Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,586
- 161,448
Nilidhani watu wa kipato cha chini tumepatiwa mkombozi na voda com,
kumbe sio mkombozi ila ni malaika izraele mtoa roho aliye kuja kwa sura ya upole, upendo na tabasamu huku nyuma yake akiwa na silaha kali yenye kukuua kifo cha taratibu chenye makali na machungu yasiyomithilika.
Nimetumiwa vijisenti kama laki nne hivi , nilipoenda kuvidroo nimekatwa shilingi elfu saba,
jamani....
Hivi ni benki gani ya biashara yenye bank charges za juu kiasi hiki?
Je mamlaka zinazosimamia maswala ya fedha zimeshindwa kabisa kumshauri rostam azizi arekebishe tariff zake??
Kweli rostam kwa sasa ndiye baba wa taifa.
pole sana buji, ila nilidhani anayetumiwa huwa akatwi maana gharama zote za huduma zimelipwa na mtumaji. Sina uzoefu wa kupokea ila nimeshatuma mara nyingi na sijapata mtu amelalamika kukatwa. Hebu wataalam wa hii kitu watupe mwongozo hapa.........inakuwaje???
wakati nilipokuwa chuo, mwalimu wangu wa ds alisema kuwa masikini ni gharama sana kuliko kuwa tajiri. Watu wengi hawakuingiwa na somo hilo. Lakini sasa hivi nazidi kuielewa kauli yake.
Watz wanapenda mambo mdebwedo, wanadanganywa na mambo wasiyotaka kujua undani wake na madhara yake ndio hayo.
Kwanza fikiria, mtu unazo pesa zako badala ya kufungua bank account uwe na uwezo wa kupata mkopo, unakimbilia x-pesa kuweka pesa bila ya riba wala uhakika wa kuomba mkopo kwa kuahidiwa kurahisishiwa mambo ambayo si kweli kuwa unarahisishiwa bali unanyonywa.
Mnapokuwa watu kama 1000 wenye account za x-pesa kila mmoja unaweka tzs 10,000; ina maana x-pesa anakuwa na 10,000,000. Kama hamjazitumia kwa mwezi mmoja na yeye ameweka katika account ya muda maalum kwa kipindi hicho kwa faida ya 6% inamaana anapata 600,000. Halafu anakuchaji 2% kwa kukutunzia fedha zako maana yake atapata 200,000 ambapo jumla yake anafaida ya 800,000.
Hii inamaana kuwa katika kila wateja 1,000 x-pesa atapata tzs 800 kwenye kila 10,000. Sasa wewe unadhani kuwa ni mjanja unaweka 500,000. Ina maana unapoteza 40,000 bila kujua (in-direct charges).
Naomba niwashauri muweke fedha benki na mkifungua akaunti benki unapata faida zaidi ya hasara hizi za x-pesa.
Sorry JF kagoma format yanguPlease angalia jedwali la miaamala katika huduma hii:-
Event From To ChargesTsh
Cash Deposit 5,000 500,000 Free
Send Money To
Registered Customer 1,000 500,000 200
Send Money To
Unregistered Customer 1,000 9,999 1000
10,000 19,999 1,500
20,000 49,999 2,500
50,000 99,999 4,000
100,000 199,999 6,000
200,000 299,999 8,000
300,000 500,000 11,000
Withdraw Money -
Registered Customer
5,000 9,999 350
10,000 19,999 500
20,000 49,999 1,000
50,000 99,999 1,500
100,000 199,999 2,500
200,000 299,999 4,000
300,000 500,000 7,000
Withdraw Money -
Unregistered Customer
1,000 500,000 Free
Mkaa Mweupe said:Wakati nilipokuwa chuo, mwalimu wangu wa DS alisema kuwa masikini ni gharama sana kuliko kuwa tajiri. Watu wengi hawakuingiwa na somo hilo. Lakini sasa hivi nazidi kuielewa kauli yake.
WaTZ wanapenda mambo mdebwedo, wanadanganywa na mambo wasiyotaka kujua undani wake na madhara yake ndio hayo.
Kwanza fikiria, mtu unazo pesa zako badala ya kufungua Bank Account uwe na uwezo wa kupata mkopo, unakimbilia X-Pesa kuweka pesa bila ya riba wala uhakika wa kuomba mkopo kwa kuahidiwa kurahisishiwa mambo ambayo si kweli kuwa unarahisishiwa bali unanyonywa.
Mnapokuwa watu kama 1000 wenye account za X-Pesa kila mmoja unaweka TZS 10,000; ina maana X-Pesa anakuwa na 10,000,000. Kama hamjazitumia kwa mwezi mmoja na yeye ameweka katika account ya muda maalum kwa kipindi hicho kwa faida ya 6% inamaana anapata 600,000. Halafu anakuchaji 2% kwa kukutunzia fedha zako maana yake atapata 200,000 ambapo jumla yake anafaida ya 800,000.
Hii inamaana kuwa katika kila wateja 1,000 X-Pesa atapata TZS 800 kwenye kila 10,000. Sasa wewe unadhani kuwa ni mjanja unaweka 500,000. Ina maana unapoteza 40,000 bila kujua (in-direct charges).
Naomba niwashauri muweke fedha Benki na mkifungua akaunti benki unapata faida zaidi ya hasara hizi za X-Pesa.
Pole sana Buji, ila nilidhani anayetumiwa huwa akatwi maana gharama zote za huduma zimelipwa na mtumaji. Sina uzoefu wa kupokea ila nimeshatuma mara nyingi na sijapata mtu amelalamika kukatwa. Hebu wataalam wa hii kitu watupe mwongozo hapa.........inakuwaje???
Anayetumiwa anakatwa kulingana na kiasi alichotumiwa, that is for sure hata ukienda kwa mpesa agent utaona mchanganuo ulivyo. Labda kwa lugha nyingine ni kuwa unatozwa charge sasa badala ya kutoa mfukoni inakatwa ile iliyotumwa. ina maana jamaa angetoa elfu saba toka mfukoni wangempa laki nne ambayo ni sawa na kupewa 393000 bila kutoa pesa ya mfukoni.....Sidhani kama anayetumiwa anakatwa pesa. best jaribu kuchat na customer care, isijekuwa hao jamaa wamekuingiza town!
i love finance!