Nakshi Nakshi ni wimbo nitakao ukumbuka milele

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Nakumbuka nilikuwa chuo nasoma sikukaa mabibo hostel nilipanga room mtaani, siku moja jumapili a msichana toka mzumbe university alikuja home kipindi hicho alikuwa mpenzi wangu. Akaniambia huna wimbo wa Nakshi Nakshi wa Alikiba nikauweka ukawa una replay wenyewe tu.

Sitosahau uliplay yapata siku nzima halafu yule binti mrembo alikuwa anachezesha kiuno chake akifuata mapigo ya ule wimbo. Siku ile haitakuja kutoka wala kusahaulika ndani ya kichwa changu. Tangu siku hiyo nimshabiki wa kutupwa wa Alikiba yaan nikiona anapondwa najisikia vibaya sana maana alitengeneza wimbo ambao nilipata midungo ambayo sijawahi ona.
 
Kuna vitu ukifanyiwa na mpenzi wako kamwe huwa havisahauriki me mwenyewe kuna wimbo nilikua nikiimbiwa wa Keisha unaitwa mapenzi..... Dah nilikua naona hakuna anayependwa kama mimi duniani
 
Hapo ndio utajua nguvu ya muziki, wengi sana waga either wanafurahi au kuudhunika pindi waskiapo wimbo flani kulingana na memory ya tukio na wimbo husika

mimi ni muhanga wa kuudhunika pindi niskiapo wimbo wa Q-jay, nakumbuka wakati nipo secondary mpenzi wangu alihama shule sasa siku ananiaga akawa anaply nimebaki lonely ya Q-jay na tangu siku hiyo sijawahi kumuona tena, japokuwa ni wimbo unayoniumiza ila sijawahi kuacha kuwa nayo kwenye simu, kila nikibadili simu wimbo wa kwanza ni huo japokuwa waga sitaki ata kuuskia

Muziki haujawahi kumuacha mtu salama kwenye swala la mapenzi
 
Back
Top Bottom