Namna ya Kukomesha Rushwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namna ya Kukomesha Rushwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabi Sanda, Dec 20, 2009.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu,

  Kutokana hali halisi iliyopo nchini mwetu, natumaini wote tunakubaliana kuwa Rushwa ni tatizo kubwa sana nchini na kimsingi tatizo hili linastahili kuitwa JANGA LA KITAIFA.

  Pamoja na juhudi na njia nyingine ambazo zinatumika katika kutatua tatizo hili kama kuboresha mishahara na kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya Rushwa, naomba mliruhusu kupendekeza njia ifuatayo ili kukomesha Rushwa nchini.

  Njia inayopendekezwa ni kufanya marekebisho ya sheria ili adhabu kwa mtu ambaye atatiwa hatiani na mahakama kwa tuhuma za Rushwa iwe ni KIFUNGO CHA MAISHA. Kifungo hiki kiambatane na VIBOKO 30 SIKU YA HUKUMU NA VIBOKO KUMI KILA MWEZI KWA MUDA WOTE MUHUSIKA ATAKAOISHI GEREZANI. Adhabu hii ya Kifungo cha Maisha na VIBOKO itolewe pia kwa wale wote wanaofuja fedha na rasilimali za taifa (Rejeeni Reports za CAG za kila mwaka) na wale wanao tumia madaraka yao vibaya na kulitia hasara taifa letu.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Rah_sputin

  Rah_sputin Member

  #2
  Dec 20, 2009
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umefanya upembuzi yakinifu?
  Wakae ndani maisha kwa gharama za nani?..kumbuka Wahalifu hawa watakuwa si walala hoi wa kulundikwa lupango kama dagaa.Hawa wakaa VIP.
   
 3. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Rah,

  Asante kwa mchango. Naomba nikutoe wasiwasi kwani gharama haitakuwa tatizo kwani baada kama ya watu watatu au wanne kupewa hiyo adhabu lazima nchi itabadilika. Kwangu mimi naamini kuwa adhabu hii ikitangazwa ipasavyo lazima tu tutabadilika. Kwa upande wangu pia kama inawezekana hiyo adhabu ya VIBOKO siku ya hukumu iwe inaonyeshwa LIVE kwenye Televisheni zetu. Pia tutaokoa fedha nyingi sana. Soma vizuri Reports za CAG ili upate picha kamili ya upotevu wa fedha unaotokea nchini mwetu kila mwaka.
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Sheria kali hazina maana kama hakuna mtu wa kuhakikisha kuwa zinafuatwa, hili ndo tatizo, sheria zipo tayari lakini serikali imeshindwa kuzisimamia.
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Bw. Sabi,

  Mimi kwa upande wangu ningekuwa na-call the shots, kitu cha kwanza kingekuwa kudhibiti rushwa kubwakubwa zinazoligharimu taifa mabilioni ya fedha, mathalani kwenye tenda na mikataba. Njia ya kuliondoa tatizo kama hili ni kuhakikisha mfumo thabiti ambapo mchakato unakuwa wa wazi na efficient at the same time, kuwahusisha watu wengi as possible, na ku-employ independent bodies za ku-crosscheck matukio na wahusika etc wakati wowote ule etc..

  Kwa watu wa rushwa ndogondogo za humu kwenye kada za umma zinazohusika na utoaji huduma. Njia pekee ni kuboresha vipato vyao. Inawezekana kwa:
  1. kupunguza watumishi na kuwalipa vizuri. au/ na
  2. kuanzisha mfumo wa mfano wa 'tips' ambazo zitawasaidia watumishi kukata makali ya maisha kufuatia vipato vyao duni.

  Hivi ndivyo nionavyo
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kingeanzishwa kikosi maalum kama ilivyo usalama wa Taifa. Kipewe nguvu kamili na kiripoti kwa bunge la Jamhuri siyo rais. Kikosi hiki kiwe na mamlaka ya kukamata na kushitaki bila kupitia kwa DPP. Kikosi hiki kiwe na ma-agent wa siri, ambao wanakuwa connected na prosecutor in chief wao. Huyu yeye anakusanya ushahidi wote toka kwa agent na kuwapatia waendesha mashitaka wao ambao nao hata agent hawamjui.

  Wakati wa mwalimu, usalama wa taifa walikuwa wanaogopwa sana, kwanza walikuwa hawafahamiki, na pili walikuwa na uwezo wa kukusanya ushahidi na kuupeleka kunakostahili kwa wabadhirifu kuchukuliwa hatua. Kipindi hicho mfanyakazi wa serikali ukijenga jumba la kifahari juu ya uwezo wako wa kipato ujue itajulikana na litataifishwa na serikali na wewe kuchukuliwa hatua kali. Turudi huko sasa, kila mtu amuogope mwenziye kwenye kufanya madili ya haramu. Hapo tutashinda vita.
   
 7. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Abdulhalim na Hofstede,

  Naomba niwashukuru kwa michango yenu mizuri na yenye kujenga. Kimsingi nakubaliana nanyi. Naamini hayo mliyoyapendekeza yakitekelezwa pamoja na kuwa na adhabu kali na zenye kuogofya (kama vile kifungo cha maisha) naamini kabisa Rushwa tutaweza kuikomesha hapa nchini.

  Kwa kuwa hapa JF tuna watu wa UwT na Wabunge tuwaombe wayachukuwe mapendekezo haya na kuyafanyia kazi kwa faida ya nchi yetu. Pia ni muhimu kila tenda ya serikali ya kiwango cha kuanzia angalau shilingi milioni 100 ziwe zinapitiwa na PPRA kwa ukamilifu wake ikiwa pamoja na mikataba kabla ya kusainiwa na pande husika.
   
 8. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mh....hivi wenzetu wamefanikiwa vipi mpaka sisi kila jambo linatushinda?
   
 9. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #9
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  SHUPAZA,

  Uzuri ni kwamba wenzetu hawana mchezo katika suala la rushwa. Mfano mzuri ni China. Tanzania tunaweza. Ni wakati sasa wa kuamua na kutenda.

  Itakapobidi kama mambo hayabadiliki tunaweza hata kufikiria kuwa na ADHABU YA KIFO KWA MAKOSA YA RUSHWA. Kama adhabu ya ATTEMPTED RAPE ni kIfungo cha Maisha kwa nini kosa la Rushwa ADHABU YAKE ISIWE KIFUNGO CHA MAISHA NA VIBOKO VYA KUTOSHA AU HATA KIFO?

  Tuanzishe adhabu hii tuone kama hali haitatengemaa. Ikiwezekana tuwe na MAHAKAMA MAALUM KWA AJILI YA MAKOSA YA RUSHWA NA UFUJAJI WA RASILIMALI ZA NCHI PAMOJA NA UTUMIAJI MBAYA WA MADARAKA.
   
 10. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sabi Sanda,

  Inamaana sisi hatuna sheria nzuri kulingana na wenzetu? je kukomesha rushwa ni suala la sheria tu au na maadili na elimu ya uraia. hapa bado sijaelewa vizuri naomba ufafanuzi please tufanye nini sasa?.
   
 11. I

  Inviolata Member

  #11
  Dec 20, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania imelogwa na Mganga aliyeiroga Tanzania alikufa kwa hiyo hakuna wa kusaidia. Rushwa ni ugonjwa sugu na si rahisi kuutibu. Tufanye kama China tu adhabu kuuawa period, that is the only way hawa watu wataelewa how serious we want Tanzania to be free of corruption!.
   
 12. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Ukiangalia vizuri, wala rushwa wakubwa ni WASOMI, wanajua SHERIA, wana elimu ya URAIA tosha, ila maadili ni ZERO.

  Sikubaliani na kifungo cha maisha au uchapaji wa viboko.

  Dawa ya wala rushwa, hasa hawa wa mabilioni ni KUWAFILISI mali yao yote waanze moja, kifungo cha miaka si chini ya kumi bila msamaha wowote, na kuhakikisha wakitoka jela hawapati kazi yeyote ya UMMA.

  They broke public trust so there's no need for them to be trusted again.
   
 13. A

  August JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kwa kuongezea Dawa ya Kupigana na Rushwa nyingine ni kuchagua Viongozi ambao wanaichukia Rushwa na Uchaguzi wake/kampeni zake hazitawaliwi na Rushwa.
  Ile mazingara ya kutuhumiwa tu kwa Rushwa iwe ni Disqualification.
  Na kama alivyo sema Abduhakim, mikataba yote mikubwa iwe inaridhiwa na Bunge ambayo inaifunga Nchi, sio kikundi kidogo cha Mafisadi wanaingiza hasara nchi, na mingine inapitiwa na kamati za Bunge husika, kama ununuzi wa Vifaa vya Kijeshi, kamati ya Ulizi, Ujenzi wa Barabara kamati ya Miundo Mbinu, mikataba ya Madini kamati ya Madini, na ikiwezejkana kamati ya sheria iwe inapitia Vifungu vya Sheria, na Kamati ya fedha kuangalia impact ya huo mkataba kifedha. nk nk.
   
 14. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Kwanza unalotaka haliwezekani kwenye jamii yenye sheria, hayo ni mambo ya Gestapo wa Hitler au KGB wa Soviet Union.

  Pili kitakachotokea ukiwapa hao watu nguvu zote hizo wataishia kuzitumia vibaya, wao ndo watakua wala rushwa namba moja, sana sana utahamisha ulaji tu.
   
 15. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Tufanye kama alivyofanya Rwalings nchini Ghana. JK achukue maamuzi magumu ya kuwakamata wote wanaohusika kwa sababu mahakamani watahonga na kushinda. Wapelekwe uwanja wa Jangwani mbele ya macho ya wananchi wote halafu wapigwe risasi na firing squad tuone kama kuna mtu ataipenda rushwa. Aanze na yale magogo. Mwaka 1967 Nyerere aliwahi kuwaleta akina Kassim Hanga na akina Otini Kambona na kuwasuta mbele ya mkutano wa hadhara pale Jangwani na akasema yoyote anaetaka kupindua Tanzania hatafanikiwa. Labda atokee mwenda wazimu ampige risasi. Kwa wale wanaJF ambao mlikuwa hamjazaliwa kasomeni historia.
   
 16. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Be careful what you wish for, you just might get it!
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Imagine you get caught first!
   
 18. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #18
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Pia China ina rushwa sana tu, angalia corruption index ya Transparency International, hiyo adhabu ya kifo haijasaidia chochote.
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  We have to have other mechanism za kudhibiti rushwa.Kama provision ya kuua ikitolewa halafu wakatokea watu kama kina ACM mbona tutakoma hapa.Watazima wapinzani wao kwa kisingizio ni wala rushwa
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Lakini si wka kiwango cha kutisha kama chetu
   
Loading...