Naibu waziri: Ulaji nyama na maziwa kwa Watanzania bado changamoto

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,786
2,000
Tutakula maharage badala ya nyama

Tena protini itokanayo na mazao ya jamii ya mikundekunde ndiyo hushauriwa kutumika kiafya zaidi kuliko protini zitokanazo na wanyama kama nyama na samaki .

Mtu akiweza kula maharagwe, choroko, kunde, mbaazi, njegere, njugumawe n.k atakuwa na afya njema zaidi kuliko mia nyama mara kwa mara
 
nipeukweli

JF-Expert Member
Jul 16, 2012
656
500
Huku tupo uchumi wa kati
Huku nyama hailiki, maziwa hayanyweki
Nafikiri nahitaji kuketi nielimishwe
 
Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
25,466
2,000
Tena protini itokanayo na mazao ya jamii ya mikundekunde ndiyo hushauriwa kutumika kiafya zaidi kuliko protini zitokanazo na wanyama kama nyama na samaki .

Mtu akiweza kula maharagwe, choroko, kunde, mbaazi, njegere, njugumawe n.k atakuwa na afya njema zaidi kuliko mia nyama mara kwa mara
Wanatufanya hatujui. Kuna watu hawali nyama na hawajapungukiwa hayo wanayoyasema
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
9,688
2,000
Hawa wataalamu wetu ni wakuwasikiliza kwa sikio moja tu. Si wa kuwaamini moja kwa moja.
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,974
2,000
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Rashid Tamatamah amesema Watanzania hawajafikia kiwango cha kimataifa cha ulaji wa nyama ambacho ni kilo 50 kwa mtu mmoja kwa mwaka

Hashim Rungwe alitaka kugawa nyama na ubwabwa ili kufikia hivyo viwango akazuiwa
 
ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
5,421
2,000
Watu walioshindwa kuweka umeme kwenye nyumba zao kwa 27,000 watapata wapi pesa ya kula nyama na kunywa maziwa? hadi harusi ,sikukuu au wasombwe kwenye malori ya ccm kuletwa mjini kwenye mikutano ya kampeni zao
 
B'REAL

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
4,205
2,000
Sisi kwetu ni wafugaji!Ila siku mbuki siku wamechinjaa mbuzi au ng'ombe Kama kiburudisho tu,atachinjwaa akiwa anaunwa taabani,atachinjwaa kukiwa na msiba au harusi.mbuzi karibia Mia nne na bado wanazaa Ila hakunaa kutafuna.huu ulikuwa ujinga sanaa
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,786
2,000
Watu walioshindwa kuweka umeme kwenye nyumba zao kwa 27,000 watapata wapi pesa ya kula nyama na kunywa maziwa? hadi harusi ,sikukuu au wasombwe kwenye malori ya ccm kuletwa mjini kwenye mikutano ya kampeni zao

Yani inasikitisha sana !

Watu wanaishi kwa kula mlo mmoja tu kwa siku na hiyo Ndiyo maana hasa ya umasikini.

Na kwa kule kuwa Ignorants wanadanganyika kirahisi hususa wakati huu wa Campaign na uchaguzi,

Wakipewa T-shirt, kofia n.k wanarubunika.
 
ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
5,421
2,000
Yani inasikitisha sana !

Watu wanaishi kwa kula mlo mmoja tu kwa siku na hiyo Ndiyo maana hasa ya umasikini.

Na kwa kule kuwa Ignorants wanadanganyika kirahisi hususa wakati huu wa Campaign na uchaguzi,

Wakipewa T-shirt, kofia n.k wanarubunika.
Ndio maana huwa nasema cdm wasije kujidanganya kwenda kupoteza pesa na mda eti kufanya kampeni kwa watu wa dizaini hii ambao kwao umaskini ni sehemu ya maisha yao hawaelewi wala kuambilika maana wana udumavu wa akili na kupaushwa na umaskini,hawa huwezi wasimulia maendeleo au mambo ya kuhitaji uelewa wakabadilika wanachojua wao ni ccm tu..Usimsaidie maskini achana nae
 
Tembomtata

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
265
500
Sisi kwetu ni wafugaji!Ila siku mbuki siku wamechinjaa mbuzi au ng'ombe Kama kiburudisho tu,atachinjwaa akiwa anaunwa taabani,atachinjwaa kukiwa na msiba au harusi.mbuzi karibia Mia nne na bado wanazaa Ila hakunaa kutafuna.huu ulikuwa ujinga sanaa
Ni ujinga ukiwa huelewi....sisi wafugaji mifugo sio chakula mifugo ni mali.....kwanini ni haribu mali yangu kwa shida isiyo ya muhimu....nikichinja damu na maziwa ntaipata wapi?......mifugo kwetu ni source ya security
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,786
2,000
Ndio maana huwa nasema cdm wasije kujidanganya kwenda kupoteza pesa na mda eti kufanya kampeni kwa watu wa dizaini hii ambao kwao umaskini ni sehemu ya maisha yao hawaelewi wala kuambilika maana wana udumavu wa akili na kupaushwa na umaskini,hawa huwezi wasimulia maendeleo au mambo ya kuhitaji uelewa wakabadilika wanachojua wao ni ccm tu..Usimsaidie maskini achana nae

Nazani kinachotakiwa ni kuwapa elimu ya uraia na elimu ya mpigakura na zaidi ya hayo yamkini wataelewa.

Kule wanatishiwa wanaambiwa mkichagua upinzani wataleta vita, Eti zamani walikuwa wanawawekea hadi video za kuonesha vita lakini sizani kama ni kweli.

Mikoani huko raia wanaogopa hadi polisi kama enzi za ukoloni.

Kwamba kujua askari ni Mtumishi wao anayelipwa kwa kodi wanazolipa wao wananchi kupitia ushuru wa bidhaa na fine mbalimbali wanazotozwa na serikali hiyo hawajui.

Kwamba askari ni Mtumishi wao wa kuwalinda wao na mali zao hiyo hawajui.

Kwamba kuwa polisi ni mgawanyo wa majukumu tu hilo hawalijui.

Kazi ipo kubwa aisee!

Yani hata nchi jirani zinazotuzunguuka mfano Zambia , Malawi na Kenya wako mbali sana!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom