Naibu waziri: Ulaji nyama na maziwa kwa Watanzania bado changamoto

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,931
2,000
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Rashid Tamatamah amesema Watanzania hawajafikia kiwango cha kimataifa cha ulaji wa nyama ambacho ni kilo 50 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Pia amesema changamoto nyengine, ni unywaji wa maziwa ambapo kila mtu anatakiwa angalau anywe lita 200 kwa mwaka.

Tamatamah aliyasema hayo juzi, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Njombe,yakiwa na kauli mbiu ‘kesho njema inajengwa na lishe bora endelevu’.

Alisema kwa mujibu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), viwango vya ulaji nyama na unywaji wa maziwa nchini bado uko chini.

‘’Bado ulaji wa nyama na unywaji wa maziwa si wa kuridhisha, natoa kutoa rai kwa wananchi kuongeza ulaji wa nyama ili tuweze kufikia kiwango hiki ambacho kinatambulika kimataifa,’’alisema.

Alisema mwaka 2019/20, uzalishaji wa maziwa umefikia lita bilioni 3, ikilinganishwa na lita bilioni 2.7 zilizozalishwa mwaka 2018/19.

‘’Ongezeko la uzalishaji linatokana na ongezeko la ng’ombe pamoja na kuboreshwa mazingira ya uwekezaji katika tasnia ya maziwa nchini,’’alisema.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la uwapo wa ongezeko la viribatumbo kwa wanawake kutokana na kutozingatia mlo kamili.

Aliwataka wananchi mkoani Njombe kuacha imani potofu, kuwa mtoto akikosa lishe amebemendwa.

“Hakuna kubemendwa, ni kukosa lishe,kuna mila potofu eti mtoto akikosa lishe kabemendwa, acheni hizo imani, jueni amepata utapiamlo,”alisema Mgumba.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya alisema ili kupambana utapiamlo tayari mkoa umepanga mikakati mbalimbami ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi.
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,786
2,000
Si tunaelezwa kuwa nyama ina madhara kiafya??!!

Inategemea na aina ya life styles za watu.

Kwa wale ambao kazi zao muda mwingi wamekaa badala ya kufanya kazi za kutembea mwendo mrefu mfano wakulima, mafundi ujenzi n.k ni hatari kiafya kama watakula nyama nyingi.
 
Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
7,350
2,000
Hakuna ulazima wa kula nyama kiasi hicho ,kiwango cha afya ni robo kilo tu kwa wiki kwa mtu mmoja,kuzidisha ni kujitafutia matatizo

Maziwa nayo yana Cholestrol
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
6,786
2,000
Hakuna ulazima wa kula nyama kiasi hicho ,kiwango cha afya ni robo kilo tu kwa wiki kwa mtu mmoja,kuzidisha ni kujitafutia matatizo

Maziwa nayo yana Cholestrol

Maziwa yakiwa skimmed hayadhuru ila sasa kwa mtaani nani anaweza ku skim maziwa ili kuondoa mafuta?!

Mtihani unakuwa hapo sasa!
 
blackcornshman

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
4,964
2,000
Kwa hiyo nikila kilo 20 badala ya 50 au lita 150 badala ya 200 inakuawje sasa?Je vipi wale wa kilo ya kitimoto mara mbili kwa wiki plus serengeti lager?
 
Tembomtata

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
265
500
Wakati wenzetu wanaachana na maziwa na nyama kwasababu ya matatizo kiafya....sisi ndo tunayakimbilia bila kueleza nikiwango gani kinapaswa kutumiwa....No wonder rate ya tezi dume, heart disease, kidney itaongezeka kwa kasi.......Hivi ni mnyama gani mwingine anakunywa maziwa ya mnyama mwingine🤔🤔
 
Mtende

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
6,388
2,000
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Rashid Tamatamah amesema Watanzania hawajafikia kiwango cha kimataifa cha ulaji wa nyama ambacho ni kilo 50 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Pia amesema changamoto nyengine, ni unywaji wa maziwa ambapo kila mtu anatakiwa angalau anywe lita 200 kwa mwaka.

Tamatamah aliyasema hayo juzi, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Njombe,yakiwa na kauli mbiu ‘kesho njema inajengwa na lishe bora endelevu’.

Alisema kwa mujibu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), viwango vya ulaji nyama na unywaji wa maziwa nchini bado uko chini.

‘’Bado ulaji wa nyama na unywaji wa maziwa si wa kuridhisha, natoa kutoa rai kwa wananchi kuongeza ulaji wa nyama ili tuweze kufikia kiwango hiki ambacho kinatambulika kimataifa,’’alisema.

Alisema mwaka 2019/20, uzalishaji wa maziwa umefikia lita bilioni 3, ikilinganishwa na lita bilioni 2.7 zilizozalishwa mwaka 2018/19.

‘’Ongezeko la uzalishaji linatokana na ongezeko la ng’ombe pamoja na kuboreshwa mazingira ya uwekezaji katika tasnia ya maziwa nchini,’’alisema.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la uwapo wa ongezeko la viribatumbo kwa wanawake kutokana na kutozingatia mlo kamili.

Aliwataka wananchi mkoani Njombe kuacha imani potofu, kuwa mtoto akikosa lishe amebemendwa.

“Hakuna kubemendwa, ni kukosa lishe,kuna mila potofu eti mtoto akikosa lishe kabemendwa, acheni hizo imani, jueni amepata utapiamlo,”alisema Mgumba.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya alisema ili kupambana utapiamlo tayari mkoa umepanga mikakati mbalimbami ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi.
Tupo uchumi wa kati, juhudi za serikali awamu hii
 
Tembomtata

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
265
500
Maziwa yakiwa skimmed hayadhuru ila sasa kwa mtaani nani anaweza ku skim maziwa ili kuondoa mafuta?!

Mtihani unakuwa hapo sasa!
Mkuu issue ya maziwa ya ngombe is beyond cholesteral.......Ngombe hasa wa kisasa wanakamuliwa wakati reproductive hormones zao ziko juu.....hizi hormones zinakuwepo kwenye maziwa pia.....nakuna uhusiano mkubwa kati ya maziwa na nguvu za kiume.....tafuta article ina title Dairy food intake in relation to semen quality and reproductive hormone levels among physical active young men ya 2013 .....pia kuna uhusiano mkubwa kati ya maziwa na tezi dume.....maziwa yanastimulate cells za tezi dume uki google utapata pia material kibao......maziwa ni yakuyaangalia sana.....
 
Ugobha

JF-Expert Member
Jul 18, 2020
869
1,000

Shukrani Duuu, vp kuhusu mtumiaji wa mtindi tusaidie kidogo wengi tunaona maziwa yanamsaada mkubwa kama asali
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
12,311
2,000
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Rashid Tamatamah amesema Watanzania hawajafikia kiwango cha kimataifa cha ulaji wa nyama ambacho ni kilo 50 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Pia amesema changamoto nyengine, ni unywaji wa maziwa ambapo kila mtu anatakiwa angalau anywe lita 200 kwa mwaka.

Tamatamah aliyasema hayo juzi, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Njombe,yakiwa na kauli mbiu ‘kesho njema inajengwa na lishe bora endelevu’.

Alisema kwa mujibu wa Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), viwango vya ulaji nyama na unywaji wa maziwa nchini bado uko chini.

‘’Bado ulaji wa nyama na unywaji wa maziwa si wa kuridhisha, natoa kutoa rai kwa wananchi kuongeza ulaji wa nyama ili tuweze kufikia kiwango hiki ambacho kinatambulika kimataifa,’’alisema.

Alisema mwaka 2019/20, uzalishaji wa maziwa umefikia lita bilioni 3, ikilinganishwa na lita bilioni 2.7 zilizozalishwa mwaka 2018/19.

‘’Ongezeko la uzalishaji linatokana na ongezeko la ng’ombe pamoja na kuboreshwa mazingira ya uwekezaji katika tasnia ya maziwa nchini,’’alisema.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la uwapo wa ongezeko la viribatumbo kwa wanawake kutokana na kutozingatia mlo kamili.

Aliwataka wananchi mkoani Njombe kuacha imani potofu, kuwa mtoto akikosa lishe amebemendwa.

“Hakuna kubemendwa, ni kukosa lishe,kuna mila potofu eti mtoto akikosa lishe kabemendwa, acheni hizo imani, jueni amepata utapiamlo,”alisema Mgumba.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya alisema ili kupambana utapiamlo tayari mkoa umepanga mikakati mbalimbami ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi.
Ccm wanasema wao wanataka kutawala wananchi wanyonge. Sasa wanyonge na nyama wapi na wapi? Wanyonge yao maharage kwa chapati 2
 
hmax4

Member
Sep 6, 2020
39
125
Nyama haina madhara na haijawahi kuwa na madhara, hiyo ni mitazamo tu ya watu na watu wanaojifanya wanajua lishe kiujanja. Mashirika ya chakula yote duniani wanashauri ule nyama na ni muhimu sana kwa mwili.
Si tunaelezwa kuwa nyama ina madhara kiafya??!!
 
hmax4

Member
Sep 6, 2020
39
125
Mkuu cholesterol haina uhusiano wowote na afya ya mwili maana mwili wenyewe unatengeneza cholesterol 80%.
Hakuna ulazima wa kula nyama kiasi hicho ,kiwango cha afya ni robo kilo tu kwa wiki kwa mtu mmoja,kuzidisha ni kujitafutia matatizo

Maziwa nayo yana Cholestrol
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom