japanese
Member
- Jul 28, 2015
- 13
- 16
Mwaka 1995, CCM ilifanya mambo kama ambayo wameyafanya mwaka huu,mwaka ule CCM iliibuka na mgombea ambaye kiukweli hakuwa kabisa chaguo halisi la wana CCM,Bali alikuwa ni mgombea chaguo binafsi la mwl Nyerere,kwa bahati nzuri kuna mambo mawili makubwa yalitokea kwanza, mwamko wa mageuzi ndani ya nchi ulikuwa mdogo ndio maana CCM waliweza kuja na siasa nyepesi za kuwatisha wananchi hasa wa vijijini, kuwa msipochagua CCM,wakiingia wapinzani wataleta mauaji kama ya Rwanda na Burundi na TV screen za hapa bongo zilijaa propaganda nyingi za namna hiyo.
Pili Mwalimu nyerere yeye binafsi aliibeba dhamana ya kuzunguka nchi nzima kumnadi mgombea wake na nchi ilimuelewa kwani Nyerere ni kiongozi pekee wa Tanzania ambae wananchi walikuwa wanamuheshimu na kumsikiliza.lakini pia ikumbukwe kuwa huyu mgombea aliyekuwa chaguo binafsi la Nyerere nae aliweza kwa uchache kujisimamia kwa mambo Fulani wakati wa kampeni,moja alikuwa na diplomasia iliyokomaa na saikolojia ya kutosha ya kiuongozi iliyomsaidia kutokuchanganya mambo na kutokuwa kama dodoki kuchukua kila analoambiwa na wanaomzunguka.
Bahati mbaya mwaka huu CCM wameyarudia Yale ya mwaka1995,kwanza wanamgombea ambaye ni zao la mpasuko ndani ya CCM yenyewe,kwani kuna wana CCM ambao ni kweli wamekubali yaishe na kundi jingine ni lile la wana CCM ambao wanajiita kula CCM lakini kulala UKAWA hawa ni mkuki wa sumu kwa CCM yenyewe,pili ni tatizo binafsi la mgombea mwenyewe yeye kama anavyosema siyo mwanasiasa kwa hiyo hajui ni wakati gani na mahali gani aseme nini kwa mfano amesikika Mara kadhaa akisema,"vijana msiiondoe CCM madarakani mtajuta,wapinzani wakiingia madarakani nchi itageuka kuwa kama Libya ,haelewi hali halisi ya siasa hapa nchini na duniani kwa ujumla,ni chama chake ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikiwalaghai watu na hatimae sasa malofa wale waliolala kwa miaka mingi sasa wameamka kwa hiyo ilitakiwa diplomasia na saikolojia ya hali ya juu kuwateka tena wananchi,
Tatu waliompendekeza wamemsusia kwani yeye mgombea kwa kujua au kutojua amekuwa akitumia muda mrefu majukwaani kueleza madhaifu mengi ya serikali inayoongozwa na mwenyekiti wake ambayo na yeye pia ni sehemu ya watendaji ndani ya serikali hiyo hiyo ndio maana mwenyekiti amepata ganzi kutoonekana Mara kadhaa kwenye kampeni za huyu bwana na badala yake amepewa watu mufilisi ambao wanakuja na siasa zilezile za kizamani za kuandaa matokeo mezani yasiyo na maelezo ya kutoshakuwashawishi watu kuwa mgombea wao eti atashinda kwa asilimia zaidi ya sitini.
Mimi nilitegemea MTU kama Mkapa kuwa angeongoza timu ya kumnadi huyu bwana lakini pia kwa bahati mbaya mkapa nae hana sifa na ushawishi kama alivyokuwa Nyerere ingawaje yeye ndiye kwa kiasi kikubwa alitumika kumbeba magufuli.Mwisho naiona CCM mwaka huu ikienda kuadhibiwa na wananchi ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakiipigia kura kwani pamoja na nguvu kubwa ya fedha inayotumika,matamasha yanayoandaliwa yakialika wasanii nyota wa nchi kama sehemu ya kuvuta umati mkubwa wa watu bado watu wamehudhuria matamasha hayo na nyoyo zao zimeshindwa kukisamehe chama cha mapinduzi na kila unayemsikia kuanzia mijini na vijijini anasema huu ni mwaka wa mabadiliko, na kuongeza kusema kuwa tutawachagua wapinzani ili dunia ijue kuwa Tanzania bila CCM inawezekana.