Namna ya kurudisha TIN no.

Namna ya kurudisha TIN no.

Madam vivian original

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2018
Posts
503
Reaction score
998
Mko pouwa
Wakuu naomba kujuzwa namna ya kurudisha TIN, mambo yamekua magumu nataka nifunge biashara kwa muda Ila nikirudi sitaki tena kutumia tin no, maana nalipa pesa kubwa wakati wenzangu sasa HV wanapeta tu na vitamburisho vya ujasiliamali,

Mm ndo nilikua wa kwanza kupanga hapo sasa HV nimepata majiran wenzangu wamechukua frem karibu yangu na chaajab wamepewa vitambulisho mm napambana na tin yangu, na mitaji yetu inalingana na wengine wamenizidi mtaji lakin hawalipi kodi TRA mm tu ndie ninae umia,

Naomben ushauri namna ya kurudisha tin, ili nikatafute kitambulisho cha ujasiriamali. mambo yamekua magumu SNA ati
 
Andika barua kwenda Mamlaka ya TRA na H/W (pitisha barua kwa MTENDAJI AU M/KITI WA MTAA/SOKO) yako ukieleza kusudio lako la kufunga biashara.Halafu Afisa wa Biashara atakuandikia barua ya kukiri kupokea maombi yako na kujiridhisha kuwa umefunga biashara ataondoa LESENI kwenye mfumo wao na hiyo barua utaenda nayo TRA kuwakabidhi.Hakikisha unawasiisha LESENI HALALI ULIYONAYO -MANISPAA/JIJI/MJI/WILAYA na CHETI CHA TRA.Mimi nimefunga hiyo kitu mwezi Januari na sasa hivi nafanya mishe zingine.
 
Back
Top Bottom