Nampongeza sana waziri wa Maji kuongea hali halisi ya upatikanaji wa nyumba Dodoma. Ni ukweli usiopingika kuwa sio rahisi kupata nyumba ya kupanga Dodoma kwani mji huo ulikuwa haujaandaliwa.
Wafanyakazi wengi ambao wamehamia wanaishi kwenye nyumba za wageni huku wakitumia kiasi kikubwa cha hela kwa ajili ya chakula na malazi, kibaya zaidi wengi waliohamia wamehamia bila familia zao kitu ambacho kwa kiasi kikubwa kitamfanya mtumishi tija yake ishuke kwani muda mwingi atakuwa anafikiria familia yake.
Kwa wale ambao wataamua kuhamia na familia zao watapata changamoto moja kubwa ya kupata shule za kuwahamishia watoto wao, na hili ndiyo swali gumu kwa wafanyakazi wengi. Pengine serikali itafute mwarobaini wa matatizo haya ya kujitakia kuliko kuwalazimisha watu kuhama huku wakijua wazi kuna matatizo, serikali ingejikita sasa kuhakikisha kuwa hao wanaohamishwa wanapata makazi bila usumbufu wowote, ni rahisi sana kuagiza na kulazimisha lakini kwa vyovyote vile naamini tija tarajiwa haiwezi kupatikana maana wafanyakazi wengi wataishi Dodoma kiujanjaujanja.
Kwa kuwa viongozi wengi waandamizi wa Wizara wameshahamia Dodoma vi vema sasa kuhahakikisha kuwa tathmini inafanyika ili kubaini changamoto mbalimbali ambazo zipowazi na kuzitafutia ufumbuzi kabla ya awamu nyingine za wafanyakazi kuhamia Dodoma hazijaendelea.