Naiona CCM ikifanikiwa na kudumu zaidi ya miaka 20 Ijayo

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Ninazitabiria Harakati za CCM zinazoendelea sasa Dodoma kukifanya kuwa Chama chenye nguvu ya kuendelea kubaki Madarakani kwa miaka mingine zaidi ya 20.

-->Ninaona watu wenye mitazamo tofauti na CCM ya awali wakimiminika kujiunga na CCM

---->Mabadiliko ya sasa na Fukuzafukuza hii, Siioni ikiidhoofisha CCM hata chembe badala yake inaonyesha CCM kama chama chenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kikomavu.

----> Ninaona CCM maslahi wakiachana na siasa, na kuanza kujaribu vitu vingine vya kufanya nje ya siasa maana Chama Sio tena sehemu salama ya kutimizia ndoto zao kimaslahi.

---->Ninaona Hakuna Vuguvugu lolote nje au ndani ya chama cha Mapinduzi likiibuka na kufanikiwa kuidhoofisha .

WAPINZANI wa CCM kama wasipobadilika na kuja na mbinu mpya zaidi ya kudandia matukio, mfano leo masikio yamesimama yameelekea DODOMA badala ya UFIPA kwenye meza ya mipango kujiandaa kupambana na CCM mpya ambayo Muda sio mrefu kishindo chake kitapokewa kwa shangwe nchi nzima Wataendelea kudumu zaidi ya miaka 20 ijayo wakiwa na ushawishi huuhuu ulio chini ya wastani na unaotiliwa mashaka kila kukicha...
 
Jamaa kagundua hana mvuto ndani ya chama hivyo imebidi kutumia polisiccm ili wampe kinga vinginevyo chaliii! awamu moja tu. Ngoja tusubiri tuone hawa waliofukuzwa na wale wote ambao hawataki mabadiliko anayoyataka malaika mkuu ili kumpa nguvu zaidi kuelekea 2020 wataamua kupambana naye vipi. Angalia hapa picha ya jana kashindwa kumuangalia Membe usoni kwa unafiki wake.

17202720_1752041818459688_1257049282776818419_n-jpg.479911

Kama haitatumia dola inajifia soon
 
Ninazitabiria Harakati za CCM zinazoendelea sasa Dodoma kukifanya kuwa Chama chenye nguvu ya kuendelea kubaki Madarakani kwa miaka mingine zaidi ya 20.

-->Ninaona watu wenye mitazamo tofauti na CCM ya awali wakimiminika kujiunga na CCM

---->Mabadiliko ya sasa na Fukuzafukuza hii, Siioni ikiidhoofisha CCM hata chembe badala yake inaonyesha CCM kama chama chenye uwezo wa kufanya maamuzi ya kikomavu.

----> Ninaona CCM maslahi wakiachana na siasa, na kuanza kujaribu vitu vingine vya kufanya nje ya siasa maana Chama Sio tena sehemu salama ya kutimizia ndoto zao kimaslahi.

---->Ninaona Hakuna Vuguvugu lolote nje au ndani ya chama cha Mapinduzi likiibuka na kufanikiwa kuidhoofisha .

WAPINZANI wa CCM kama wasipobadilika na kuja na mbinu mpya zaidi ya kudandia matukio, mfano leo masikio yamesimama yameelekea DODOMA badala ya UFIPA kwenye meza ya mipango kujiandaa kupambana na CCM mpya ambayo Muda sio mrefu kishindo chake kitapokewa kwa shangwe nchi nzima Wataendelea kudumu zaidi ya miaka 20 ijayo wakiwa na ushawishi huuhuu ulio chini ya wastani...
Naona ni mpango mzuri kwa ccm kama kikundi na hatari kwa ccm kama chama
 
Chama cha siasa watu wasipingane na misimamo au mawazo ya wengine?kwahiyo mtu akisema anachotaka yeye basi iwe hicho?uhuru wa mawazo na kuhoji umekufa?
 
Kama haitatumia dola inajifia soon
Huko kwenye dola umeenda mbali , Uwepo wa wapinzani ambao wanaoperate chini ya viwango na hawaeleweki wanachokipigania wakiwa wametawanyika kama wajenzi wa mnara wa babeli na kukaa kusubiri tukio walifanyie amplification ni tiketi isiyo na ghalama ya kuendelea kuwepo kwa ccm, hilo ni pambano katika phase ya chini kabisa
 
Inawezekana tu iwapo waliofukuzwa kama ni kweli ndio waliokua wasaliti halisi ,lkn halitowezekana iwapo wameacha mbegu zao nyuma ambazo zitaendelea kumea na kuleta mashaka!
 
Usisahau pia kila siku wanalazwa polisi au wanafikishwa mahakamani
 
Chama cha siasa watu wasipingane na misimamo au mawazo ya wengine?kwahiyo mtu akisema anachotaka yeye basi iwe hicho?uhuru wa mawazo na kuhoji umekufa?
ukipingana na mawazo ya wengi, wengi wakapitisha, unaoption moja ya kukubaliana nayo kama ni udhaifu ilaumu democracy sio watu.
 
Sasa kama wapinzani hawaeleweki na wametawanyika hawajui wanachokipigania wapo wapo tu! woga wa malaika mkuu hadi kuamua kujificha nyuma ya mgongo wa polisi ili kuendesha nchi kidikteta kauli za vitisho kila kukicha na visasi juu unatoka wapi!? Si ndiyo angeona hawa wapinzani hawajitambui hivyo uchaguzi anashinda kirahisi kabisa! Anapitisha katiba mpya ya rasimu ya Warioba na pia kuruhusu Tume huru ya uchaguzi. Thubutu! anajua Watanzania tutafanya kweli na kuipiga chini CCM milele. Hapo kwenye rangi neno halisi ni gharama hatuna neno ghalama kwenye lugha yetu ya Taifa.

Huko kwenye dola umeenda mbali , Uwepo wa wapinzani ambao wanaoperate chini ya viwango na hawaeleweki wanachokipigania wakiwa wametawanyika kama wajenzi wa mnara wa babeli na kukaa kusubiri tukio walifanyie amplification ni tiketi isiyo na ghalama ya kuendelea kuwepo kwa ccm, hilo ni pambano katika phase ya chini kabisa
 
Inawezekana tu iwapo waliofukuzwa kama ni kweli ndio waliokua wasaliti halisi ,lkn halitowezekana iwapo wameacha mbegu zao nyuma ambazo zitaendelea kumea na kuleta mashaka!
Safari hii ndiyo watakuwa wasaliti wabaya zaidi
 
Back
Top Bottom