Pilipilihoho
JF-Expert Member
- Jan 29, 2016
- 202
- 145
Mahitaji muhimu
Nyanya kubwa 2
Vitunguu maji 3
Karoti 3
Pilipili hoho ya kijani 1
Pilipili hoho nyekundu 1
Tango 1
Kotmiri 1/2 fungu (1/2 kicha) au 1/2 bunch
Majani ya iliki (parsley) 1/2 fungu (1/2 kichana au 1/2)
Cerely vijiti 4
Chumvi kiasi
Ndimu kiasi
Jinsi ya kuandaa/ kutayarisha
1. Osha mbogamboga kwa kutumia maji safi ya uvuguvugu (pendelea kuosha saladi kwa kutumia maji ya namna hii ili kuua vijidudu)
2. Katakata vitu vyote isipokuwa ndimu, kisha uweke katika mashine ya kusagia chakula ( yaani food processor)
3. Weka namna mbili kwenye mashine yako kisha saga mchanganyiko wako kwa kusita kila baada ya sekunde 1 mpaka kachumbari yako ichanganyike vizuri.
4. Ikishachanganyika vizuri, weka maji ya ndimu kisha changanya na kijiko, tia ndani ya bakuli tayari kwa kuliwa.
Vilevile waweza kutumia brenda kwa ajili ya kusagia, hakikisha usisage kwa muda mrefu ili isiwe majimaji sana. Hivyo nio namna ya kuandaa kachumbari mchanganyiko.