Najuta kuanzisha haya mahusiano

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,897
19,080
Kuna wakati unaweza kuanzisha mahusiano kisha badae ukajuta kuhusu hayo mahusiano,unaweza kujuta kwa mema au kwa mabaya ya hayo mahusiano.

Kuna mahusiano nimeyaanzisha ila najuta na natamani bora huyu binti angenikataa, najuta kwa kua naona huyu binti ntakua sijamtendea haki.

Najuta kwa kua huyu binti hakustahili kupata mwanaume kama mimi, najua hajui kama namtumia tu na sina lengo lolote na yeye ila adhabu hii hakustahiki kuipata maana huyu dada ni mtu mwema sana, ni mtu anaejua anafanya nini.

Natamani angenikataa mapema labda angepata mwanaume ambae angejali na kutambua upendo wake, natamani haya mahusiano yasingekuwepo.

Bado sijapata jibu siku akijua kua nilikua namtumia tu bila lengo lolote itakuaje, huyu binti ana upendo wa dhati, najua ananipenda sana na kunijali ila ukweli toka moyoni mwangu sina lengo lolote na yeye.

Kwa ujumla najuta kuanzisha huu uhusiano.
 
Kwasababu umeshamtafuna na umeona uchi wake ndiyo unaona hakufai.............
Wakati unamtongoza ulikuwa umeshapiga kiroba ama......
 
Mkuu...better late than never..mwambie tu ukweli na wewe utakua huru...atakuchukia ila ndo ivo inaitwa thank me later
 
Najuta kwa kua huyu binti hakustahili kupata mwanaume kama mimi, najua hajui kama namtumia tu na sina lengo lolote na yeye ila adhabu hii hakustahiki kuipata maana huyu dada ni mtu mwema sana, ni mtu anaejua anafanya nini.

Natamani mwenza angekuwa anachaguliwa kwa kugongagonga kichwa chake kama tunavyochagua NAZI ili kufahamu ni ipi nazi na ipi Koroma. Kwa kweli wengi tungetupwa dampo.
 
Huwezi kujuta ilhali unaendelea kumko.joza.....

Mwambie ukweli....

Kuna ile methali inasema mkataa Pema.....
 
Acha uzinzi,yatakurudia hayo unayoyafanya huwa hakuna kitu duniani unachomfanyia mwezako kikabaki kama kilivyo na ukabaki salama
 
Kwasababu umeshamtafuna na umeona uchi wake ndiyo unaona hakufai.............
Wakati unamtongoza ulikuwa umeshapiga kiroba ama......
Mkuu, kuna ile nipige nisepe Unakuta binti kakolea... Double coincident of wants inakuwa shida
 
Mkuu, kuna ile nipige nisepe Unakuta binti kakolea... Double coincident of wants inakuwa shida
Mkuu unakosea, yani umenza mahusiano na umjenga na kibanda kabisa leo unataka kukichoma kibanda, je umemwazia mwenzako atalipokeaje hili maana yeye mind set yake anajuwa tayari ana mume wakati wewe mwenzake huna future plan naye hata, ni vyema ukamwambia mapema ili ajipange kisaikolojia......sometime men we are so rude.... Nao hawa ni human being..... Tusijiangali sisi tu

Halafu ngoja nikuambia mkuu mwanamke usio kuwa na plan naye ndiyo huwa perfect na utaishi naye maisha mazuri sana kuliko huyo waku search.... Utakuja niambia, nimeliona hili kwa watu wengi
 
Hata hujakosea aiseeee yaani uko vizuri sana tu mkuu toxic9
 
Back
Top Bottom