Nakuheshimu sana Mbowe, lakini sasa huwezi, wape vijana walete mawazo mapya

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2016
4,332
10,540
Mbowe ni kiongozi mzuri wa kisiasa katika taifa hili,pia amefanya kazi kubwa katika kuujenga upinzani mpaka hapa ulipofikia.

Mimi binafsi namuheshimu Mbowe kama mtu alie groom viongozi wazuri.Kwa bahati nzuri viongozi hao wanamaono ya hali ya juu.Amefanya kila mbinu safi na pia chafu ili kuikuza CDM.Na kwa kiwango kikubwa amejitahidi vyakutosha.

Amewaibua viongozi kama Mnyika,Mdee,Heche,Sugu,na wengine wengi.Katika mafanikio Mbowe aliyoweza kuyapata kwa kiwango kikubwa nikuaminika ndani ya chama.Mbowe amefanikiwa sana katika hili,chochote atakachosema,amua wanachama walio wengi watamuunga mkono.Na kwa hili kwakweli inafaa kumpongeza maana amewaweka wanachama wake pamoja.

Mbowe aionapo fursa lazima aitumie,tunafahamu ushawaishi alionao kwa kuwahamisha wanachama wengine,kutoka katika vyama vyao na kuingia chadema.Mfano wa wanachama alio wahamisha ni Lissu,Lwakatare,Lema,Msigwa,Prof Safali,Lowasa na wengine wengi.Kafanya yote hayo ili kuikuza taasisi anayoiongoza,kiukweli inapaswa apewe pongezi nyingi.

Lakini Mbowe amekuwa nikiongozi anaependa madaraka,hayupo tayali kuona akiongozwa na wengine hasa katika chama.Mbowe lazima atafakari mustakabari wa chama,atambue anataka sasa hivi kukipeleka chama wapi?.

Mbowe lazima atambue kwa miaka mitano ijayo hatoweza kuiongoza CDM kushika dola.Na pia lazima atambue ushawishi alio nao nje ya chama unazidi kushuka.Lazima kama kiongozi awe anajichunguza anapoelekea atafanikiwa zaidi au ataporomoka zaidi?.Kiukweli kwa maono yangu nafikiri Mbowe asipokuwa makini chama kitamshinda.

Sioni dalili zozote za Mbowe kuandaa viongozi watakao kuja kumrithi,na viongozi nao waona ndani ya chadema kiatu cha Mbowe kitawapwaya.Lakini nafahamu Mbowe anafanya haya yote kwa makusudi ili aendelee kuitawala Chadema miaka takribani 20 ijayo.

Mbowe amekuwa kiongozi asie na maono ndani ya bunge,Mbowe hajui katika bunge yampasa kufanya nini,kwa wakati gani.Mikutano nje ya bunge imepigwa marufuku,nasehemu pekee yakukijenga chama ni ndani ya bunge.

Tunapokuwa na kiongozi asie kuwa na maono yoyote katika kuzua mijadara bungeni,kuleta hoja binafsi bungeni,kutofahamu kanuni nyingi uendeshaji wa bunge,akili yake kutoona fursa haraka yakuzuia baadhi ya hoja bungeni huyo hafai kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni(KUB).

Mbowe nafasi hii inakuchea,nafasi hii huiwezi,nafasi hii ya KUB wewe sio size yako.Lazima utafakari kwa makini nakukaa pembeni katika nafasi hii.Mbowe waachie vijana kama Myika,Lissu,Lijuakali,Bulaya,Mdee waongoze nafasi hii.

Tumeona namna ulivyoshindwa kuhimiri nafasi hii katika miaka mitano iliyopita.Umeshindwa kupeleka hoja binafsi zakudai tume huru bungeni.Umeshindwa kutambua kiu ya wanabadiliko wakweli huanza na nini ili kushika dola.

Mbowe kiukweli bila kumung'unya maneno nafasi hii huiwezi wape damu mpya nao tuone watatufikisha wapi.Sasa hivi hata kuuzungumzia ufisadi bungeni imekuwa kazi kwako,wape uongozi vijana ambao hawakushiriki kumleta Edo chadema.

Waanze kujenga na kurudisha hadhi ya chama bungeni,kama bunge la 2005-2010,ambapo liliendeshwa na hoja juu ya hoja.

Mbowe ninaheshimu mchango wako katika chama,lakini KUB kamwe huiwezi,wape vijana watuletee hoja tunazozihitaji.

Mimi nimetimiza wajibu wangu kwa kukueleza Mh Mbowe nafasi ya KUB achia na wengine.

Ewe mtanzania weka masrahi ya taifa mbele kwa kuwaeleza viongozi wako ukweli.

Note.
Sina kadi ya chama chochote,sio mpenzi wa chama chochote.

Ni mimi mjukuu wa Luhanyula.
 

Mbowe kiukweli bila kumung'unya maneno nafasi hii huiwezi wape damu mpya nao tuone watatufikisha wapi.

CHADEMA wanaweza kupewa damu mpya.Ila hao damu mpya wafanye kazi moja.Waiombe serikali ifute ruzuku kwenye vyama vya siasa.Siku ruzuku ikifutwa CHADEMA siku hiyo hiyo Mbowe atakuwa tayari kukabidhi chama kwa yeyote anayejisikia kukiongoza.Kumwambia Mbowe atoke apishe atoke kwenye chungu chenye pesa (RUZUKU) hapo nisikufiche unampigia mbuzi gitaa.Mangi aachie pesa!!!! Tafakari mwenyewe
 
Kosa kubwa la Mbowe/CHADEMA ni chama kutokuwa na Media mpaka leo hii wala kutomikili majengo yake yenyewe na kutokuwa na asset nyingi zisizohamishika.

CHADEMA walipaswa kuwa na ofisi zao(majengo yao) kwa baadhi ya mikoa au hata mikoa yote.Hili jambo la chama kushindwa ku-invest mpaka leo hii mimi halinifurahishi kabisa.
 
CHADEMA wanaweza kupewa damu mpya.Ila hao damu mpya wafanye kazi moja.Waiombe serikali ifute ruzuku kwenye vyama vya siasa.Siku ruzuku ikifutwa CHADEMA siku hiyo hiyo Mbowe atakuwa tayari kukabidhi chama kwa yeyote anayejisikia kukiongoza.Kumwambia Mbowe atoke apishe atoke kwenye chungu chenye pesa (RUZUKU) hapo nisikufiche unampigia mbuzi gitaa.Mangi aachie pesa!!!! Tafakari mwenyewe
Lazima Mbowe ajiangalie aachie hata KUB abaki kuwa mwenyekiti wa chama tu.
 
Mkuu, kiongozi wa CDM lazima apate baraka za mwenye chama chake mzee Mtei. Nyingine ni mbwembwe tu.
Sasa hivi mzee Mtei kampa chama mkwe wake.
Naamini viongozi wote wa chadema wanachaguliwa kwa kufata kanuni na taratibu.Ingawa pia sifahamu wanamchuguaje KUB.
 
Wakuu...mnamaoni makali.lakin kumbuka kila mtu anayo ayawezayo na mengne acyoyaweza.no one perfect 100% na kama chama cha Mzee mtei.....mlipaswa kuwashauri mnao waamini kuwa waanzishe chama chao....kama zito..so guys themselves they trust mbowe problem ni nyie mashabiki kumtaka awe uñaezani ni bora co hvyo jamani mda ukfka watakuwa
 
Inamaana huoni mbele?
Mwenyekiti wa chama ajaye ni John Heche.
KUB kwa mujibu wa jumuiya ya madola (mfumo wa kibunge) ni lazima awe mwenyekiti wa chama kama ni miongoni mwa wabunge.Kwa hiyo hii nafasi haigombewi wala haitolewi kwa utashi wa mtu
 
Mbowempaka sasa ameshindwa kuziba nafasi ya katibu mkuu huu ni udhaifu mkubwa kwani wote tunajua katibu mkuu wa chama ndio mtendaji mkuu hivyo usione ajabu kwa yanayotokea
 
Inamaana huoni mbele?
Mwenyekiti wa chama ajaye ni John Heche.
KUB kwa mujibu wa jumuiya ya madola (mfumo wa kibunge) ni lazima awe mwenyekiti wa chama kama ni miongoni mwa wabunge.Kwa hiyo hii nafasi haigombewi wala haitolewi kwa utashi wa mtu
Mkuu asante kwa kunifahamisha,lengo ni kupata chama bora kilichokamilik.

Pia kwa nini uamini mwenyekiti atakuwa Heche na sio Silinde au Wenje?.
 
Shida katika Africa watu hawana maono ya kuzalisha viongozi wazuri halafu wawaamini na kuwaachia waongoze wakiwa wanaangalia na kuwakosoa wanapokosea na kuwanyoosha mwisho unawaachia kabisa
 
Back
Top Bottom