Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Amani iwe kwenu wadau.
Kwa viki sasa, zimeripotiwa taarifa na jeshi la polisi zikieleza mafanikio yao katika mapambano dhidi ya Ujambazi na Ugaidi. Taarifa hizo zimetoa takwimu ya watu waliokamatwa na kuuawa katika operesheni ya kupambana na Ugaidi na ujambazo. Idadi ya waliokamatwa kwenye operesheni hiyo kwa mujibu wa polisi ni kubwa na wote waliokamatwa wamekutwa na vitu kadhaa ikiwa ni pamoja na silaha za kivita.
Aidha, kwa siku ya juzi na jana, zimeripotiwa taarifa kuwa magaidi na majambazi watano wameuawa Dar es Salaam na Tanga. taarifa hizo zinasema kuwa watatu wameuawa kwenye mapango ya Tanga ambako walijificha wale waliochinja ndugu zetu huko Tanga. Polisi ilifanikiwa kuwaua watu hao baada ya majibizano ya risasi kwa muda wa masaa matano.
Wiki mbili zilizopita, magaidi watatu waliohusika kuchinja watu Msikitini huko Mwanza nao wameuawa ikiwa ni pamoja na mtu anayesadikiwa kuwa ni kiongozi wao. Nachukua fursa hii kulipongeza jeshi letu la polisi kwa mafanikio waliyofikia. Aidha, niwapongeze pia Watanzania wote wanaojitolea kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ambazo zinawasaidia katika harakati zao.
Niwaombe sana ndugu zangu wa CHADEMA. Waliache jeshi la polisi lifanye kazi yake. Kama walidhani kuwa jeshi la polisi ni kwa ajili ya CCM basi ifike wakati tuwapime akili zao maana inawezekana kabisa wana matatizo ya akili. Hawa waliouawa ni majambazi na magaidi. Polisi wamefanya kazi zao kwa weledi na ufanisi Mkubwa.
Tanzania bila ya Ugaidi na Ujambazi inawezekana. Naamini kuwa mpaka 2020, Tanzania tutakuwa hatuna matukio ya Ugaidi na Ujambazi kama ilivyo kwa majirani zetu wa Rwanda. Kama wao wameweza, sisi tutashindwaje? Ni vema kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa.