Nane nane

Nane nane

heroone

Member
Joined
Dec 15, 2011
Posts
24
Reaction score
3
Msingi wa sherehe na maonesho ya kilimo (nane nane) ulikuwa ni kutekeleza kwa vitendo falsafa ya Nyerere kuwa Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi ndio maana akaanzisha siku hii maalum kwa heshima ya wakulima kama iliyo Mei mosi kwa wafanyakazi lengo ni kuwapa fursa wakulima kutoa kero na mawazo yao kwa serikal ili kujenga taifa moja lisilo na matabaka. Kwa sasa nchi si ya wakulima na wafanyakazi tena bali ni ya wafanya biashara na viongozi mafisadi na wauza madawa ya kulevya wachache. Wakulima hawathaminik tena, hawana masoko ya mazao yao, bei ni mbaya na miundombinu hafifu. Je kuna haja ya kuendelea na nane nane iliyogeuka ulaji, katka nchi hii ya wamwaga tindikali?
 
umelenga kuongea kiti gani hasa kwenye uzi huu
 
umelenga kuongea kiti gani hasa kwenye uzi huu

tukiangalia sasa nchi ilivyoshikiliwa na wafanyabiashara na mafisadi. Na wakulima kila siku matatzo hakuna masoko, pembejeo hazieleweki, kila kitu majanga... Nin umuhmu wa nane nane kwa sasa?
 
Back
Top Bottom