka mingi walioshiriki kukiimarisha.

Nasema hivyo kwa sababu chama tawala CCM kimeidaka ajenda hiyo na kinaitumia vizuri katika kampeni, na sasa kila dalili zinaonyesha kitaibuka na ushindi Oktoba 25. Wakati kwenye kampeni Chadema kinahangaika kumsafisha mgombea urais wake, Edward Lowassa dhidi ya tuhuma za kuhusika na ufisadi wa Richmond, CCM kinasisimua maelfu kwa kauli za mgombea urais wake, John Magufuli kwamba ataunda mahakama maalumu za kuwashughulikia mafisadi na majizi!

Hivi ni nani aliyeidanganya Chadema kwamba kinaweza kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu bila kujikita sana kwenye ajenda ya ufisadi ambayo kwayo kilipata umaarufu kilionao? Hivi ni nani ndani ya Chadema asiyejua ya kuwa kwa miaka karibu 20 iliyopita hakuna ajenda kuu iliyotawala chaguzi mbili kuu zilizopita zaidi ya ile ya ufisadi? Hivi ni nani asiyekumbuka kwamba kwenye uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa Chadema kilifanya vizuri kwa sababu kilitumia ufisadi wa Escrow Account kuipa kipigo CCM?

Hivi ni nani ndani ya chama hicho asiyejua kuwa ajenda ya ufisadi ina umri wa zaidi ya miaka 20 nchini, na kwamba huwezi kuitosa ghafla (‘kubadili gia angani' kwa mujibu wa Mbowe), na kisha ukashinda uchaguzi mkuu? "Hakuna kitakachowezekana katika jamii hii mpaka hapo tutakapokuwa tumevaa njuga kupambana na uozo uliotufika shingoni. Ndiyo maana hatutakiwi kufanya mchezo katika kuchagua viongozi wetu. Kigezo cha kwanza cha kila mgombea kiwe ni uwezo wake na mwelekeo wake katika kupambana na uozo huu.

" Ni ujinga kumchagua mtu kwa sababu ni rafiki yako, au anatoka unakotoka wewe, au ni wa kabila lako. Hali tuliyo nayo ni hali ya hatari kubwa kiasi kwamba hakuna anayeweza kutuhakikishia kwamba tutaendelea kuwa na amani. Bima pekee tunayoweza kununua ili tuwe na amani ni kujitosa katika mapambano dhidi ya uozo huu." Hayo si maneno yangu. Hayo ni maneno ya mwanasafu wa gazeti hili, Jenerali Ulimwengu. Yamo katika makala aliyoiandika katika gazeti la Rai zaidi ya miaka 20 iliyopita.Mfano wa uozo alioutoa katika makala hiyo ni ufisadi uliokuwa umeikumba miradi ya wakati ule ya kudhibiti malaria na Ukimwi.

Waratibu wa miradi hiyo walikuwa wameigeuza kama njia ya kujitajirisha wao binafsi; licha ya kwamba ililenga kunusuru maisha ya watu. Kama nilivyosema awali, Jenerali aliiandika makala hiyo zaidi ya miaka 20 iliyopita. Kama zaidi ya miaka 20 iliyopita aliandika ya kwamba hali ya ufisadi iliyokuwepo wakati huo ilikuwa ya hatari kubwa, sijui leo angelitumia maneno gani kuieleza hali ya sasa ya ufisadi ya Tanzania yetu!

Ndugu zangu, hali sasa ni mbaya mara 20 zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita wakati Jenerali akiandika makala hiyo kulalamikia ufisadi uliokuwa umetamalaki nchini. Huo ndio ukweli mchungu! Na ndo maana naishangaa Chadema kuitosa ajenda ya ufisadi. Huko nyuma nilishawahi kusema kwamba mtu akiniamsha usingizini saa nane usiku na kuniuliza ni tatizo gani moja kuu linaloiangamiza Tanzania yetu kwa sasa nitamjibu kuwa ni ufisadi na kuporomoka kwa maadili.

IPTL ni ufisadi, Escrow ni ufisadi, ununuzi vipaza sauti bungeni – ufisadi, biashara meno ya tembo – ufisadi, ugawaji vitalu vya uwindaji na vya gesi asilia – ufisadi, ujenzi maabara – ufisadi, uuzaji UDA na mashirika mengine ya umma – ufisadi, zabuni za halmashauri – ufisadi, uchimbaji madini – ufisadi, vyeo, chaguzi na nyadhifa – ufisadi, manunuzi ya umma – ufisadi, utoaji ajira – ufisadi, huduma za jamii kama elimu na afya – ufisadi, utoaji haki mahakamani – ufisadi, ujenzi wa barabara – ufisadi, utoaji ardhi za vijiji kwa wawekezaji - ufisadi; yaani ni ufisadi, ufisadi, ufisadi!

Ni kweli kuwa tuna matatizo mengi – kuanzia ya ukosefu wa ajira, elimu duni, kilimo duni, huduma duni za afya, miundombinu duni, ukosefu wa maji safi na salama kwa watu wetu, demokrasia changa na utawala dhaifu nk.Ni kweli pia kwamba wagombea wetu wakuu wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 – John Magufuli na Edward Lowassa wamekuwa wakipita mikoani kwenye kampeni zao na kuahidi kuyashughulikia baadhi ya matatizo hayo.

Hata hivyo, ni mtazamo wangu kwamba hakuna atakayefanikiwa kwa kiwango cha kuridhisha kama hatapambana kwanza kuuondosha uozo huo; yaani ufisadi na kuporomoka kwa maadili. Naamini hivyo kwa sababu juhudi zozote zitakazofanywa na rais wetu mpya (awe Magufuli au Lowassa) za kutatua matatizo ya ukosefu wa ajira, elimu duni, kilimo duni, huduma duni za afya, miundombinu duni nk, zitakwazwa na kutamalaki kwa ufisadi katika kila nyanja ya maisha yetu.

Ndugu zangu, Rais Kikwete alipotamka ya kwamba kuna ‘mchwa' serikalini wanaotafuna fedha za umma hakuwa anatania. Huo ndiyo ukweli. Kwa hiyo, adui mkubwa wa rais wetu mpya ajaye ni ufisadi. Jenerali Ulimwengu ameandika katika makala yake hiyo ya zaidi ya miaka 20 iliyopita ya kwamba; "kigezo cha kwanza cha kila mgombea urais kiwe ni uwezo wake na mwelekeo wake katika kupambana na uozo huu."

Mimi nakubaliana naye kwamba kigezo hicho kilikuwa muhimu miaka 20 iliyopita alipoandika makala hiyo, lakini nasisitiza kwamba bado kigezo hicho ni muhimu mno katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu; kwani tatizo limekuwa kubwa mara 20 zaidi kuliko lilivyokuwa zama hizo. Na ndiyo maana, binafsi, nawapima Magufuli na Lowassa kwa kigezo hicho. Mwenye nafuu katika hilo huyo ndiye nitampa kura yangu Oktoba 25, na naamini inapaswa pia kuwa hivyo kwa wengine wote wenye mapenzi ya kweli na nchi hii.

Bahati nzuri (kama unaweza kuiita bahati nzuri) ukiwasikiliza wakihutubia mikutano yao ya kampeni ni vigumu kuwaelewa Magufuli na Lowassa wanaegemea upande gani katika siasa za dunia hii – yaani Kushoto au Kulia au Kati au Kati Kulia au Kati Kushoto. Hivi sasa wanahenya majukwaani na kutoa jasho wakiahidi kuwa watafanya hiki na kile wakiingia Ikulu. Mmojawao (Lowassa) wala hata hahangaiki kuwafafanulia wapiga kura ilani au sera za chama chake (Chadema) ambazo kwazo atazisimamia akiingia Ikulu.

Kwa hiyo, kwa kuwa hatuwaelewi wakiingia Ikulu wataielekeza Tanzania yetu upande gani katika siasa za dunia hii, na kwa kuwa pia wakiwa majukwaani hawazungumzii sana ilani na sera za vyama vyao, wanatubakishia kigezo kimoja tu kikubwa cha kuwapima – nacho ni uwezo wao wa kupambana na ufisadi na mmomonyoko wa maadili. Katika makala yake hiyo ya zaidi ya miaka 20 iliyopita, Jenerali ameandika: "Ndiyo maana hatutakiwi kufanya mchezo katika kuchagua viongozi wetu". Nami nasisitiza leo - zaidi ya miaka 20 baadaye ya kwamba tusifanye mchezo katika kuwapima Lowassa na Magufuli. Natutumie kigezo hicho kuwapima.

Tukipuuza na kufanya mchezo na kushabikia ule ujinga wa baadhi yetu kwamba eti tufanye tu mabadiliko hata kama tunayemwingiza Ikulu ni shetani, tutakuja kujuta kwa sababu tutamwingiza Ikulu ‘Bw. Changamkiatenda'; yaani rais ambaye atataka kujichotea ten percent katika kila mradi mkubwa wa serikali – uwe ni wa ujenzi wa barabara au ugawaji vitalu vya gesi asilia nk. Kwangu mimi - kati ya hao wawili – Magufuli na Lowassa, sipati taabu mno kumtambua ni nani anayeweza kugeuka kuwa ‘Rais Mchangamkiatenda' akiingia Ikulu.

Yule mwenye ugonjwa wa kupenda kujilimbikizia mali… yule ambaye amejilimbikizia mali nyingi katika muda wake wa uongozi serikalini ndiye mwenye uwezekano mkubwa wa kugeuka ‘Rais Mchangamkiatenda' akiingia Ikulu! Vyovyote vile, tusibabaishwe na ahadi zinazowatoka midomoni wakiwa majukwaani wakati wa kampeni; bali tupime na kuangalia iwapo maneno wanayoyatamka kuhusu vita dhidi ya ufisadi yanatoka kweli mioyoni mwao au ni usanii mtupu. Vita dhidi ya ufisadi si jambo la kufanyia usanii hata kidogo. Matatizo makubwa yanayowakabili wananchi na taifa hili yangekuwa yamepungua kwa asilimia 50 kama taifa lisingekuwa linatafunwa na kansa hii ya ufisadi na kumomonyoka kwa maadili.

Na ndiyo maana nakubaliana na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliposema, wiki iliyopita, kwamba ufisadi nchini unasababisha asilimia 30 ya bajeti ya nchi kuishia mifukoni mwa vigogo serikalini na maswahiba wao nje ya serikali – yaani wachezaji wenzao wa ile timu ninayoiita mimi Mafisadi United!Nihitimishe safu yangu ya leo kwa kusisitiza tena kwamba wapimeni wenyewe Magufuli na Lowassa kwa kutumia akili zenu wenyewe za kuzaliwa na zile za kuambiwa, na kisha fanyeni uamuzi sahihi unaotokana na kuwajua vyema wote wawili.

Jiulizeni wenyewe ni yupi kati ya Lowassa na Magufuli anakidhi kigezo kile cha kwanza alichokizungumzia Jenerali yapata miaka 20 iliyopita.Jiulizeni:Ni yupi ana uwezo, mwelekeo na dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi akiingia Ikulu? Ni Edward Lowassa au ni John Magufuli?Jiulizeni hayo; maana itakuwa balaa kumsindikiza kuingia Ikulu ‘Rais Mchangamkiatenda'. Binafsi – hata nitukanwe vipi kwa simu, sms na emails, siko tayari kumsindikiza Ikulu rais wa sampuli hiyo. Tafakari.

Chanzo: Raia Mwema

Tena tenda zote atazichukua yeye na kundi lake na kufunga mikataba ya miaka Mia kiasi kwamba hata hao wanaomsindikiza watajuta na kuishia kuwa wasindikizaji wa maisha milele kwa kuishia kuwa watumwa wa kundi hilo. Jamaa hao wanafanya biashara ya akili za hali ya juu utadhani kama vile weeeema kumbe offside. Bora lichama letu ambalo ni open ground la kila mtu kuchangamkia nafasi na mara nawe una win. Hilo lichama la hilo kundi litaendeshwa kiukoo milele kwa staili ya u kanda na u dini ambayo ndiyo msingi mkuu. Ole wako unayeni shit sasa
 
Nani aliidangaya Chadema iitose vita dhidi ya ufisadi?

Raia Mwema

Kaka lowasa ni mpiga dili ataiuza nchi huyu, hatufai
 
Sisi wa upande wa pili yaani Chadema asilia tutakachofanya ni haya
1) tutafukuza mafisadi na majizi yaliyotoka ccm yarudi hukohuko. Hatuyataki tena kwa sababu yamekuja kuua upinzani
2) tutawataka makamanda waliowakaribisha mafisadi wote wajipime na wakae pembeni. Hiyo ni lazima. Na sio pembeni tuu hata pia tusiwaone maofisini kwetu. Tutakwenda funga makufuli pale ofisini.
3) tutawataka viongozi makamanda watuambie ni hela ngapi walihongwa ili kupokea wageni hao. Kwa sababu tunajua haiwezi kuwa burebure
4) tutataka kujua sasa mapato na matumizi ya fedha za wananchi. Kwa sababu tumeshaona ufisadi upi sana ndani ya chama chetu.
5) hapo sasa tutawaita Dr Slaa na Prof Lipumba waje wabebe na kuibua jahazi lililozama.
6) tutawataka viongozi wa vyama vingine warudi kwenye vyama vyama vyao vinavyokufakufa wasije wakatulaumu tumechangia kuua vyama vyao. Kwa sababu kiukweli vyama hivi Mbowe ameshaviua kabisa hatujui vitaibukaje tena. Wananchi wamepoteza matumaini kabisaaa. Kwa mtaji huu ukiunganisha na wenzetu kwa maslahi mapana ya mama Tanzania tutaweza kufungua mahakama ya mafisadi haraka ili tuwakamate tuanze nao hao. ni hayo kwa ufupi
 
Fisadi ni ccm na wanachama wote walioiba pesa za escrow! Ulimsikia Lowassa akitajwa kwenye orodha ya escrow? Subirini wiki 2 zijazo ndo mtajua Lowassa anamaanisha kitu gani. Lumumba itaungua yote hamtapata pa kutokea mtakanyagana wenyewe .
 
Sisi wa upande wa pili yaani Chadema asilia tutakachofanya ni haya
1) tutafukuza mafisadi na majizi yaliyotoka ccm yarudi hukohuko. Hatuyataki tena kwa sababu yamekuja kuua upinzani
2) tutawataka makamanda waliowakaribisha mafisadi wote wajipime na wakae pembeni. Hiyo ni lazima. Na sio pembeni tuu hata pia tusiwaone maofisini kwetu. Tutakwenda funga makufuli pale ofisini.
3) tutawataka viongozi makamanda watuambie ni hela ngapi walihongwa ili kupokea wageni hao. Kwa sababu tunajua haiwezi kuwa burebure
4) tutataka kujua sasa mapato na matumizi ya fedha za wananchi. Kwa sababu tumeshaona ufisadi upi sana ndani ya chama chetu.
5) hapo sasa tutawaita Dr Slaa na Prof Lipumba waje wabebe na kuibua jahazi lililozama.
6) tutawataka viongozi wa vyama vingine warudi kwenye vyama vyama vyao vinavyokufakufa wasije wakatulaumu tumechangia kuua vyama vyao. Kwa sababu kiukweli vyama hivi Mbowe ameshaviua kabisa hatujui vitaibukaje tena. Wananchi wamepoteza matumaini kabisaaa. Kwa mtaji huu ukiunganisha na wenzetu kwa maslahi mapana ya mama Tanzania tutaweza kufungua mahakama ya mafisadi haraka ili tuwakamate tuanze nao hao. ni hayo kwa ufupi

UmeshafukuZwa ...anzisha cha kwako..eti chadema asilia ?wewe unaweza ukamshinda Mtei kwa uasilia wa Chadema?Fanya hivi wewe kaanzishe chama chako au jiunge na CcM haahaaaa
 
Lowassa na wenzie ni genge la wezi wakubwa ila tunamshukuru Mungu kwani hawatakaa waione Ikulu yetu hawa majizi
 
Walisema ni ndoto cdm kushinda bila ya Daktari Slaa sasa pengo lake naliona..
 
Haiitaj kutumia IQ kuelewa kilicho andikwa tumia elim yako kusoma hyo habar ndo uulize sawar lako

Agenda ya uchaguzi wa mwaka huu kama ni ufisadi basi ccm itaondoka madarakani saa 4 asubuhi.

Kama tunalazimishwa tuendelee kuamini fisadi ni Lowassa peke yake ili Ccm ibaki madarakani tunalidanganya taifa.

Wezi wa Epa, kagoda, escrow , waliouza nyumba za serikali na kuleta kivuko cha MV Dar es salaam kikiwa chini ya kiwango kulingana na pesa iliyotumika kukinunua, leo nao wanaomba urais tunacheka tu.

Juzi wamepitisha mafuta na gesi kwa hati ya upepo tena bila uoga leo tunawachekea tu, sitakuwa sehemu ya ujunga huo nitamchagua Lowassa fisadi mmoja kuliko kuchagua mafisadi 100000 yaliyobaki ccm mtanisamehe.
 
MPAKA sasa kila nikitafakari nashindwa kuelewa nini hasa kilikuwa kinaendelea katika vichwa vya viongozi wa juu wa Chadema hadi kukubaliana kuitosa ajenda ya ufisadi katika uchaguzi mkuu wa safari hii na kumchukua Edward Lowassa kuwa mgombea urais wake. Mbali ya kumteua Lowassa kuwa mgombea urais wake, Chadema kilikwenda mbali zaidi hivi karibuni kwa kuiondoa kwenye tovuti yake ile orodha yake ya ‘mafisadi papa’ (list of shame) ambayo huko nyuma kilikuwa kikiitumia kujenga hoja kuwa CCM ni chama cha mafisadi. Kwenye orodha hiyo Lowassa alikuwa Na. 9.

Hatua hiyo ya kuiondoa orodha ya ‘mafisadi papa’ katika tovuti yake inathibitisha, pasipo shaka yoyote, kwamba vita dhidi ya ufisadi sasa siyo tena ajenda kuu ya chama hicho kikuu cha Upinzani nchini. Vyovyote vile; imani yangu ni kwamba baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 kufahamika, Chadema kitaishi na majuto. Kitajutia kosa hilo kubwa la kiuongozi kililofanya ikiwa ni pamoja na lile la kuwapokea watuhumiwa wa ufisadi kutoka CCM na kuwapa nafasi za kugombea ubunge huku kikiwatosa baadhi ya makada wake wa miaka mingi walioshiriki kukiimarisha.

Nasema hivyo kwa sababu chama tawala CCM kimeidaka ajenda hiyo na kinaitumia vizuri katika kampeni, na sasa kila dalili zinaonyesha kitaibuka na ushindi Oktoba 25. Wakati kwenye kampeni Chadema kinahangaika kumsafisha mgombea urais wake, Edward Lowassa dhidi ya tuhuma za kuhusika na ufisadi wa Richmond, CCM kinasisimua maelfu kwa kauli za mgombea urais wake, John Magufuli kwamba ataunda mahakama maalumu za kuwashughulikia mafisadi na majizi!

Hivi ni nani aliyeidanganya Chadema kwamba kinaweza kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka huu bila kujikita sana kwenye ajenda ya ufisadi ambayo kwayo kilipata umaarufu kilionao? Hivi ni nani ndani ya Chadema asiyejua ya kuwa kwa miaka karibu 20 iliyopita hakuna ajenda kuu iliyotawala chaguzi mbili kuu zilizopita zaidi ya ile ya ufisadi? Hivi ni nani asiyekumbuka kwamba kwenye uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa Chadema kilifanya vizuri kwa sababu kilitumia ufisadi wa Escrow Account kuipa kipigo CCM?

Hivi ni nani ndani ya chama hicho asiyejua kuwa ajenda ya ufisadi ina umri wa zaidi ya miaka 20 nchini, na kwamba huwezi kuitosa ghafla (‘kubadili gia angani’ kwa mujibu wa Mbowe), na kisha ukashinda uchaguzi mkuu? “Hakuna kitakachowezekana katika jamii hii mpaka hapo tutakapokuwa tumevaa njuga kupambana na uozo uliotufika shingoni. Ndiyo maana hatutakiwi kufanya mchezo katika kuchagua viongozi wetu. Kigezo cha kwanza cha kila mgombea kiwe ni uwezo wake na mwelekeo wake katika kupambana na uozo huu.

“ Ni ujinga kumchagua mtu kwa sababu ni rafiki yako, au anatoka unakotoka wewe, au ni wa kabila lako. Hali tuliyo nayo ni hali ya hatari kubwa kiasi kwamba hakuna anayeweza kutuhakikishia kwamba tutaendelea kuwa na amani. Bima pekee tunayoweza kununua ili tuwe na amani ni kujitosa katika mapambano dhidi ya uozo huu.” Hayo si maneno yangu. Hayo ni maneno ya mwanasafu wa gazeti hili, Jenerali Ulimwengu. Yamo katika makala aliyoiandika katika gazeti la Rai zaidi ya miaka 20 iliyopita.Mfano wa uozo alioutoa katika makala hiyo ni ufisadi uliokuwa umeikumba miradi ya wakati ule ya kudhibiti malaria na Ukimwi.

Waratibu wa miradi hiyo walikuwa wameigeuza kama njia ya kujitajirisha wao binafsi; licha ya kwamba ililenga kunusuru maisha ya watu. Kama nilivyosema awali, Jenerali aliiandika makala hiyo zaidi ya miaka 20 iliyopita. Kama zaidi ya miaka 20 iliyopita aliandika ya kwamba hali ya ufisadi iliyokuwepo wakati huo ilikuwa ya hatari kubwa, sijui leo angelitumia maneno gani kuieleza hali ya sasa ya ufisadi ya Tanzania yetu!

Ndugu zangu, hali sasa ni mbaya mara 20 zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita wakati Jenerali akiandika makala hiyo kulalamikia ufisadi uliokuwa umetamalaki nchini. Huo ndio ukweli mchungu! Na ndo maana naishangaa Chadema kuitosa ajenda ya ufisadi. Huko nyuma nilishawahi kusema kwamba mtu akiniamsha usingizini saa nane usiku na kuniuliza ni tatizo gani moja kuu linaloiangamiza Tanzania yetu kwa sasa nitamjibu kuwa ni ufisadi na kuporomoka kwa maadili.

IPTL ni ufisadi, Escrow ni ufisadi, ununuzi vipaza sauti bungeni – ufisadi, biashara meno ya tembo – ufisadi, ugawaji vitalu vya uwindaji na vya gesi asilia – ufisadi, ujenzi maabara – ufisadi, uuzaji UDA na mashirika mengine ya umma – ufisadi, zabuni za halmashauri – ufisadi, uchimbaji madini – ufisadi, vyeo, chaguzi na nyadhifa – ufisadi, manunuzi ya umma – ufisadi, utoaji ajira – ufisadi, huduma za jamii kama elimu na afya – ufisadi, utoaji haki mahakamani – ufisadi, ujenzi wa barabara – ufisadi, utoaji ardhi za vijiji kwa wawekezaji - ufisadi; yaani ni ufisadi, ufisadi, ufisadi!

Ni kweli kuwa tuna matatizo mengi – kuanzia ya ukosefu wa ajira, elimu duni, kilimo duni, huduma duni za afya, miundombinu duni, ukosefu wa maji safi na salama kwa watu wetu, demokrasia changa na utawala dhaifu nk.Ni kweli pia kwamba wagombea wetu wakuu wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 – John Magufuli na Edward Lowassa wamekuwa wakipita mikoani kwenye kampeni zao na kuahidi kuyashughulikia baadhi ya matatizo hayo.

Hata hivyo, ni mtazamo wangu kwamba hakuna atakayefanikiwa kwa kiwango cha kuridhisha kama hatapambana kwanza kuuondosha uozo huo; yaani ufisadi na kuporomoka kwa maadili. Naamini hivyo kwa sababu juhudi zozote zitakazofanywa na rais wetu mpya (awe Magufuli au Lowassa) za kutatua matatizo ya ukosefu wa ajira, elimu duni, kilimo duni, huduma duni za afya, miundombinu duni nk, zitakwazwa na kutamalaki kwa ufisadi katika kila nyanja ya maisha yetu.

Ndugu zangu, Rais Kikwete alipotamka ya kwamba kuna ‘mchwa’ serikalini wanaotafuna fedha za umma hakuwa anatania. Huo ndiyo ukweli. Kwa hiyo, adui mkubwa wa rais wetu mpya ajaye ni ufisadi. Jenerali Ulimwengu ameandika katika makala yake hiyo ya zaidi ya miaka 20 iliyopita ya kwamba; “kigezo cha kwanza cha kila mgombea urais kiwe ni uwezo wake na mwelekeo wake katika kupambana na uozo huu.”

Mimi nakubaliana naye kwamba kigezo hicho kilikuwa muhimu miaka 20 iliyopita alipoandika makala hiyo, lakini nasisitiza kwamba bado kigezo hicho ni muhimu mno katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu; kwani tatizo limekuwa kubwa mara 20 zaidi kuliko lilivyokuwa zama hizo. Na ndiyo maana, binafsi, nawapima Magufuli na Lowassa kwa kigezo hicho. Mwenye nafuu katika hilo huyo ndiye nitampa kura yangu Oktoba 25, na naamini inapaswa pia kuwa hivyo kwa wengine wote wenye mapenzi ya kweli na nchi hii.

Bahati nzuri (kama unaweza kuiita bahati nzuri) ukiwasikiliza wakihutubia mikutano yao ya kampeni ni vigumu kuwaelewa Magufuli na Lowassa wanaegemea upande gani katika siasa za dunia hii – yaani Kushoto au Kulia au Kati au Kati Kulia au Kati Kushoto. Hivi sasa wanahenya majukwaani na kutoa jasho wakiahidi kuwa watafanya hiki na kile wakiingia Ikulu. Mmojawao (Lowassa) wala hata hahangaiki kuwafafanulia wapiga kura ilani au sera za chama chake (Chadema) ambazo kwazo atazisimamia akiingia Ikulu.

Kwa hiyo, kwa kuwa hatuwaelewi wakiingia Ikulu wataielekeza Tanzania yetu upande gani katika siasa za dunia hii, na kwa kuwa pia wakiwa majukwaani hawazungumzii sana ilani na sera za vyama vyao, wanatubakishia kigezo kimoja tu kikubwa cha kuwapima – nacho ni uwezo wao wa kupambana na ufisadi na mmomonyoko wa maadili. Katika makala yake hiyo ya zaidi ya miaka 20 iliyopita, Jenerali ameandika: “Ndiyo maana hatutakiwi kufanya mchezo katika kuchagua viongozi wetu”. Nami nasisitiza leo - zaidi ya miaka 20 baadaye ya kwamba tusifanye mchezo katika kuwapima Lowassa na Magufuli. Natutumie kigezo hicho kuwapima.

Tukipuuza na kufanya mchezo na kushabikia ule ujinga wa baadhi yetu kwamba eti tufanye tu mabadiliko hata kama tunayemwingiza Ikulu ni shetani, tutakuja kujuta kwa sababu tutamwingiza Ikulu ‘Bw. Changamkiatenda’; yaani rais ambaye atataka kujichotea ten percent katika kila mradi mkubwa wa serikali – uwe ni wa ujenzi wa barabara au ugawaji vitalu vya gesi asilia nk. Kwangu mimi - kati ya hao wawili – Magufuli na Lowassa, sipati taabu mno kumtambua ni nani anayeweza kugeuka kuwa ‘Rais Mchangamkiatenda’ akiingia Ikulu.

Yule mwenye ugonjwa wa kupenda kujilimbikizia mali… yule ambaye amejilimbikizia mali nyingi katika muda wake wa uongozi serikalini ndiye mwenye uwezekano mkubwa wa kugeuka ‘Rais Mchangamkiatenda’ akiingia Ikulu! Vyovyote vile, tusibabaishwe na ahadi zinazowatoka midomoni wakiwa majukwaani wakati wa kampeni; bali tupime na kuangalia iwapo maneno wanayoyatamka kuhusu vita dhidi ya ufisadi yanatoka kweli mioyoni mwao au ni usanii mtupu. Vita dhidi ya ufisadi si jambo la kufanyia usanii hata kidogo. Matatizo makubwa yanayowakabili wananchi na taifa hili yangekuwa yamepungua kwa asilimia 50 kama taifa lisingekuwa linatafunwa na kansa hii ya ufisadi na kumomonyoka kwa maadili.

Na ndiyo maana nakubaliana na kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliposema, wiki iliyopita, kwamba ufisadi nchini unasababisha asilimia 30 ya bajeti ya nchi kuishia mifukoni mwa vigogo serikalini na maswahiba wao nje ya serikali – yaani wachezaji wenzao wa ile timu ninayoiita mimi Mafisadi United!Nihitimishe safu yangu ya leo kwa kusisitiza tena kwamba wapimeni wenyewe Magufuli na Lowassa kwa kutumia akili zenu wenyewe za kuzaliwa na zile za kuambiwa, na kisha fanyeni uamuzi sahihi unaotokana na kuwajua vyema wote wawili.

Jiulizeni wenyewe ni yupi kati ya Lowassa na Magufuli anakidhi kigezo kile cha kwanza alichokizungumzia Jenerali yapata miaka 20 iliyopita.Jiulizeni:Ni yupi ana uwezo, mwelekeo na dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi akiingia Ikulu? Ni Edward Lowassa au ni John Magufuli?Jiulizeni hayo; maana itakuwa balaa kumsindikiza kuingia Ikulu ‘Rais Mchangamkiatenda’. Binafsi – hata nitukanwe vipi kwa simu, sms na emails, siko tayari kumsindikiza Ikulu rais wa sampuli hiyo. Tafakari.

Chanzo: Raia Mwema

Wapi umewahi kupasikia vita ya ufisadi inapiganwa kwa maneno?je tangu tumeanza kupigana vita hii chini ya uongozi wa general Dr.Slaa tumepata mafanikio gani zaidi ya kuwa Kelele za mlango?
 
Lowassa na wenzie ni genge la wezi wakubwa ila tunamshukuru Mungu kwani hawatakaa waione Ikulu yetu hawa majizi
CCM ni chama kilichoshika dola,je meno ya dola yamenyofolewa na nini mpaka tunalia lia badala ya kuchukua hatua.

Kwa kuwa ccm imekuwa ikilia lia badala ya kuchukua hatua dhidi ya mafisadi na mawaziri mizigo,tarehe 25/10 tunachukua madaraka yetu na kuyakasimu kwa mtu mwingine mwenye uwezo wa kuchukua hatua
 
Sisi wa upande wa pili yaani Chadema asilia tutakachofanya ni haya
1) tutafukuza mafisadi na majizi yaliyotoka ccm yarudi hukohuko. Hatuyataki tena kwa sababu yamekuja kuua upinzani
2) tutawataka makamanda waliowakaribisha mafisadi wote wajipime na wakae pembeni. Hiyo ni lazima. Na sio pembeni tuu hata pia tusiwaone maofisini kwetu. Tutakwenda funga makufuli pale ofisini.
3) tutawataka viongozi makamanda watuambie ni hela ngapi walihongwa ili kupokea wageni hao. Kwa sababu tunajua haiwezi kuwa burebure
4) tutataka kujua sasa mapato na matumizi ya fedha za wananchi. Kwa sababu tumeshaona ufisadi upi sana ndani ya chama chetu.
5) hapo sasa tutawaita Dr Slaa na Prof Lipumba waje wabebe na kuibua jahazi lililozama.
6) tutawataka viongozi wa vyama vingine warudi kwenye vyama vyama vyao vinavyokufakufa wasije wakatulaumu tumechangia kuua vyama vyao. Kwa sababu kiukweli vyama hivi Mbowe ameshaviua kabisa hatujui vitaibukaje tena. Wananchi wamepoteza matumaini kabisaaa. Kwa mtaji huu ukiunganisha na wenzetu kwa maslahi mapana ya mama Tanzania tutaweza kufungua mahakama ya mafisadi haraka ili tuwakamate tuanze nao hao. ni hayo kwa ufupi

Tupo pamoja kamanda, mafisadi yametoboa matairi ya gari letu maana mwaka huu CDM ilipewa open check na raia wa nchi hii; wameirudisha bila kuandika kiasi wanachokitaka na Makufuli bila kusita kaiokota na kujiwekea kiasi anachohitaji kama mtaji wa kuanzia!
 
Wapi umewahi kupasikia vita ya ufisadi inapiganwa kwa maneno?je tangu tumeanza kupigana vita hii chini ya uongozi wa general Dr.Slaa tumepata mafanikio gani zaidi ya kuwa Kelele za mlango?

Hivi baraza la mawaziri lilipanguliwa mara ngapi? Na agenda kuu ilikuwa nini na kina nani waliibeba?

Mmechemka mbaya ila Mungu si athimani tumejipatia "mtu" atakaye choma chaka la mafisadi....
 
utafiti wa TWAWEZA unaonesha kuwa 69% ya ambao hawakusoma kabisa ndiyo wanamwunga mkono Magufuli.
 
Hakuna aliyewadanganya CHADEMA waitose ajenda ya ufisadi isipokuwa Lowassa aliwatisha CHADEMA na kuwapa masharti kama wanataka haondoke CCM basi ni lazima kwanza; yeye awe mgombea wa urais, pili waache kutumia ajenda ya ufisadi kwasababu Lowassa alijua CHADEMA / UKAWA wakiendelea kutumia ajenda ya ufisadi na yeye akiwa kama mgombea urais ingalikuwa kazi kubwa kumsafisha kuliko hii ya sasa wanayoifanya...!! Huo ndio ukweli ndugu zangu!!
 
Wapi umewahi kupasikia vita ya ufisadi inapiganwa kwa maneno?je tangu tumeanza kupigana vita hii chini ya uongozi wa general Dr.Slaa tumepata mafanikio gani zaidi ya kuwa Kelele za mlango?

Kama hujui mafanikio ya vita dhidi ya ufisadi mpaka sasa basi hutajua kamwe.

Richmond, EPA, BUZWAGI,n.k

Bila vita ile Lowassa asingetolewa madarakani 2008 na kuondolewa kweny deal zake, bila vita ile marafiki wa Lowassa akina Chenge na Rostam Azizi na Karamagi wangeendelea kutuibia pesa zetu, hii ni vita muhimu sana kwa taifa letu.

Lowassa ni hatari kwa maslahi mapana ya taifa
 
Agenda ya uchaguzi wa mwaka huu kama ni ufisadi basi ccm itaondoka madarakani saa 4 asubuhi.

Kama tunalazimishwa tuendelee kuamini fisadi ni Lowassa peke yake ili Ccm ibaki madarakani tunalidanganya taifa.

Wezi wa Epa, kagoda, escrow , waliouza nyumba za serikali na kuleta kivuko cha MV Dar es salaam kikiwa chini ya kiwango kulingana na pesa iliyotumika kukinunua, leo nao wanaomba urais tunacheka tu.

Juzi wamepitisha mafuta na gesi kwa hati ya upepo tena bila uoga leo tunawachekea tu, sitakuwa sehemu ya ujunga huo nitamchagua Lowassa fisadi mmoja kuliko kuchagua mafisadi 100000 yaliyobaki ccm mtanisamehe.

Nani mtuhumiwa wa escrow anayegombea urais? Nway Rais ni taasisi kubwa sana kwa nchi kama tz, na tz ni nchi rahisi sana kurekebisha huu uozo..mafisadi 100,000 wa CCM wakiongozwa na mtu makini watakula walichovuna na nchi kusonga mbele kuliko taasisi hiyo apewe fisadi mmoja na genge lake lililo kwenye giza (hata hatuwajui ni kina nani wako nyuma yake Ukitoa wachache kama karamagi, rostam, mengi,), na chama ambacho kinaonyesha udhaifu mkubwa katika kusimamia kile ilichokiamini, chama ambacho hakiwezi kumdhibiti mh. Lowassa kama mtu binafsi aliye taasisi na akiwa rais itakua vibaya zaidi...
Tusifanye mzaha na kua wapuuzi urais tz ni ufalme na bado tuna nafasi Nzuri ya kurekebisha uozo huu kwa kutochagua mtu anayeona aibu hata kusema neno ufisadi...
 
Ondoa chaka ndugu yangu, agenda ya ufisadi iko pale pale tulia next wiki Lowassa atakavyowafumua na ufisadi wa gesi na mafuta ulioletwa kwa hati ya zima moto! Kura zitaamua nani Rais.
 
Too late. Labda baada ya uchaguzi. Wakati huo jahazi litakuwa limeshazama.
 
Back
Top Bottom