Nakumbushia ili mnikumbushe

Nakumbushia ili mnikumbushe

boyfriendy

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2012
Posts
1,988
Reaction score
1,034
Kuna nyakati fulani zilizopita huyu Mr. Polepole nikikumbuka alishawahi sema CCM ikimsimamisha Lowassa ataenda kuweka pingamizi mahakamani kwa kuwa Lowassa ni mwizi. Bahati kwa CCM hawakumsimika Mr. Lowassa matokeo yake kasimamishwa upande wa pili wa upinzani.

Swali kwa Polepole;

1. Kwa kuwa alishajiaminisha na huenda akawa na ushahidi kuwa lowassa mwizi, je ni sahihi yeye polepole akijifanya mzalendo wa nchi yake kumuacha mwizi akiinyemelea ikulu kwa mlango wa nyuma?

2 . Kwanini asimuwekee yale mapingamizi aliyotaka kumuwekea kipindi akiwa CCM?

Naweza sema huyu Bwana Polepole si mzalendo wa nchi ni mzalendo wa CCM na wenzake maana ukiwa mzalendo wa nchi mwizi ni mwizi ata akiwa chama gani haimuondolei yeye kutokushitakiwa au kuwekewa pingamizi.

Baada ya kampeni kuanza nilikua napata habari kupitia humu humu JF kuwa kuna majopo la majaji sijui wanasheria wanakusanya ushahidi unaomuhusu Mr. Lowassa katika wizi wa Richmond alafu siku si nyingi wataupeleka mahakamani na kumuwekea pingamizi na kumfungulia kesi.

Nauliza tu kampeni zinafungwa leo vipi huo ushahidi bado haujakamilika tu?

Jana nimemuona Mwakyembe Star tv au ndio amepeleka ushahidi star tv?.

Huyu Lowassa ni kiumbe gani mpaka Rais wa nchi na vyombo vyake vyote vya dola vinashindwa kumtia hatiani na kumfungulia mashitaka?

Hivi ni kweli inaingia akilini leo mwaka wa 8 raisi anashindwa kulitamka hata jina la uyo mwizi matokeo yake anapanda juu ya jukwaa na kusema mwizi wa richmond anatembea na boyfrieny kweli jamani ndio tunaonwa malofa na wapumbavu kiasi hichi?

Mungu bariki uchaguzi huu ufanyike salama
 
hapa kazi tu
12122547_903630489718847_713999003090196057_n.jpg
 
Back
Top Bottom