Namna ya Kumkanda mama aliyejifungua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namna ya Kumkanda mama aliyejifungua

Discussion in 'JF Doctor' started by Bujibuji, Oct 6, 2012.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Naomba msaada, mke wangu kajifungua na niko mbali na ndugu, je nimkandeje? Maji yaweje? Nikande maeneo yepi?
   
 2. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Maji yawe ya moto ila si ya kubabua mkande tumboni,chini ya tumbo,mgongoni,kifuani,na kichwani
   
 3. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Mkuu salaam,

  Nimeona umeuliza suala muhimu nikaona si busara kwangu kupita pasi na kukupa uzoefu wangu,kifupi mi si Daktari bali nina uzoefu na hili ikizingatiwa kuwa mimi ni mzazi.

  1)Chemsha maji kwaajili ya kumuogesha mkeo,weka maji kiasi kwaajili ya kumkandia na kumsafisha maeneo muhimu.

  2)Kwanza anza kumkanda maeneo ya tumboni taratibu taratibu kwa kukandamiza hasa eneo la tumbo la uzazi kushuka chini,fanya hivyo mara kadhaa then endelea kuzunguka nyonga zake halafu mgongoni na maeneo ya mbavu hizi huwa zina wauma wanawake kwasababu hutumia nguvu nyingi katika kupush mtoto.Pia unaweza kuwa unamuuliza maeneo mengine anakohisi maumivu mkande,fanya kwa upole na upendo ili asijisikie kama hasaidiwi,ila usikubali yeye akuambie uache kwa kuwa mkikosea hapo itamletea shida baadae.

  3)Wakati wa kukanda utaona kuna uchafu mzito unamtoka maeneo ya sehem zake za siri,ni uchafu wa kawaida na unatakiwa umkande mpaka uchafu huo utakapo koma si wastani wa siku 30 ama zaidi,uchafu huo huwa unanuka sana lakini kama utakuwa unamsafisha vizuri baadae harufu itakuwa ya kawaida na si kali sana,mvumilie mkeo ndo tunda hilo kakuletea.Msafishe walau mara 2 kwa siku hasa asubuhi na jioni wakati wa kwenda kulala.

  4)Pia msafishe sehem zake za siri kwa pamba ambayo utailoweka kidogo kwenye maji,ingiza ndani kwenye sehem zake za siri na kusafisha kwa taratibu mpaka unapoona pamba unayoingiza inatoka ikiwa safi no usaha wala damu.Fanya hivyo daily mkuu na njia nzuri ya kusafisha nyeti zake muweke ajilaze kitandani then atanue miguu ndipo fanya maelekezo ya juu.

  5)Muogeshe vizuri na apumzike.


  6)Kwakuwa katika kipindi hiki mama huitaji kupumzika kwa muda wa kutosha jitahidi basi pia unamsaidie kufanya kazi nzito nzito mfano;-msaidie kufua nguo zake,nguo za mtoto na usafi ambao unadhani huwa ni lazima afanye yeye kama usafi wa chumba.


  7)Mkuu mwisho hakikisha mama anapata vyakula vya majimaji lakini vya moto moto,kama supu,uji wenye pilipili manga ili imsaidie kutoa maziwa ya mtoto na hakikisheni mtoto mnamfunika muda wote,mtoto hasikii joto kama mtu mzima

  Baada ya kusema hayo,napena kukupa HONGERA za dhati za moyo wangu,Mwenyezi Mungu akupeni hekima katika kumlea mtoto wenu,naamini utamvumilia mwenzio mpaka siku arobaini zitakapokwisha.Simamia vema nyumba yako na usiruhusu yeyote kuharibu malengo yako kwa familia yako.Simama Imara!God bless you!!
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Hongera kwako na mkeo.
  Chemsha maji, yachemke haswa.
  Chukua taulo, chovya majini.
  Bandika taulo tumboni mwa mama sehemu ya chini, kisha kanda ukielekea maeneo ya juu (kuelekea kifuani)
   
 5. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 283
  Trophy Points: 160
  du! mimi nikioa sijui kama nitaweza hivo nazan ndugu zake watakuja kumsaidia
   
 6. MSHARI

  MSHARI Member

  #6
  May 27, 2016
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  AISEE HONGERA KWA HUU USHAURI NIMEJIFUNZA JAPO SI MIMI NILIEULIZA NI MUDA UMEPITA NAAMINI
   
 7. Barbarosa

  Barbarosa JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2016
  Joined: Apr 16, 2015
  Messages: 14,556
  Likes Received: 13,040
  Trophy Points: 280

  Kwa nini anapswa akandwe?
   
 8. Miss Natafuta

  Miss Natafuta JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2016
  Joined: Sep 16, 2015
  Messages: 17,306
  Likes Received: 28,215
  Trophy Points: 280
  KUKANDA KAZI NGUMU SANA
  NUNUA KONDOO
  KATA MKIA CHUKUA MAFUTA YAKE ANYWE
  ATAHARISHA UCHAFU WOTE NDANI YA WEEK ATAKUWA OK
  PIA KUNA NGOZI YA NGOMBE ATAZUNGUSHIA KIUNONI KAMA WEEK TUMBO LOTE LINARUDI
  NAONA UVIVU KUANDIKA NINGEKUAMBIA VIZURI UNGEENDA VINGUNGUTI TU PALE AU MKOANI MACHINJIO YOYOTE ILA NDO HVO AM TIRED
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2016
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,611
  Likes Received: 4,601
  Trophy Points: 280
  Umkande kwa maji ya moto yenye chumvi umkande tumboni unaroweka taulo kwenye maji ya moto yenye chumvi kisha unamkanda tumboni utakuwa unamkanda asubuhi na jioni kw amuda wa siku 7
  akisha maliza kuoga mfunge kanga tumboni ili lipate kurudi tumbo dogo kama la zamani kwa muda wa siku 40 kila anapo maliza kuoga mfunge kanga tumbo ikaze .Uwe unamtengenezea supu ya kuku yenye pilipli kali na uji wa pilipli mtama kwa siku 40 ili aweze kunyonyesha na kutoka maziwa kwa wingi. Kichwani mwake kwenye nywele mwambie afunge pini aweke kichwani isitoke kwa muda wa siku 40.Pini ya mtoto ya kufungia chupi au nepi itasaidia kumlinda na mapepo wachafu wasiweze kumsogelea. Asubuhi akisha maliza kuoga mpikie uji wa piliplimtama na mchana umpikie supu ya kuku yenye pilipili mtama kwa wingi.
   
 10. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2016
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Science ya wapi hii? Hivi kuna muingiliano kati ya womb na stomach/large intestine. Najaribu ku connect tumbo la uzazi na tumbo la kuharisha! Unaotoka ni uchafu wa wapi?
   
 11. Werrason

  Werrason JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2016
  Joined: Nov 5, 2014
  Messages: 12,359
  Likes Received: 37,606
  Trophy Points: 280
  Nikisoma ID ya mleta mada na ya alie-quote-wa post namba mbili
   
 12. lady mmarangu

  lady mmarangu JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2016
  Joined: Dec 7, 2015
  Messages: 293
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 60
  Hahahahaha,afunge pin kichwani!!!are you serious?
   
 13. Kaplizer

  Kaplizer JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2016
  Joined: Apr 27, 2014
  Messages: 469
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  Hongera maelezo yamejitosheleza kabisaa
   
 14. Jmujun

  Jmujun JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2016
  Joined: Feb 12, 2015
  Messages: 975
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 80
  nimeamini we masikini sana ndugu wapo mbali sana hata majirani wanaojua hawapo, ish na watu vzur
   
Loading...