Nakupenda Tanzania Lakini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakupenda Tanzania Lakini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Apr 22, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wana Jf Naipenda sana Tanzania lakini bado nashangazwa na mipango na mambo yanayoendelea ktk nchi yetu.
  Nashangaa hivi Tanzania tumetowa wapi hii sera mbovu ya ubinafsishaji na uuzaji wa mashirika ya umma?

  Kwani nikiangalia nchi kama China ambayo ipo juu kiuchumi imejitahidi mpaka sasa kumiliki kwa asilimia mia mashilika muhimu ya umma

  kwa mfano

  ,(1)Shirika la reli hapa china linaendeshwa na serikali na linaiingizia kipato kikubwa sana nchi
  (2) Viwanja vya ndege vyote na ndege zake zinamilikiwa na nchi hakuna mwekezaji kama tulivyofanya Bongo

  (3) Bandari zake zote zinamilikiwa na serikali hakuna mwekezaji
  (4) Usafirishaji kwa njia ya mabasi ktk miji kwetu tunaita Daladala hapa ni serikali ndio inamiliki kwa kiwangu kikubwa,ingawaje hata watu binafsi wapo lakini mkono wa serikali upo,zamani tulikuwa na shirika la uda tumeuwa na kulitokomeza
  (5) viwanda vikubwa na vidogo

  Hivyo ni vitu baadhi tu ambavyo serikali ya china inamiliki yenyewe pasipo kuwa na ubia na mtu yeyote yule

  Sasa iweje sisi serikali zetu tuna sera za uwekezaji na ubinafsishaji? tumezitowa wapi hizi sera?

  Ok hata kama tunalazimishwa ili tupewe misaada lakini sija wahi sikia nchi ikaendelea kwa misaada,na iweje basi tubinafsishe mashirika nyeti kama Bandari,Umeme,Maji,Reli hivi kweli tutatoka ktk wimbi hili la umasikini kwa mtaji huu?
   
Loading...