Demokrasia ya nini Tanzania. Ni upuuzi mtupu. Ningekuwa na uwezo ningeondoa kabisa kitu kinachoitwa demokrasia Tanzania. Yapo majamaa yalishinikiza mchakato wa katiba mpya mpaka Kikwete akakubali. Baadaye hayo hayo majamaa yakaikataa. Mabilioni ya Tshs yakawa yametumika bila sababu.
Matokeo yake uchaguzi mkuu 2015 nusura usifanyike. Majamaa yakaanza kumcheka Kikwete na kumwita rais dhaifu. Yakasema yanataka rais wa maamuzi magumu. Amekuja Magufuli wa maamuzi magumu yanasema yanataka mpole.
Yalisema Kikwete anasafiri mno, amekuja asiyesafiri yanasema rais huyu mbona hasafiri. Yalimsema Lowassa fisadi baadaye yalipomchukua menyewe yakasema mbona msafi mno. Kitu kizuri cha Tanzania yanasema kibaya. Yaani vurugu tu. Kimsingi Tanzania hatujakomaa kwa Demokrasia.Tutakuwa tayari miaka 200 baadaye. Subiri niwe rais maana nina mpango wa kuwa rais na ni lazima niwe.
Hakika nafuta Demokrasia Tanzania.