Naishi nikisubiri kifo, nimechoka sana

Naishi nikisubiri kifo, nimechoka sana

Kila mmoja anaishi kwa kusubiri kifo maana kifo ni lazima.
 
Wakuu habari za mihangaiko .....

Kiufupi nimechoka sana. Maisha yangu siyaelewi nimepambana vyakutosha
Nimejitesa sana ili nipate mafanikio badala yake nimepata shida nyingine vidonda vya tumbo Au ulcers ,

Nime hustle sana nikawa bize mpaka nikaachika na mpenzi wangu niliyempenda sana lakini wapi

Kila nikipiga hatua tatizo linatokea narudi nyuma ,

Nimepaniki sana nimekuwa nakunywa pombe hatari ila bado naona kama bado haziwezi kunisahaulisha natumia kijiti ila bado naona kama hakifanyi kazi vizuri kunisahaulisha malengo niridhike tu na maisha ya kawaida lakini wapi , mimoshi tu inaniletea kikohozi bure.

Sikutamani kabisa nife sijamiliki gari kali mabiashara makubwa mjengo wa maana , ila sasa naona kukata tamaa kukinifunika

Bangi zikinikolea , madawa ya kulevya na kifo kikija mapema , na moto mkali wa jehunum ukinichoma kwa madhambi yangu[emoji24]
Be wise, work smart maisha si magumu.
 
Personal hio hali imenitoka Kama wiki 2 au tatu zilizopita, Mimi ni kijana mdogo ila nilikuwa najipa presha kubwa Sana kuhusiana na maisha

My focus ilikuwa another level kaka,nasoma vitabu na articles zinazohusisha biashara na mafanikio, believed I was here for a big reason

Ila Sasa it's quite different sijui nini kimenikuta cause nafeel happy,japo bado namtafuta Yule Mimi wa zamani.

Kikubwa tuliza akili yako,omba Mungu kwa imani yako(kuanzia saa 6 usiku ) coz Kuna nguvu iliyojificha hapo,pambana mwisho wako bado,jipende na uipende familia yako
 
Unaposema hela ya pombe ipo , nishukuru wakati tayari nipo kwenye depression ambayo unaona kabisa future inaenda kuwaje aisee utani huo ,
 
Acha upumbavu we huna shida mbona. Ishu ya kupigika kiuchumi sio shida. Ungeniambia afya sawa. Kama unadhani una shida nenda hospital ukajiona una mtoto wa shida na sio shida, pana watu wamekatika mikono na miguu walikuwa wazima awali na still wapo happy na matumaini. Pana watu wamepata hasara za mabilioni still wapo na hope. Mimi nimepambana miaka 17 na sijapata hata mia nimepoteza jumla ya milioni 400 na still nipo na hope ya mabilioni na tapata nchi imejaa utajiri wote huu nakuaje masikini sasa.
 
Nadhani jambo la kushukuru kwako kwanza ni kuwa una afya ya kuendelea na michakato ya maisha. Siku ukiumwa ukapata tatizo la kukuweka kitandani miezi 6 utaelewa hii point vema.

Kimsingi, kumiliki gari au magari sio mwisho wa changamoto za kiamaisha kuna gharama ambazo zinakuja nazo ambazo kwasasa hauzioni kama kupambana na matrafiki, manunuzi ya spears, kulipia bima, na mafuta. So si kwamba ni starehe tu ila pia unapata gharama zaidi za kimaisha ambazo utatakiwa uzibebe kama sehemu ya maisha yako.

Nikwambie tu, maisha si vile vitu unatamani bali ni vitu unahitaji. Na kutokana na makuzi yetu tunatofautiana mahitaji. Kila mtu huwa anapewa kile anahitaji ili kuweza kuishi kwa furaha kama wengine.

Jitahidi sana kuelewa hii point, unaweza kuta unakosa amani na unaona haufikii malengo sababu umechukua akili ya watu wengine na kuapply kwenye maisha yako. Kwamba umechukua idea za vitu wengine wanataka umegeuza kuwa mahitaji yako mwisho wa siku hata ukivipata hautafurahia hata iwaje.

Wakati unavuta hizo bangi nakushauri usikilize wimbo wa 20% unaoitwa "tamaa mbaya",sijui kama nakosea jina au napatia. Sikiliza huo wimbo maneno yake ni ya hekima sana na utakusaidia kutafakari maisha kwa level yako. Mimi ulinisaidia sana kuyaelewa maisha na kujipanga upya niliposhuka chini.

Panga upya maisha yako. Kaa chini jiulize hivyo vitu unataka ni hitaji la moyo na maisha yako au ni matamanio baada ya kutazama wengine kuwa navyo. Itakusaidia kujua uanzie wapi na kupata furaha. Watu wanaishi kwa tamaa ndio maana furaha inawatenga muda wote wanabakia kutafuta faraja.

Tamaa na furaha haviishi nyumba moja, chagua kimoja uteseke au ufurahie maisha.
 
Umewahi jiuliza hivi umetumiaje muda wako hapa duniani??? Ikiwa kuna watu ni walemavu na wagomjwa wanapambana ww mwenye afya ukate tamaa kisa mapenzi??? Hebu fikiria wnawake ni wengi kuliko wanaume, watu duniani karibia bilioni 8 kweli ukose hata mmoja???

Kabla hujajiua au kukata tamaa, kama umeshindwa hapo ulipo hebu tafuta passport nenda ukajaribu upepo nchi nyingine....chukua passport tafuta visa nenda hata vietnam au ufilipino huko ukaanze upya utapata challenge mpya na utaanza upya.

Kama huko mbali basi ingia hata hapo Angola au Botswana....dunia ni kubwa sana kuliko unavyodhani
 
Umeingia kwenye tatizo langu , kila mtu ana mtazamo wake wa maisha kutokana na familia aliyotoka na jamii yake iliyomzunguka , kila mtu ana level ya maisha anaitafuta ili awe happy, mwingine 100k anakuwa happy mwingine 2M ndio atakuwa happy mwingine 20M na mwingine above 100M , kwahiyo mtu wa level ya 2M lazima akushangae wewe wa level ya 20M unapokosa furaha kisa umedondoka una 15M , natamani kujiupdate niweke level niliyonayo ndio iwe level yangu , kupanda kuwe ni bahati tu au zali ,

Masaibu ni mengi , bomoa bomoa inikumbe mimi, wezi wanikumbe mimi, ajali ya moto , maradhi , furaha iko wapi ??
 
Umewahi jiuliza hivi umetumiaje muda wako hapa duniani??? Ikiwa kuna watu ni walemavu na wagomjwa wanapambana ww mwenye afya ukate tamaa kisa mapenzi??? Hebu fikiria wnawake ni wengi kuliko wanaume, watu duniani karibia bilioni 8 kweli ukose hata mmoja???

Kabla hujajiua au kukata tamaa, kama umeshindwa hapo ulipo hebu tafuta passport nenda ukajaribu upepo nchi nyingine....chukua passport tafuta visa nenda hata vietnam au ufilipino huko ukaanze upya utapata challenge mpya na utaanza upya.

Kama huko mbali basi ingia hata hapo Angola au Botswana....dunia ni kubwa sana kuliko unavyodhani
Ushauri wako wa kutafuta passport ni mzuri sana ngoja niugongelee kichwani uwe mbadala wa kuharibu akili yangu kwa kijiti na ulevi
 
Kujiua huwa hakutajwi wala kuruhusu kuwaza tu yaani unambip jini makata na subiani watakupigia
 
Back
Top Bottom