KANDA MBILI
Member
- Jul 9, 2012
- 60
- 57
Ndoa inayotarajiwa kufungwa inaweza kuzuiwa kwa pingamizi.Sheria ilishaweka utaratibu maalum wa kuzuia ndoa kufungwa kwa wale wenye malengo ya kufanya hivyo. Badala ya kutumia fujo,mabaunsa na hila zisizo za kisheria kuzuia ndoa au harusi waweza kutumia njia halali ya kisheria na ukafanikiwa kuzuia ndoa kufungwa.
Fujo na hila zisizo za kisheria katika kuzuia ndoa zaweza kukuletea madhara makubwa na hata jinai. Ya nini basi ufanye hivyo wakati ipo namna halali na salama ya kuzuia.Sababu zipi unaweza kutumia kuzuia na mengine tutaona hapa chini.
1.SABABU ZINAZOKUBALIKA KATIKA KUZUIA NDOA KUFUNGWA.
(a) Sababu ya kwanza unayoweza kutumia kuzuia ndoa isifungwe ni kuthibitisha kuwa kuna ndoa nyingine inayoendelea. Muoaji au muolewaji wote kwa pamoja hawatakiwi kuwa wapo katika ndoa nyingine tofauti na hii inayofungwa sasa.
Maana yake ni kuwa mwanaume asiwe na mke mwingine wa ndoa na mwanamke asiwe na mwanaume mwingine wa ndoa.Isipokuwa tu kamamwanaume ni muislam na katika ndoa ya awali alifunga ndoa ya kiislam basi pingamizi hili halitasimana. Lakini akiwa ni mkristo na hapo awali alifunga ndoa ya kanisani basi pingamizi litasimama.
Lakini pia mwanaume akiwa muislam au dini nyingine na hapo awali alifunga ndoa ya serikali ya mke mmoja basi naye ndoa yake mpya itazuiwa kwa pingamizi. Isipokuwa tu kama ndoa hiyo ilishakufa kwa talaka. Hayo ni kutoka kifungu cha 15 cha sheria ya ndoa.
(b) Sababu nyingine ya kuzuia ndoa ni pale panapo ushahidi kuwa mtu anayetarajiwa kuoa au kuolewa ana magonjwa ya kuambukiza. Kama ni mume anataka kuongeza mke basi mke wake wa kwanza anaweza kuweka pingamizi ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza.
Hapohapo ithibati ya tabia mbaya ya mke anayetarajiwa kuolewa nayo ni sababu ya kuzuia ndoa.
(c) Sababu nyingine ni ile iliyoelezwa kifungu cha 14 sheria ya ndoa. Kimesema kuwa pale ambapo watu wenye undugu wa damu watataka kufunga ndoa basi linaweza kuwekwa pingamizi na ndoa hiyo ikasitishwa. Undugu wa damu uliotajwa ni mtu na kaka, dada, mzazi, mjukuu, mtoto wa kuzaa, shangazi, mjomba, na mtoto uliyemuasili( adopt),
(d) Umri mdogo wa muoaji au muolewaji ni sababu ya pingamizi. Aidha nje na sababu hizi sheria inakubali sababu nyingine yoyote ambayo itaonekana ni ya msingi mbele ya macho ya sheria.
2. NAMNA YA KUWEKA PINGAMIZI.
( a ) PINGAMIZI LIWASILISHWE WAPI.
Zipo sehemu tatu ambapo waweza kupeleka pingamizi lako. Kwanza ni mahakamani.Mahakama ya mwanzo au ya wilaya katika eneo lako yaweza kutumika katika kuweka pingamizi.
Pili ni kwa wakala wa usajili,ufilisi na udhamini( RITA).
Tatu ni katika baraza la usuluhishi wa ndoa. Kwa waislamu baraza hili ni BAKWATA na kwa wengine ni ustawi wa jamii. Ofisi za ustawi wa jamii huwa katika makao makuu ya kila wilaya.
Hata hivyo waislamu nao hawazuiwi kutumia ustawi wa jamii katika kuweka pingamizi. Katika ofisi nilizotaja ukifika hapo utaeleza shida yako halafu utaelezwa utaratibu.
(b) KUSIKILIZWA PINGAMIZI NA UAMUZI.
Baada ya kuwasilisha pingamizi haraka iwezekanavyo pingamizi litasikilizwa na uamuzi utatolewa. Kama sababu ni za msingi ndoa itazuiwa na kama si za msingi pingamizi litatupiliwa mbali.
Na katika kusikiliza pande zote zitaitwa kutoa maelezo. Upande unaopingwa ukikaidi kufika basi mlalamikaji atasikilizwa peke yake na uamuzi utatolewa.