Huyo Bwana alizaa na dada yangu mwaka 2003, lakini wakati wanazaa huyo mtoto hawakuoana, yani kwa kiswahili cha sasa alizaa na dada yangu nje ya ndoa. Huyo Bwana walizaa huyo mtoto wakiwa Mlandizi, Pwani. Bwana alikuwa anafanya kazi eti Dawasco/ingawa naye hakuwa mkweli kwa dada yangu kwa miaka hiyo. Baada ya kuzaa na yule dada yangu ndani ya wiki 1 mtoto kuzaliwa akamtelekeza dada yangu akarudi kijijini/ Tanga tangu 24.08.2003 hadi sasa ni miaka 15 hatujui alipo. Yeye baada ya yule mtoto kuzaliwa alimpa jina tu la Ibrahim, baada ya hapo mpaka sasa kimyaaa. Mtoto saivi amefaulu STD VII anatakiwa ajiunge na form 1 - 2019 ni mtoto wa kiume. So popote pale alipo if is still alive anitafute mimi ni mjonba wa huyo mtoto.