Nakupenda nimekusamehe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nakupenda nimekusamehe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by platozoom, Jun 27, 2012.

 1. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  " D..Unaikumbuka siku ile? Takribani miaka 6 iliyopita, nilikutokea.. sikuwa mahiri katika kutongoza bali nilivutiwa na wewe kiasi kwamba nikaingia ujasiri wa ajabu na kuanza kumwaga sera. Ulikuwa mchangamfu na sura nzuri. Kifupi baada ya kunizungusha kwa muda wa miezi miwili hatimaye tukawa wapenzi……Na hapa lazima niseme ukweli : Nilikupenda…na tena siku zilivyokwenda nilikupenda zaidi na wewe naamini ulinipenda hasa katika nyakati za matatizo kwenye mahusiano yetu.

  Sikujali ni nini unafanya kwa ajili ya mapenzi yetu lakini la msingi nilihakikisha unakuwa na furaha. Sikuwa na pesa nyingi…kazi yangu ndogo na kipato cha kawaida.

  Hatimaye tukafunga ndoa, furaha iliyoje kwamba sitahangaika kukutafuta. Napokuhitaji nakupata..sina mashaka yeyote.
  Kadri siku zilivyokuwa zinakwenda ukaanza kunionyesha rangi yako nyingine nisiyoijua: Mkali,mkorofi hutaki kunisikiliza unalotaka wewe ndilo unataka lifanyike….Nikajua kwa sababu nakupenda sana ndio maana unanitendea hivyo…Lakini nilikuvumilia kwa sababu nimejifunza ndoa pia ni kuchukuliana madhaifu yetu. Unajua kabisa tabia yangu, mpole na mcheshi ingawa kuna nyakati chache naweza kukasirika sana…….Unajua kabisa sipendi kuudhiwa lakini uliniudhi na nilikwambia kwa upendo, Acha.

  Muda ulivyoenda nikaona napoteza heshima yangu kama mume. Nikaanza kuhisi napoteza uwezo wangu wa kutafuta riziki……….akili ikaanza kuchoka na pia ndoa nikaanza kuichoka lakini sikuthubutu kuwa na mahusiano nje.  Mbaya zaidi ukanisaliti..Nilipokuuliza ukakataa lakini baadaye ukakubali lakini bila kuonyesha kujuta, na nilikuuliza, Hivi "D" nini unachokosa: Sikutoi out? Huli na kulala vizuri? Nakutesa? Sikupi ngono ya kukutosha?............Yote ulijibu hakuna unayokosa. Sasa nini kinachokusumbua? Ukanijibu "nimeshakuomba msamaha tuendelee na maisha".Niliumia lakini nikakubali yaishe. Laiti kama asingekuwa mtoto wetu Prec…..Pengine ningeshakuacha siku ileile.

  Bahati mbaya siku kadhaa baadaye nikawa na mahusiano na binti mmoja (Ver)..sijui ilitokeaje lakini tulizoeana ghafla….Ni mdogo kwa umri na ndio alikuwa anaingia kwenye ulimwengu wa mapenzi. Alinipenda sana na mimi nikampenda lakini si kama nilivyokupenda wewe. Kadri siku zilivyokwenda nikagundua nilikuwa nakosa vitu vingi sana kwako…

  Pengine kwa miaka mingi sikuwahi kuonewa wivu lakini hapa sikukosa…..Amani hapa niliipata..furaha isyokuwa na mfano, hakuna kuombwa pesa na angalau akili yangu ikarudi kwenye hali yake, mwili ukachangamka. Na hata wewe ulijua kweli nimebadilika kwa sababu sasa sikuwa najali kero zako, sikasiriki hovyo, sina hofu na wala usiponiaga ukaenda kwa marafiki zako sikuulizi. Pia sikuonyesha dharau kwako.

  Ulistuka na nina imani ukaanza kujiuliza….Na hatimaye ukapata jibu, nina nyumba ndogo na jina lake ukalipata. Binti mdogo kwako na mzuri kiasi…lazima nikubali hakushindi uzuri pengine hilo ndilo ulilotafuta kwanza. Lakini ni mchangamfu na yule mama pale CafĂ© akakwambia ni binti mwenye tabia nzuri ingawa wanashangaa kutembea na mume wa mtu!  Kwa hakika baada ya kipindi kifupi ulibadilika na kuanza kuniuliza na mimi nilikueleza kwa upole:
  Binti yule ananipa furaha, amani na upendo naoukosa. Niache niwe na amani, mtoto wetu angependa kuwa na baba mwenye furaha wakati wote na zaidi inanipa nguvu ya kutafuta riziki. Na wewe furahia maisha kwa namna inayokupendeza.

  Baada ya hayo ulilia sana ukawa kama umechanganyikiwa. Ukabadilika sana kitabia nikaanza kukuona kama mtu mpya..mama anayejua wajibu wake…na hata Ibada hukosi, aina ya marafiki pia imebadilika. Unanijali sana, mwanzoni nilifikiri una-act, lakini leo ni mwaka mmoja tokea hayo yatokee na bado umeendelea kuwa mama,mke na rafiki bora. Huwa unaniuliza kuhusu (Ver..) lakini sikupi jibu la kukuridhisha.

  Leo nakuandikia waraka huu kwamba: Nimefunga mahusiano na Ver..Na nitaendelea kukupenda na kukujali daima…wewe ndiye mke wangu kwa shida na raha. Yaliyopita yamepita.
  Nakupenda D"

  Hayajanitokea mimi jamani, ni mjumbe tu kwa shemeji yangu, nimepewa ruksa kulibandika hapa.
   
 2. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Duh kwenye haya mambo bwana hakunaga formula,kwa wengine kuwa na nyumba dogo kungeweza kumfanya mkewe nae apotelee kwingine,alete kale kaungonjwa mwishowe mtoto wao awe yatima.
  Nimejifunza mengi through experience,kikubwa kuliko vyote kwenye ndoa ni COMMUNICATION,kuongea,kuongea na kuongea basi .

  Kama hiyo ili-work out kwao sidhani ita-work out kwa mwingine.Kuwa mwili mmoja kwa watu waliozaliwa na kulelewa katika mazingira tofauti is not a joke
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Mmmh haya bhana!
   
 5. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Unaweza kusamehe? kwa makosa hayo hapo juu
   
 6. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280


  Tena ni mtihani wakati mwingine nakifikiria haya hamu inakwisha!
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Oops Kijasho chembamba ..
   
 8. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
   
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  First laddy A.K.A Nyumba kubwa....unasamehe wewe?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Ndio maana huwa nawaambia member wenzangu wa chama cha Mabachela kwamba ndoa haina formula usiingie na ma-formula yako. Utapigika
   
Loading...