Labda yupo Segerea, nakumbuka kuna Chinga mmoja wenzake walisema kapotea, kumbe alikamatwa na mgambo wa jiji wakati anatembeza mazagazaga yake. Alikaa Segerea miezi minne, karandinga hakuna, siku aliyoletwa tena mahakamani hakimu akamuonea huruma akamwachia. Karudi uswahilini kwanza unaweza kucheka kabla hujamuonea huruma. Suruali kakata pensi, ndala miguu tofauti halafu zimechokaa, yaani nchini Tanzania watu wanaoneana sana.