VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Fadhila huwa ina gharama zake. Huwa ina ugumu na wepesi wake. Baada ya kupata ngekewa ya kuteuliwa kuwa Mbunge na Rais halafu baadaye kusimamiwa awe mgombea wa Unaibu Spika, Dr. Tulia Ackson ana wajibu, sababu na malengo ya kulipa fadhila kwa aliyemteua na kumsimamia. Kwa Rais.
Kwa wanaokumbuka, Dr. Tulia alianza kuchukua fomu za kugombea Uspika. Kwakuwa Uspika hauhitaji mgombea kuwa Mbunge, kama ulivyo Unaibu Spika, alikuwa ana sifa. Alipozidiwa nguvu huko na akina Ndugai, haraka akateuliwa Mbunge ili awanie Unaibu Spika. Akawahi kugombea na hatimaye kuchaguliwa.
Macho na fikra za Dr. Tulia ni kwa aliyemteua na kumsimamia. Katika hali na mtazamo huo, Dr. Tulia atapaswa kuwa msaliti kwa wanaomzunguka ili kumpendeza mkuu. Ameanza na kumsaliti mkuu wake Spika kwa kurejesha fedha za Bunge kwa Rais huku Spika akisoma habari hiyo facebook na watsapp. Ni kwa mujibu wa Mbunge G. J. Lema.
Wabunge wote wa CCM wanaomshangilia,kumshabikia na kuvutiwa naye,wakae chonjo. Usaliti utajitokeza wakati wowote itakapotakiwa kumridhisha mkuu. Waweke akiba ya maneno na matendo. Kijamii,mlipafadhila anafaa. Kisiasa,mlipafadhila anatisha!
Mzee Tupatupa wa 'Ulevini'
Lumumba,Dar es Salaam