Namba hii 0752 733557 inatumika kuibia watu

Aljazeera

Senior Member
Jun 27, 2006
128
43
Namba tajwa hapo juu inatumika kuwaibia wateja wa vodacom M-Pesa na M-Pawa.

Wanapigia wateja na kujifanya ni wawakilishi wa Vodacom, watakupa info zote kukuhusu na pia watakwambia umeshinda zawadi za mpawa


Tunaomba muwe makini na tunaomna wahusika wachukue hatua
 
Ili uweze kushinda shindano lolote lile:ni
1.Lazima utaratibu wa kushiriki uwe wazi na kujulikana
2.Umeshiriki ktk shindano kwa kuzingatia vigezo na masharti
3.Utaratibu wa kutafuta mshindi uko wazi na kusimamiwa na balaza la bahati nasibu la taifa.

Sasa;
Unawezaje kushinda bila mtu kushiriki?
sasa kama umeshinda kwa nini unatakiwa kulipia kabla?

UTAPELI HAUTAKAA UKAISHA DUNIAN MPKA PALE WANAO PENDA KUTAPELIWA WATAKAPO KATAA
 
Kuna mtu aliniambia kuwa namba hii 0788 69 25 00 pia ya utapeli,

Nadhani namba za utapeli si moja tu, na matapeli siku hizi wamebuni mbinu nyingi sana, wanaweza kutumia mabinti wazuri -wazuri kuomba pesa, au hata nafasi ya kazi kwa kukuahidi kukupa kazi, so muwe makini.

hiyo namba ukiicheki WhatsApp kuna binti fulani hivi ana asili ya shombe-shombe hivi, so huyu jamaa yangu alitapeliwa pesa kipumbavu sana.
 
Nina maswali tafadhali.....
1- Wewe umejuaje kama ni tapeli?
2 - Nini kimetokea hata utuaminishe ni namba ya tapeli?
3 - Itapendeza kama utaweka moja ya vithibitisho ili tuamini kwamba huyo ni tapeli.
4 - Je ikiwa umetofautiana na huyo mwenye hiyo namba na ikawa umeamua kumchafua tutajuaje?
 
Mimi ngoja niipige kabla hajanipigia ili ajue na mimi ni tapeli naleta mrejesho nikifanikiwa kumtapeli
 
Back
Top Bottom