Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza kwa Dr. Mwaka

Mheshimiwa Rais hapa ndipo orientation inahitajika si lazima kwenda Ngurudoto bali hapo DSM na iwe ya siku moja. Mimi naungana nawe kabisa ulivyofanya Ziara ya kushtukiza naamini ulikuwa da lengo maalumu, ulikuwa na data za kutosha na kweli ziara zakozimeleta impact kwani ulikuwa unatoa ujumbe kwa Wafanyakazi kuhusu uwajibikaji ukiwa pamoja na uwepo kazini muda wa kazi.
Sasa Seriously, kama ni kweli,Clinic ya Dr mwaka ndio kipaumbele cha wizara yako??????????

Anahudumia watu zaidi ya 60 kwa siku, hakuna alie thibitishwa kupona ugumba au kuondokewa na uvimbe, tokea ameanza kuhudumia unadhani ame dhuru maisha ya Watanzania wangapi kiafya na kiuchumi wewe kwako sio kipaumbele kwakuwa hakuna dada ama mama yako aliye pitia kwa mtu huyu
 
Dr kikwete nae kasomea wapi?

Akimalizana na Dr. Mwaka awaeleze watu wa Elimu wachunguze uProfessor wa China aliotunukiwa Rais wetu kipenzi pasipo kufundisha darasa lolote.

attachment.php
 
Attachments

  • kikwete_professorship.jpg
    kikwete_professorship.jpg
    71.9 KB · Views: 468
Kwa mujibu wa waziri ni kuwa kuna watu walioadhirika na tiba hii nafikiri ingekuwa muhimu kuadress hao walioadhirika kwanza maana kama ni kweli dawa zake sio sahihi basi watakao umia ni wengi sana..
 
Hapa shida ni Mwaka kujiita Dr.ama Matibabu anayoyatoa kwa Wagonjwa wake?Wanapona!Wanapata Ujazito?Wagonjwa waliyotibiwa wanasemaje?Tatizo hapa ni kuwa Mwaka anafanya shughuli zake ktk hali ya Ulimwengu wa sasa Ulivyo.Mandhari safi Nadhimu Eneo la Kliniki yake Japo Anatumia Tiba Mbadala(MATUNDA).Ulitegemea Afanye vichochoroni Eneo chafu Huyu Jamaa amepiga hatua kubwa ktk shughuli yake ya UJASIRIAMALI pia ameongeza Ajira.Hebu tusiwe na WIVU WA MAENDELEO YA WATU WANAOJITUMA KATIKA SHUGHULI ZAO.Swali kuu hapa Je wanaokwenda kwake na kufuata Masharti ya Tiba Wanapona na kupata watoto?
 
Habari zilizonifikia mchana ni kuwa mh. Kigwangallah alifanya ziara ya kustukiza ForePlan clinic na kumuamuru Dk.Mwaka kufika wizarani na kujieleza kwanini anajiita daktari wakati hajasomea maana ana elimu tu ya uganga.

Pili ajieleze kwanini anajitangaza sana kinyume na ethics za udaktari.

Dr. Kigwangallah amesema kuwa hataishia hapo bali atawatimbia wengine kama dokta Sigwa.

Kuna mambo ya msingi si hili
 
Last edited by a moderator:
Mke wake ndio kamponza wiki iliyopita alikuwa anakojiwa na Joyce Kiria kwenye Television anasema Mimi yaani Mke wa Mwaka ninatembelea Gari ya bei ghali sana lakini siringi pia akasema tumepata mafanikio makubwa sana na sasa tunategemea kuhamia kwenye ghorofa yetu.sasa yoote hayo ya nini? Kweli mwanamke mpumbavu huvunja nyuma Yake mwenyewe.
 
Wivu' Fitna' Chuki' Uchawi' Majungu ' Umasikini' Roho mbaya n.k vimewajaa wote wanaompinga Mwaka.

Na tatizo ni siku ile tu alipoonesha mikoko yake ya maana Clouds Tv.
 
Habari za Dr. Mwaka zimekuwa gumzo tena hasa baada ya kumpa Diamond kinachosemwa ni million 50 ili amtangaze, na moto ukakolezwa na Naibu Waziri Kigwangala alipofanya ziara ya ghafla kwenye kituo chake
Dr. Mwaka aliondoka dakika kumi kabla ya Kigwangala na ugeni wake kuwasili na wahudumu nao wakitorokea mlango wa nyuma
Commotion nzima ilionekana kama Dr. Mwaka ni mhalifu akivunja taratibu kadha za kitabibu katika kituo chake..mijadala ipo kwenye mitandao ya kijamii wengine wakiponda wengine wakikosoa na wengine wakisifu
Kama taifa tusikubali kubebwa na kuwa watumwa wa tamaduni za nje... China iko vizuri sana kwenye tiba za asili kwakuwa tu walikataa kuburuzwa na wazungu na kukienzi walicho nacho..leo hii wazungu hao hao ndio wanapigia upatu tiba mbadala
Kwa muktadha wa Kigwangala daktari ni yule mwenyewe vyeti vinavyotambulika toka kwenye vyuo vya kitabibu vinavyojulikana....huu ni utumwa mamboleo, kwani kama taifa hatuwezi kuwa na watu wa kaliba ya Dr. Mwaka kwenye vipawa na ujuzi wa mambo ya kitabibu? Tena aliyefanikiwa kuifanya tiba asili ya kisasa kwa kuweza kuchanganya utaalam wa kigeni na wa kienyeji
Hiki ni kipaji asikatishwe tamaa aendelezwe pamoja na wengine wote wa aina yake..asaidiwe aelekezwe kwenye makosa na sio kumnyanyapaa kama ilivyotokea...hii ni tunu tukiitumia vizuri tunaweza kupata chanzo kikubwa cha mapato huku tukisaidia watu wetu wenyewe kwenye unafuu na uhakika wa tiba
Tuna wazee wengi wanaofanya vizuri kwenye tiba za asili wanatibu magonjwa Yaliyoshindikana hospital za kizungu, wanaunga viungo vilivyokatika bila P.O.P....Lakini hawatambuliwi na hawapewi kipaumbele....... Tunakosea sana

Mshana huyu unayemsema anaunga mifupa bila POP walikuwepo toka zamani na wapo mpaka leo tatizo la kundi la kina mwaka ni wafanya biashara halisi kwa nguvu zote ukiwemo uwongo naamini wewe siyo mnafiki dozi ya malaria kwenye kliniki za mfumo wa Mwaka ni kubwa kuliko bei ya dawa hiyo hiyo kwenye maduka ya madawa ya hospitali na tiba inachukua muda mrefu na gharama ni kubwa lakini zaidi ya yote watu hawa hawana uelewa sahihi wa madawa wanayoyauza na wengi wanawaachia watu wasiokuwa na ujuzi sahihi juu ya tiba wao mabosi muda mwingi wanakwenda kutafuta masoko zaidi na kuwaacha hawa vihiyo kwenye kliniki zao na ndiyo maana mara nyingi ukienda pale huwezi kumpata muhusika utaambiwa mpaka kwa appointment siyo kwamba anawahudumia wagonjwa wengine pale bali yuko mikoani kufanya marketing. Tiba mbadala wanatakiwa wapewe mwongozo kuna ndugu yetu mmoja sengerema alikwenda kwenye duka lao hao wanaojiita tiba mdadala alikuwa akisumbuliwa na fungus sehemu za siri wakampa madawa ya mitishamba ili aweke ukeni matokeo alivimba sana sehemu hizo na zikaanza kuoza hadi mauti inampata alikuwa ameoza mpaka ini kwa mujibu wa madaktari waliokuwa wakimtibu hospitali ya DDH sengerema hivyo nashauri watu hawa tuwatumie kwa tahadhari sana kwani wengi wao hawana uelewa sahihi wa madawa wanayoyauza na ghrama zao ni kubwa sana ukilinganisha na madawa ya hospital.
 
Anahudumia watu zaidi ya 60 kwa siku, hakuna alie thibitishwa kupona ugumba au kuondokewa na uvimbe, tokea ameanza kuhudumia unadhani ame dhuru maisha ya Watanzania wangapi kiafya na kiuchumi wewe kwako sio kipaumbele kwakuwa hakuna dada ama mama yako aliye pitia kwa mtu huyu

Tujiulize kwanza kwanini watanzania hao waende huko??Kama kuna shida ya hospitali zetu na watoa huduma wetu kwenye Hospitali zetu,na aina ya treatment tunayopewa na hospitali zetu ukichanganya na Rushwa tunayotakiwa kutoa kwa madakatari waliosomeshwa kwa kodi zetu,lazima watanzania wataenda mahali ambako wanapewa huduma kama malkia au mfalme,hata kama wanadanganywa.

Treatment tu inamfanya mtu apone ugonjwa wake
 
Mwaka ni bonge la tapeli,anawezaje kujiaddress kama Dr wakati siyo? Kwenye matangazo yake kama hili la diamond yaani kajiadress kama Dr kabisa.
Teh teh...Diamond kamponza Dr wa watu..Alizidi sana kujitangaza nae..Ila ni furaha kwa jamii..Acha wanyooshwe
 
Kwanini kakimbia mtu unayejiamini hukimbii.angebaki atoe maelezo kama Kuna makosa mnayamalizia mbele ga safari.kukimbia anaonesha ana mapungufu makubwa katika kazi zake.
 
namuunga mkono dr kutorokea mlango wa nyuma hizi ghafla ghafla ni kudhalilishana tu
 
Habari za Dr. Mwaka zimekuwa gumzo tena hasa baada ya kumpa Diamond kinachosemwa ni million 50 ili amtangaze, na moto ukakolezwa na Naibu Waziri Kigwangala alipofanya ziara ya ghafla kwenye kituo chake
Dr. Mwaka aliondoka dakika kumi kabla ya Kigwangala na ugeni wake kuwasili na wahudumu nao wakitorokea mlango wa nyuma
Commotion nzima ilionekana kama Dr. Mwaka ni mhalifu akivunja taratibu kadha za kitabibu katika kituo chake..mijadala ipo kwenye mitandao ya kijamii wengine wakiponda wengine wakikosoa na wengine wakisifu
Kama taifa tusikubali kubebwa na kuwa watumwa wa tamaduni za nje... China iko vizuri sana kwenye tiba za asili kwakuwa tu walikataa kuburuzwa na wazungu na kukienzi walicho nacho..leo hii wazungu hao hao ndio wanapigia upatu tiba mbadala
Kwa muktadha wa Kigwangala daktari ni yule mwenyewe vyeti vinavyotambulika toka kwenye vyuo vya kitabibu vinavyojulikana....huu ni utumwa mamboleo, kwani kama taifa hatuwezi kuwa na watu wa kaliba ya Dr. Mwaka kwenye vipawa na ujuzi wa mambo ya kitabibu? Tena aliyefanikiwa kuifanya tiba asili ya kisasa kwa kuweza kuchanganya utaalam wa kigeni na wa kienyeji
Hiki ni kipaji asikatishwe tamaa aendelezwe pamoja na wengine wote wa aina yake..asaidiwe aelekezwe kwenye makosa na sio kumnyanyapaa kama ilivyotokea...hii ni tunu tukiitumia vizuri tunaweza kupata chanzo kikubwa cha mapato huku tukisaidia watu wetu wenyewe kwenye unafuu na uhakika wa tiba
Tuna wazee wengi wanaofanya vizuri kwenye tiba za asili wanatibu magonjwa Yaliyoshindikana hospital za kizungu, wanaunga viungo vilivyokatika bila P.O.P....Lakini hawatambuliwi na hawapewi kipaumbele....... Tunakosea sana

Mkuu ulichoongea ni sawa kwa upeo wako lakini unatakiwa uintergrate na medical legal laws( legal medicine)

Dr. Mwaka kazi zake zinakiuka medical legal
 
Wivu' Fitna' Chuki' Uchawi' Majungu ' Umasikini' Roho mbaya n.k vimewajaa wote wanaompinga Mwaka.

Na tatizo ni siku ile tu alipoonesha mikoko yake ya maana Clouds Tv.

Nani anashida na vipesa vyake? Udaktari una ethics wewe nyau mkianza kuharisha mnaanza kuilaumu serikali .pumbavu sana. Kama hakuwa na kasoro yeyote kilichomfanya akimbie kitu gani?
 
Back
Top Bottom