mwali wa giningi
Member
- Nov 14, 2013
- 67
- 42
Viamba vya upishi
Manda za sambusa kiachi 40 -50
Mafuta ya kukaangia lita moja
Nyama ya kuku iliyosagwa kilo moja
Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja
Pilipili mbichi iliyosagwa kiasi kama utapendelea
Pilipili manga kijiko kikoja cha mezani
Bizari nyembamba ya unga kijiko kimoja cha chai
Bizari ya mchuzi kijiko kimoja cha chai
Juisi ya ndimu kijiko kimoja cha mezani
Mbogamboga mchanganyiko kikombe kimoja cha chai
Chumvi kiasi
Vitunguu maji vilivyokatwakatwa kikombe kimoja
Kotmiri iliyokatwa vkijiko viwili
Jinsi ya kupika
Pika nyama ya kuku ya kusagwa kwa kutia chumvi, kitunguu saumu na tangawizi, pilipili, ndimu na bizari zote.
Ikikaribia kuiva tia mboga za mchanganyiko. Changanya vizuri kisha ipua na weka pembeni halafu weka vitunguu na kotmiri. Chukua manda zako na weka mchanganyiko wa nyama na kasha funga.
Baada ya hapo weka mafuta jikoni na yakishapata moto anza kuweka sambusa zako jikoni na kanga hadi ziwe za hudhurungi. Ipua na weka pembeni. Sambusa zako zitakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kula sambusa na kinywaji cha aina yeyote na kufurahia ladha yake.
Kwani wataka nn?Najua ntapata ninachotaka humu.
He he he unakumbuka sambusa ama?
He he he unakumbuka sambusa ama?
Yuko bize na ulezi wa mwali wetu!!!Yaani kama nawaona vile, haya huyo dada yako yuwapi?
Yuko bize na ulezi wa mwali wetu!!!
My D. Uko kwenye angle zoote,daahMahitaji ya manda(ule mkate wa sambusa):
Unga wa ngano 1/4 kg
mafuta ya kupikia kiasi
maji ya joto la kawaida kiasi
Chumvi kiasi
Jinsi ya kutengeneza manda:
- Changanya unga na maji kidogokidogo mpaka upate donge la unga,hakikisha haushikani.Kata vidonge vidogo vidogo vingi.
- Sukuma hivo vidonge utengenze vichapati vidogovidogo vingi
- Kisha weka chapati chini,paka mafuta ienee mafuta vizuri,weka nyingine juu paka mafuta mpaka ziishe,OBS:ile chapati ya mwisho ya juu haipakwi mafuta
- Pasha chuma cha chapati moto.
- Ule mlima wa vichapati usukume utengeneze chapati moja kubwa,kwahio utakuwa kama na layers nyingi za chapati.
- Pasha moto kama dakika tano kila upande.
- Kata ncha kutoka kwenye hio chapati,
- Igawe mara tatu/nne inategemea na jinsi utakavyozikunja.
- Chambua manda ziwe moja moja ,zinatakiwa ziwe nyepesi kwahio unahitajika umakini kwenye kuzichambua au unaweza kuziharibu,
- Zifunge/zihifadhi kwenye kitambaa ili zisikauke.
Nyama ya sambusa mahitaji:
Nyama ya kusaga kilo 1
Vitunguu maji 3 vikubwa
kitunguu swaumu kijiko kimoja cha supu
Tangawizi kijiko kimoja cha supu
Chumvi kiasi
Pilipili manga kiasi
Giligilani fresh(Coriander)
Mafuta ya kukaangia 1 liter
Unaweza kuweka mbogamboga nyingine kama unapendelea mfano karoti,viazi,pilipili hoho ila inabidi vichanganywe na nyama ili viive kwanza