Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,016
- 9,885
Si tunaelezwa kuwa nyama ina madhara kiafya??!!
Vyuma vimekazaJeuri ya kufanya anasa kama hiyo tunaitolea wapi awamu hii ya tano ?, cha msingi tungoje tu 28th october ijulikane mbivu na mbichi ..
Hapo Sasa Utaambiwa Nyama Siyo NzuriSi tunaelezwa kuwa nyama ina madhara kiafya??!!
Wazigua Wanasema Msunga Na Bobwe
Maziwa Mwiko
Hakuna ulazima wa kula nyama kiasi hicho ,kiwango cha afya ni robo kilo tu kwa wiki kwa mtu mmoja,kuzidisha ni kujitafutia matatizo
Maziwa nayo yana Cholestrol
Tupo uchumi wa kati, juhudi za serikali awamu hiiKatibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Rashid Tamatamah amesema Watanzania hawajafikia kiwango cha kimataifa cha ulaji wa nyama ambacho ni kilo 50 kwa mtu mmoja kwa mwaka.
Pia amesema changamoto nyengine, ni unywaji wa maziwa ambapo kila mtu anatakiwa angalau anywe lita 200 kwa mwaka.
Tamatamah aliyasema hayo juzi, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Njombe,yakiwa na kauli mbiu ‘kesho njema inajengwa na lishe bora endelevu’.
Alisema kwa mujibu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), viwango vya ulaji nyama na unywaji wa maziwa nchini bado uko chini.
‘’Bado ulaji wa nyama na unywaji wa maziwa si wa kuridhisha, natoa kutoa rai kwa wananchi kuongeza ulaji wa nyama ili tuweze kufikia kiwango hiki ambacho kinatambulika kimataifa,’’alisema.
Alisema mwaka 2019/20, uzalishaji wa maziwa umefikia lita bilioni 3, ikilinganishwa na lita bilioni 2.7 zilizozalishwa mwaka 2018/19.
‘’Ongezeko la uzalishaji linatokana na ongezeko la ng’ombe pamoja na kuboreshwa mazingira ya uwekezaji katika tasnia ya maziwa nchini,’’alisema.
Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la uwapo wa ongezeko la viribatumbo kwa wanawake kutokana na kutozingatia mlo kamili.
Aliwataka wananchi mkoani Njombe kuacha imani potofu, kuwa mtoto akikosa lishe amebemendwa.
“Hakuna kubemendwa, ni kukosa lishe,kuna mila potofu eti mtoto akikosa lishe kabemendwa, acheni hizo imani, jueni amepata utapiamlo,”alisema Mgumba.
Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya alisema ili kupambana utapiamlo tayari mkoa umepanga mikakati mbalimbami ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi.
Mkuu issue ya maziwa ya ngombe is beyond cholesteral.......Ngombe hasa wa kisasa wanakamuliwa wakati reproductive hormones zao ziko juu.....hizi hormones zinakuwepo kwenye maziwa pia.....nakuna uhusiano mkubwa kati ya maziwa na nguvu za kiume.....tafuta article ina title Dairy food intake in relation to semen quality and reproductive hormone levels among physical active young men ya 2013 .....pia kuna uhusiano mkubwa kati ya maziwa na tezi dume.....maziwa yanastimulate cells za tezi dume uki google utapata pia material kibao......maziwa ni yakuyaangalia sana.....Maziwa yakiwa skimmed hayadhuru ila sasa kwa mtaani nani anaweza ku skim maziwa ili kuondoa mafuta?!
Mtihani unakuwa hapo sasa!
Shukrani Duuu, vp kuhusu mtumiaji wa mtindi tusaidie kidogo wengi tunaona maziwa yanamsaada mkubwa kama asaliMkuu issue ya maziwa ya ngombe is beyond cholesteral.......Ngombe hasa wa kisasa wanakamuliwa wakati reproductive hormones zao ziko juu.....hizi hormones zinakuwepo kwenye maziwa pia.....nakuna uhusiano mkubwa kati ya maziwa na nguvu za kiume.....tafuta article ina title Dairy food intake in relation to semen quality and reproductive hormone levels among physical active young men ya 2013 .....pia kuna uhusiano mkubwa kati ya maziwa na tezi dume.....maziwa yanastimulate cells za tezi dume uki google utapata pia material kibao......maziwa ni yakuyaangalia sana.....
Ccm wanasema wao wanataka kutawala wananchi wanyonge. Sasa wanyonge na nyama wapi na wapi? Wanyonge yao maharage kwa chapati 2Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Rashid Tamatamah amesema Watanzania hawajafikia kiwango cha kimataifa cha ulaji wa nyama ambacho ni kilo 50 kwa mtu mmoja kwa mwaka.