Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Ilikuwa ni mwaka 2000.Wakati huo,nilikuwa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Ruvu,Kibaha Pwani. Siku moja, katika mwezi Septemba,alikuja mgombea wa CCM: Benjamin William Mkapa.
Alipokuja,akiwa anamalizia muhula wake wa kwanza na kuomba wa pili,angalau nasi tulikula ubwabwa mfululizo shuleni. Na soda tukanywa. Nikiwa na umri wa miaka 18,niliamini ubwabwa na soda ni kishawishi tosha cha kumchagua Mkapa. Kweli nikampigia kura na Mgombea Mwenza wake,Hayati Dr.Omar Ally Juma.
Nakumbuka ahadi mbalimbali za mgombea-Mkapa alizozimwaga shuleni kwetu. Mojawapo ilikuwa ni kulirejesha bwawa la samaki shuleni hapo.Pia,aliahidi kufanyia ukarabati mabweni ya shule yetu (ya wasichana na wavulana).
Hakukutekelezwa hata ahadi moja hadi namaliza kidat cha nne mwaka 2001. Isitoshe, mgeni rasmi katika Mahafali yetu ya mwaka 2001 shuleni hapo Luteni Mstaafu Yusuph Makamba (wakati huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar) alimimina ahadi kama za Mkapa na nyinginezo.
Hadi leo,naikumbuka ahadi moja kubwa ya Makamba.Aliahidi kusimamia kwa namna yoyote ujenzi wa stendi ya kusubiria mabasi pale shuleni.Ilipaswa kuwa kandokando ya barabara ya Morogoro katika kituo cha shule.
Hadi leo kimya. Naamini,Luteni Makamba anapita mara kwa mara eneo hilo. Labda kama amesahau. Badala yake, JKT wamejenga sehemu ya vinjwaji na chakula.
Baada ya hayo yote pamoja na ya Mbunge wetu wa zamani Dr.Ibrahim Msabaha,nikiri kuwa sikuwahi tena kuichagua CCM katika chaguzi za 2005 na 2010. Na sitarajii kufanya hivyo mwaka 2015.
Nimejifunza kutochagua chama,ubwabwa wala soda. Nitachagua watu wenye uwezo na wenye nia ya kutupeleka mbele kimaendeleo. Uzuri wake tunawajua.Tutawachagua.
Kiukweli, ubwabwa na soda za Mkapa ziliniponza!