Nakodisha kiwanja 900m2, Bunju B, viwanja vya mradi

Kama kichwa cha habari kisemavyo, nakodisha kiwanja huku Bunju B, 900m2, kwa 400,000/- kwa mwezi, malipo ni miezi 12 (in advance), waweza piga tofali, egesha magari madogo au makubwa, kufuga n.k.

Ni pm please kwenye inbox yangu..

KARIBUNI
Muda wa kukodisha ni miaka mingapi?
 
Mkuu

Hapo kuna mambo mawili ambayo nimeyaona.

1. Kodi ya laki 4 (400,000) kwa mwezi ni kubwa sana kwa hali ya sasa ya kibiashara.

Tambua kwamba kuna kodi ya TRA na kodi ya manispaa vyote vyaningoja. Nijilipe mshahara, na vile vile kuna gharama za kuendesha ofisi.

Ili niweze kukukupa wewe laki nne kwa mwezi lazima niweze kufanya biashara ambayo italeta zaidi ya gross profit ya 3mil.

Sasa, biadhara ya matofali unaweza kupata gross profit ya 3mil kwa mwezi?

2. Kulipa kodi yote ya 4.8mil kwa mwaka ni changamoto.

Sasa hivi pesa imekuwa ngumu mno. Kupata mtu ambaye atakuwa tayari kuchimbia 4.8 mil before biashara haijaanza itakuwa ni ngumu mnoo.

Ungekuwa flexible na kukubali 6 months (ambayo ni 2.4mil), hapo naamini watu wangefanya consideration.

Kwa sababu kutokana na hali ya kiuchumi, biashara zimekuwa za "kubahatisha" sana.
 
Kiwanja unakodisha laki nne? Bunju? Nyumba unafaham wanakodisha sh ngapi hapa Bunju?
 
Kakushangaza sana Tupac
Tupac ni first born wangu. Nna nyumba hapa Bunju B (standard) jirani jirani kabisa na barabara, ina vyumba vitatu, kimoja master, jiko sebule dining na store. Ndani ya fence na ukuta, mpangaji wangu analipa 450,000. Anatakiwa kulipa kodi January ameanza kulia kuwa vyuma vimekaza sana anaomba alipe laki tatu na nusu nimemwambia mwisho laki nne. Sasa huyu ndugu anakodisha kiwanja ambacho hakina hata fence kwa laki nne dah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom