Nakutamani moyoni, kidosho nakulilia

feysher

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
2,656
2,762
Nakutamani moyoni, kidosho nakulilia,
Nakupenda siutani, hakika hunivutia,
Dumu nami maishani, pamoya tukasalia,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Huba ongeza mvuto, yawe laini ja pamba,
Kwetu yawe motomoto, yawake kama maramba,
Tuwe sawa kwa mpito, tufungane kwayo kamba,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Niahidi kuyalinda, mahaba yetu wawili,
Namba wani kunipenda, katu nisiwe wa pili,
Hata milima kipanda, mapenzi yawe kamili,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Nifanye wako uhai, kila tyimu nipumue,
Kuishi nami tumai, mie wako kupendae,
Sio Machi si Julai, mahaba tupalilie,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Nami takupenda hani, sitokuacha milele,
Takuzamisha hubani, tulivu bila kelele,
Damuni na fuwadini, pate hanjamu belele,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Waseme menipa dumba, siti nitakuwa wako,
Tujuane kwa vilemba, kwao vibaki vituko,
Nitakuwa lako shamba, vuna huba sosumbuko,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Nina mangi yakusema, ila penzi lanizidi,
Kalamu yakwamakwama, damu yawaka shadidi,
Yanibidi kutuama, kumipenda niahidi, Sauti Njiwa natua, moyo wangu wakupenda.
 
Kidosho kuna mtu kachizika nawe huku na kukutongoza hawezi,akikuona na kimada mwengine anabaki kuvimbisha mashavu tu na salamu haitikii.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Shairi lako ni Zuri, hakika nimelisoma,
Feysher toto zuri, si utani unanona
Mlevi mwenye kiburi, hakika nimekuona,
Pm yako toa kufuli, rohoo iweze pona

Kwako pombe nitaacha,huo uongo natania
Pombe kwangu malkia, hakika naizimia
Kuiacha najikaza, mawazo inaondoa
Mtoto ninakupenda, kwa hilo usijepinga,
 
Shairi lako ni Zuri, hakika nimelisoma,
Feysher toto zuri, si utani unanona
Mlevi mwenye kiburi, hakika nimekuona,
Pm yako toa kufuli, rohoo iweze pona

Kwako pombe nitaacha,huo uongo natania
Pombe kwangu malkia, hakika naizimia
Kuiacha najikaza, mawazo inaondoa
Mtoto ninakupenda, kwa hilo usijepinga,

uko vizuri mkuu
 
Sijui kwanini huyu bazazi hajawahi kuwa na lugha tamu kwangu kama hii.
Nakutamani moyoni, kidosho nakulilia,
Nakupenda siutani, hakika hunivutia,
Dumu nami maishani, pamoya tukasalia,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Huba ongeza mvuto, yawe laini ja pamba,
Kwetu yawe motomoto, yawake kama maramba,
Tuwe sawa kwa mpito, tufungane kwayo kamba,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Niahidi kuyalinda, mahaba yetu wawili,
Namba wani kunipenda, katu nisiwe wa pili,
Hata milima kipanda, mapenzi yawe kamili,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Nifanye wako uhai, kila tyimu nipumue,
Kuishi nami tumai, mie wako kupendae,
Sio Machi si Julai, mahaba tupalilie,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Nami takupenda hani, sitokuacha milele,
Takuzamisha hubani, tulivu bila kelele,
Damuni na fuwadini, pate hanjamu belele,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Waseme menipa dumba, siti nitakuwa wako,
Tujuane kwa vilemba, kwao vibaki vituko,
Nitakuwa lako shamba, vuna huba sosumbuko,
Nipe ahadi mpenzi, daima hutoniacha.

Nina mangi yakusema, ila penzi lanizidi,
Kalamu yakwamakwama, damu yawaka shadidi,
Yanibidi kutuama, kumipenda niahidi, Sauti Njiwa natua, moyo wangu wakupenda.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom