Naililia Tanzania Yangu

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Nianze kwa kusema vita dhidi ya Mabeberu sio vita lelemama, inahitaji vijana wa kike na wakiume walioiva na kujitoa kwa mioyo yao hata mauti ili kuipigania nchi yao.

Kushindana na watu wenye fedha (matajiri waliojaa utajiri wa udhalimu) sio kazi rahisi. Hayati JPM, kama mashujaa wengi waliopigania nchi zao tangu akiwa waziri, atakumbukwa milele hasahasa kwa watanzania maskini.

Sishangai baada ya kulala kwake, usingizi wa mauti, kuanza kuibuka kwa kashifa nyingi dhidi yake, kwani yeye sio shujaa wa kwanza kuandamwa na kivuli cha kinyume cha mambo aliyokuwa akiyafanya.

Leo mtu aliyejitoa kupigana na mafsadi; mtu aliyewakamata Seth na Rugemalila, kwa kuhusika na wizi wa Escrow ac. ataonekana alikurupuka, na watugumiwa wataachiwa huru na kuonekana ni washindi.

Kuzikwa kwa Magufuli kutazika mambo mengi sana. Waliokuwa wanakula nchi na maadui zetu wanaingia madarakani sasa.

Wachimbaji wadogo wadogo, jiandaeni kuachia maeneo mliyoyagundua muwaachie wawekezaji maana wao wanalipa kodi.

Nchi jiandaeni kupokea misaada yote iliyokuwa imezuiwa kuingia nchini. Zama zimebadilika sasa.

Muda utaongea...

NB: Sitaandika tena kwenye hili jukwaa.

Mods. naombaa huu uzi usifutwa ili uwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Ndimi mzalendo wa taifa langu.

King. Nebu.
 
Beberu unakaa naye meza moja mnayajenga basi.... Haya tumefaidika nini Kwa kushindana na mabeberu ,? Tanzania ya viwanda ipo wapi? Tusidanganyane wakuu....!!!
Sitaandika tena kwenye hili jukwaa.

Mods. naombaa huu uzi usifutwa ili uwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.
 
Nukuu:
Wapo wanaosema mimi ni mwanamke nitaongozaje,naomba niwaambie mimi ni niliesimama hapa ni Rais mwenye jinsia ya kike marudiaimi nilieaimama mbele yenu ndie Rais.mwisho.
Sisi kama mamisaa tumemwelewa sana sasa kazi kwenu.
 
Nyie MATAGA mna matatizo.

JPM alipokuwa anatumbua viongozi wazembe/wezi.

Mlishangilia humu.

Leo SHS anafanya hivyohivyo.

Mnaanza kulialia, eti JPM anahujumiwa.
 
Tatizo lenu mlishaaminishwa kuwa Hayati Rais Magufuli alikuwa Masihi na nyinyi waumini wa hili dhehebu hamtaamini kuwa kuna sehemu alikosea pia na kuibuliwa kwa madudu hayo sio kumkashifu bali kuendeleza ile kazi yake iliyotukuka.

Hakuna sehemu Magufuli alisema kuwa kashamaliza kupigania Rushwa na uzembe serikalini ila alikuwa bado anapambana nao.

Nyinyi MATAGA sasa hivi mtakuwa kama wale wafuasi wa JK tu na kibaya zaid kazi zenu za kusifu na kuabudu zimefika tamati mrudi mtaani mkafanye kazi kama mlivyokuwa mnaitikia kiitikio cha wimbo wa Mkuu wenu.
 
Sitaandika tena kwenye hili jukwaa.

Mods. naombaa huu uzi usifutwa ili uwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

Yapo ambayo marehem aliyafanya ambayo ni mazur,lakin haikuwa justification ya yeye kuzuia mabaya yake yasisemwe,siyo justification ya yeye kuzuia freedom of speech n democracy,haikua justification ya yeye kuua solo letu la korosho na uhai wake kwa ujumla,kama binadam alikuwa na upande wake mwingine ambao ni wa hovyo,hakuwa malaika yule...

Lazima yale ambayo yalifichwa tuyajue Ili tujifunze.
 
Yaani misaada ilizuiwa kwa sababu gani sasa! Ndo maana maisha yalikuwa magumu kisa upumbafu wa jpm. Alikuwa anajua watanzania kwa kiasa Cha uzalendo ambao haupo. Maisha huwa hayasimami ndugu yangu. Yeye hata akisimamosha misaada alikuwa ana uhakika wa kula na kusaza ila anatuumiza sisi. Bora limekufa ili owe ahueni yetu
 
Nyie MATAGA mna matatizo.

JPM alipokuwa anatumbua viongozi wazembe/wezi.

Mlishangilia humu.

Leo SHS anafanya hivyohivyo.

Mnaanza kulialia, eti JPM anahujumiwa.

Watu wa ajabu Sana,

Sasa JPM wanamlilia kwann kwani alipolala si panajulikana?

Amepigana vita vikuu na mwendo ameumaliza,na sisi tunafuata kwenye hiyo safari,aache watu waendelee kujenga nchi
 
Yaani misaada ilizuiwa kwa sababu gani sasa! Ndo maana maisha yalikuwa magumu kisa upumbafu wa jpm. Alikuwa anajua watanzania kwa kiasa Cha uzalendo ambao haupo. Maisha huwa hayasimami ndugu yangu. Yeye hata akisimamosha misaada alikuwa ana uhakika wa kula na kusaza ila anatuumiza sisi. Bora limekufa ili owe ahueni yetu

Duuh,mkuu mbona umeongea kwa ukali sana mkuu,

Calm down,Mimi nikikumbuka alivyonitia umaskin wa kunidhulumu korosho zangu eti kisa zingine nimeinunua kwa kangomba sina ham nae kabisa,

Nimemsamehe namuachia mungu ila amenipa umaskin Sana Hayati magufuli
 
Usikate tamaa Mama Samia hana nia ya kumvua JPM nguo nia yake ni nzuri tu.

Mimi ni pro Magufuli ila Mama ametaka kuonyesha sehemu ambazo yeye hakukubaliana na Magufuli haswa eneo la transparency.

Ni kawaida tu hiyo Magufuli kafanya makubwa nchi hii ila tutakuwa waongo kusema kafanya kila kitu.

Hakuna anaeweza kufuta mazuri ya Magufuli sababu mengi yanaonekana kwa macho na mengine yataamuliwa na muda. Mfano kuna siku watu wataitaji sauti ya ukali kwenye maamuzi na haitakuwepo na hapo ndio watamkumbuka Magufuli.

So msiwe na mtazamo hasi kwa mama, hii nchi sasa yeye ndio kiongozi ana haki ya ku-set vision yake.
 
Tatizo lenu mlishaaminishwa kuwa Hayati Rais Magufuli alikuwa Masihi na nyinyi waumini wa hili dhehebu hamtaamini kuwa kuna sehemu alikosea pia na kuibuliwa kwa madudu hayo sio kumkashifu bali kuendeleza ile kazi yake iliyotukuka.
Hakuna sehemu Magufuli alisema kuwa kashamaliza kupigania Rushwa na uzembe serikalini ila alikuwa bado anapambana nao.
Nyinyi MATAGA sasa hivi mtakuwa kama wale wafuasi wa JK tu na kibaya zaid kazi zenu za kusifu na kuabudu zimefika tamati mrudi mtaani mkafanye kazi kama mlivyokuwa mnaitikia kiitikio cha wimbo wa Mkuu wenu.
Utapata taabu sana kama utataka kuwatofautisha Wafuasi wa Magufuli na Wafuasi wa Kibwetele.
 
Back
Top Bottom