mwambunnyara
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 518
- 208
Wanabodi wenzangu,
Hakika dunia hadaa,nina mpenzi wangu ambaye kwa kiasi kikubwa sana nimekuwa nikimheshimu sana tu,kiasi cha kujitahidi sana kuepuka vishawishi vya hapa na pale.Mtakumbuka mada yangu ya mwisho nilijitahidi kwa udi na uvumba kumkwepa shemeji yangu aliyetaka tunsaliti rafiki yangu,thanks be to God nilishinda jaribu like.
Ni wiki kadhaa zimepita nikijaribu kutafakari kwa kinanini nifanye juu ya kilichonitokea, ilikuwa siku ya Alhamisi mpenzi wangu kutoka mkoani alinitembelea,(tunaishi mikoa tofauti),bahati mbaya sana nilipata safari ya ghafla nikamuacha mpenzi wangu nyumbani kwangu,nikitarajia kurudi J.pili.
Lakini kwa bahati nzuri nikapata fursa ya kurudi Morogoro (ndo ninapoishi) siku ya J.mosi,roho yangu ilikuwa nzito sana siku hiyo,pasipo kujua sababu sikumtaarifu mpenzi wangu kuwa narudi.
Nilinunua zawadi kwa ajili yake nikaanza safari kurudi Moro, cha ajabu nimefika nyumbani Jirani yangu ananiuliza "vipi mwenzio umemwacha wapi?"
Nilishtuka kidogo,nkamuuliza vipi hajafika? Akanijibu tangu mmeondoka wote sijamuona!Nikiwa siamini kinachoelezwa na mpangaji mwenzangu,nikachukua simu yangu na kumpigia nikiwa sebuleni,nikamuuliza habari ya Moro? Bila wasi wasi akanijibu "nzuri za huko!?" tukapiga stori 2,3 nikamuuliza unafanya nini,akanambia anacheck TV sebuleni!
Taratibu hasira zikaanza kunijaa,nikamuaga ili asigundue kwa haraka.
Cha ajabu mpaka giza linaingia hakuwa amerudi,mpaka J.pili majira ya saa nne asubuhi ndo anarudi home, akanikuta sebuleni naangalia gospal songs,aliponiona alishtuka sana,then akapitiliza chumbani,nilimuacha pasipo kumuuliza neno,lakini moyoni nikiwa na hasira sana.
Jioni ilipofika nikamuuliza kwa ustaarabu kabisa aniambie alienda wapi akanambia alienda kuonana na rafiki yake somewhere,nikamwambia kwa vyovyote vile amenisaliti,namimi sitaweza kuvumilia usaliti.Baadaye akanambia anaomba aniambie ukweli,nikamsikiliza.Alichonambia ndo kimeniacha midomo wazi,sielewi nini cha kufanya,(mnishauri kwa hili jamani)
Akambia "kusema ukweli nilienda kwa mganga wa kienyeji,kutafuta kujua kama kweli unanipenda,nimetoa sh.30000,mganga kaniambia unanipenda sana,ila kuna wana wake wengine wanakusumbua sana,amenifanyia dawa na kunichanjia dawa,"Akaishia kunionyesha michale aliyochanjwa maeneo ya mbavuni na mgongoni karibu na kiuno.
Kiukweli sijaamini lakini ndiyo ukweli wenyewe,kaniendea kwa mganga japo nimekuwa mwaminifu sana kwake!What should I do,huyu atakuwa mwema kwangu kweli?, Japo ameomba msamaha sana lakini kichwani kwangu kuna maruruwe mengi mno,sielewi nifanyeje.