Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,323
- 152,136
Watumishi wa umma na vyama vya wafanyakazi mnapaswa kuzinduka tunakoelekea sasa siko.
Wanasiasa sasa wameamua kujisafisha kupitia watumishi wa umma huku wao wakionekana kulindana na bahati mbaya sana watumishi wa umma wamelala usingizi wa pona huku wakiwa wamefunikwa na blanketi la hapa kazi tu linaowatia woga wasithubutu hata kuhoji juu ya haki zao.
Tujiulize hivi nchi hii wabadhirifu na wanaotumia vibaya madaraka ni watumishi wa umma tu?Hivi ni kweli wanasiasa wa nchi hii mpaka sasa hakuna aliestahili kuwajibika?
Hivi karibuni iliripotiwa kuwa wakurugenzi wanaotakiwa kwenda Dodoma kwenye maswala ya Bajeti watatakiwa kusafiri na gari la pamoja na asietaka aende na usafiri wake binafsi kwa gharama zake mwenyewe.
Cha kushangaza,mawaziri,manaibu mawaziri na vigogo wengine wanasafiri na mashangingi tena kila mtu na lake kutoka Dar hadi Dodoma.
Hivi kama hoja ni kubana matumizi,ni kwanini basi mawaziri hawa wasiende Dodoma na RAV4 au magari mengine yenye CC ndogo?
Ukweli ni kwamba,ukiwa Dodoma sasa hivi, wingi wa mashangingi haya hapa mjini unaondoa kabisa maana nzima ya kinachoitwa kubana matumizi kwani ni magari haya ya anasa ya serikali ndio yanatawala hapa mjini.
Leo hii Makonda kaja na mkataba unaotakiwa kusainiwa na maofisa utumishi wa Halamashauri za mkoa wa Dar-es-salaam kuhusiana na watumishi hewa.
Cha kujiuliza,hivi ni kwanini tusiwe na mikataba ya aina hii kwa wateule wa raisi wanapotuhumiwa wawajibike mara moja mfano mawaziri?Makonda nae ana mkataba maalumu wa aina hii kuhusu watumishi hewa na boss wake?
Hivi sasa kuna juhudi kubwa za kukabiliana na watumishi hewa (jambo jema kabisa).Lakini tujiulize, wabunge (wanasiasa) wana sheria inayowalazimisha kusaini mwanzo wa kikao na mwisho wa kikao kabla ya kulipwa posho zao za siku?
Naamini kadri siku zinavyokwenda huu mstari utajidhihirisha kwa wengi.