Ndugu husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu.
Mimi ni kijana (27) na nimeoa.
Nina mke wangu nimpendaye katika maisha yangu ila kwa anavyonishutuma mimi ni mzinzi, mara malaya , siaminiki, kazi nampa madeni kibao lakini bado naendelea kumsaliti , kazi kuwa na watoto wa nje [emoji22] yaani inafikia hatua nakuwa nampuuza tu na roho yangu inakuwa inatamani niachane naye tu si kwamba simpendi, rahasha nampenda sana na upendo wangu kwake huwa haujifichi , katika enzi ambazo sijaoa kweli nilikuwa na mabinti wengi ila nilivyooa nilianza kuwaacha kwa kuwaambia nimeoa, ila wengine wakawa hawaamini , na mwingine akasema hayuko tayari anikose bora aendelee kuwa nami na haijalishi nimeoa , nami roho yangu nikaifanya kuwa ngumu kweli nikawa naye kwenye mahusiano haswa kwenye handing over ila siku moja nilimla vyombo nakurudi nyumbani , niliporudi nilienda kuoga wakati naoga nimejisahau kama password wife anaijua , akachukua simu akaangalia sms yule mchepuko wangu anavyonishukuru kwa penzi nililompa. Nilikuta mke wangu analia huku akidondosha machozi.
Nilivyofika alinitukana wee , nikamuomba nisamehe yakaisha .
Ila kwa sasa niko mbali naye yeye yuko nyumbani nami niko mwanza yaani kila kukicha lazima tukwazane haswa kwa kunishutuma mara sitaki kuchart nae , yaani sielewi kabisa inafikia stage naamua kuchart nae kinyonge, na nampenda sana ila sitaki anipande sana kichwani , kichwa changu nakijua vema.
Hivi kwa tulipofikia kila kuchapo matusi si tutaachana tu maana mimi hasira zangu najitaidi kuzicontrol lkn yeye anakuwa ananifanyia visa kuwa niko na wanawake wengine .