Namtafuta shemeji yangu JUMA IDDI

Namtafuta shemeji yangu JUMA IDDI

Magita

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2013
Posts
319
Reaction score
144
Huyo Bwana alizaa na dada yangu mwaka 2003, lakini wakati wanazaa huyo mtoto hawakuoana, yani kwa kiswahili cha sasa alizaa na dada yangu nje ya ndoa. Huyo Bwana walizaa huyo mtoto wakiwa Mlandizi, Pwani. Bwana alikuwa anafanya kazi eti Dawasco/ingawa naye hakuwa mkweli kwa dada yangu kwa miaka hiyo. Baada ya kuzaa na yule dada yangu ndani ya wiki 1 mtoto kuzaliwa akamtelekeza dada yangu akarudi kijijini/ Tanga tangu 24.08.2003 hadi sasa ni miaka 15 hatujui alipo. Yeye baada ya yule mtoto kuzaliwa alimpa jina tu la Ibrahim, baada ya hapo mpaka sasa kimyaaa. Mtoto saivi amefaulu STD VII anatakiwa ajiunge na form 1 - 2019 ni mtoto wa kiume. So popote pale alipo if is still alive anitafute mimi ni mjonba wa huyo mtoto.
 
Dingii pambana ya hela yote dogo aende sekondary.huyo ni mjomba wako(mwanao).

Huyo shemeji sio wa kutafuta,anatakiwa awatafute yeye maana aliwajosea.
 
Ni sawa Mr. Mkorinto nitamsomesha ila nimeona ngoja kwanza nijiridhishe kumtafuta if failed basi.
 
Aiseee hii heading imenistua sana, Nina mjomba angu ndo jina Lake hilo hilo na anawatoto mpaka wengine hawafahamu, tofauti ni kwamba yeye siyo mtu wa songea na wala hakuwahi kufanya Kazi huko...kama angekua kapita huko ningekutafuta pm.
 
Kama ungeweza kutaja jina lake la tatu ingekuwa rahis, kina juma idd wapo weng
 
Aiseee hii heading imenistua sana, Nina mjomba angu ndo jina Lake hilo hilo na anawatoto mpaka wengine hawafahamu, tofauti ni kwamba yeye siyo mtu wa songea na wala hakuwahi kufanya Kazi huko...kama angekua kapita huko ningekutafuta pm.
Mtafute, huwezi jua labda hajawahi kukueleza tu.
 
Juma Iddi atajitokeza wakati Ibra keshamaliza chuo anafanya kazi au amejiajiri na mambo yake ni mazuri. Basi Juma Iddi atakuja na stori nyiingi na kumwomba msamaha Ibra ili maisha yaendelee.
 
Mkuu msaidie tu,anaweza kuja kuwa msaada kwako pia baadaye,achana na Baba yake na hili jambo si vema kumshirikisha huyo mjomba yako,atapoteza focus ya masomo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom