Naibu Spika awatoa nje ya Ukumbi wa Bunge, Wabunge wote wanawake wa Upinzani (UKAWA)

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,320
16,296
Wabunge wanawake wa Upinzani wametoka wote nje ya Bunge kwa madai ya kudhalilishwa bungeni na mbunge mmoja wa CCM kuwa wanapewa viti hivyo kwa kuwa na mahusiano na viongozi wao wa juu.

Wabunge hao waliomba muongozo kwa naibu spika lakini hawakusikilizwa ndipo waliposimama wote na naibu spika kuwataka kukaa chini na ndipo kulipoibuka sekeseke la wabunge hao na kuamua kususia kikao hicho cha bunge asubuhi hii na kutoka nnje huku wakiahidi kuja na tamko kali kuhusu udhalilishaji waliofanyiwa huku naibu spika tulia akifurahia tukio hilo

Msikilize hapa Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja Wanawake CHADEMA, Halima Mdee akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge wanawake wa Ukawa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge kufuatia Mbunge wa viti maalumu Sophia Mwakagenda kuomba mwongozo wa Spika wa Bunge kwa kauli aliyotoa jana Mbunge wa jimbo la Ulanga Goodluck Mlinga kuzungumza bungeni kuwa wabunge wa CHADEMA ili wapate ubunge wa viti maalumu lazima wawe na mahusiano na viongozi wao.



=================

Update;


Taarifa za hivi punde kutoka bungeni, wabunge hao wamezungukwa na watu wa Usalama kwenye ofisi za KUB ambako walikuwa wanaendelea na kikao baada ya kutoka bungeni. Wanausalama hao ni wa kiume lakini ndo wameanza kuwaita WPs kupanda ghorofa ya pili ziliko ofisi hizo. Ni mwendelezo wa sakata lililoanza jana hadi NS akaagiza askari wamtoe Mbunge wa Ukonga, Waitara.

Maelezo mafupi juu ya hasa kilichotokea jana bungeni kuhusu Mbunge wetu Waitara Mwita Mwikabwe akatolewa nje kwa amri ya Naibu Spika. Kisha yatafuatiwa na maelezo (katika sauti) ya kina kutoka kwa Mbunge mwenyewe Ndugu Waitara alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea kwa ufasaha kilichotokea jana bungeni ambao ni mwendelezo wa 'maelekezo' ya namna ya kuliendesha bunge kwa kudhibiti sauti na nguvu za hoja kutoka UKAWA kwa manufaa ya CCM na Serikali yake.

Jana mara baada ya Bunge kurejea session ya jioni Naibu Spika alionekana kuyumba katika kulisimamia bunge kwa kuruhusu matusi, lugha za kejeli na upotoshaji kutoka kwa wabunge wa CCM walionekana kupangwa kimkakati huku yeye akizuia juhudi zote za Wabunge wa UKAWA waliokuwa wakitumia haki yao ya kikanuni kuomba miongozo, kutaka kutoa taarifa na kuhusu utaratibu ili baadhi ya mambo yatolewe ufafanuzi. Jambo ambalo ni mojawapo ya misingi ya uendeshaji na usimamiaji wa mabunge.

Alianza Mbunge wa CCM kutoka Zanzibar akisema kuwa Wabunge wa Upinzani (UKAWA) wanaharishia mdomoni badala ya nyuma.

Naibu Spika hakuchukua hatua yoyote kama ambavyo hata akili ya kawaida ingetarajia ifanyike hivyo. Akapiga kimya huku akizuia wabunge wetu kuhoji.

Mbunge wa Ulanga ambaye ni mtoto wa marehemu Celina Kombani naye akaendeleza lugha za kejeli na kupotosha. Akasema eti Wabunge wa UKAWA wamerudi Bungeni kuchangia baada ya yeye kumshauri shemeji yake Mbowe (Freeman, KUB) ili aturuhusu. Kwa hiyo wako pale bungeni kwa sababu yake.

Akaendelea kudai kuwa sifa ya Wabunge wanawake wa Chadema kupata Ubunge ni kila mtu lazima aitwe Baby kabla ya kupata Ubunge viti maalum.

Akaendelea kudai tena kwamba Wabunge wetu wanafanya vitendo vya kishoga.

Wabunge wetu kadhaa wakasimama kuomba miongozo, kutoa taarifa na kuomba utaratibu. Lakini kiti hakikujali. Hakikutoa nafasi hiyo.

Baada ya kuwepo kwa kelele nyingi na baadae kukawa na utetezi kutoka kwa Jenista Mhagama kwamba hata wabunge wa upinzani walikuwa wamesema matusi, kelele zikawa nyingi zaidi, ndipo NS akamtaka mwandishi wa Hansard afute maneno machafu yote.

Akafuata Mbunge mwingine wa CCM kutoka Kigoma, Kasulu akasema yeye ana ushahidi kwamba Ndugu Lissu ana jalada la ugonjwa Hospitali ya Milembe!

Wabunge wetu ambao hadi hatua hiyo walikuwa wamenyimwa nafasi ya kuzungumza, wakaendelea kupiga kelele na kusimama.

NS akamtaka afute au adhibitishe kauli yake baada ya Lissu kuomba muongozo. Yule Mbunge wa CCM badala ya kufuta maneno akawa anazunguka zunguka mtu ooh mara ni maneno yako mtaani, mara hivi mara vile.

Baada ya kuona kiti kinazidi kuyumba, ama kwa makusudi au kwa kujua kinachofanya, Mbunge wetu Waitara akalazimika kusimama akimtaka yule Mbunge wa CCM afute kauli zake hizo za upotoshaji. Ndipo akafuta.

Akafuta lakini tena akasema Mnyika anaumwa na anajua yuko Mhimbili anatibiwa.

Kitendo hicho cha yule mbunge kuendelea kutoa lugha za kejeli, kupotosha na kuzungumza mambo ambayo hawezi kuthibitisha huku kiti kikiwa kimya, kikamfanya Waitara asogee kwake ili kuwa karibu naye.

Baada ya kuona hivyo Naibu Spika akaagiza askari wamtoe nje, kama ambavyo inaonekana kwenye picha inayosambaa.

Hicho kilichotokea jana jioni, ndiyo mwendelezo wake wa asubuhi hii ambapo wabunge wanawake wa Ukawa wametolewa bungeni baada ya kutaka ufafanuzi na hatua dhidi ya hizo kauli za udhalilishaji zilizotolewa jana, mbele ya Naibu Spika ambaye naye ni Mbunge wa Viti Maalum.

Wabunge hao wameshazungumza na wanahabari kuelezea suala hilo na sasa wanaendelea na kikao. Tusubiri maamuzi ya kikao hicho.

Lakini jambo la kushangaza sana ni kwamba wakati lugha za kudhalilisha zikitolewa jana, si tu NS alikuwa anaonekana kunyamazia lkn pia viongozi wa Umoja wa Wabunge Wanawake (wote) walikuwa wanapiga makofi.

Hayo ni mbali na majibu ya mmoja wa Manaibu Waziri aliyesema jana bungeni kuwa anaweza 'kuwatia/kuwapiga za uso' wabunge wa upinzani, kisa walihoji alivyokuwa akijibu hoja zao bungeni

Makene
 
Maneno hayo yametolewa na nani? Nini reaction ya kiti cha Spika? Aliyewadhalilisha amechukuliwa hatua gani hadi sasa?
 
Wabunge wa viti maalum wa upinzani wametoka wote nnje ya bunge kwa madai ya kudhalilishwa bungeni na mbunge mmoja wa ccm kua wanapewa viti hivyo kwa kua na mahusiano na viongozi wao wa juu

Wabunge hao waliomba muongozo kwa naibu spika lakini hawakusikilizwa ndipo waliposimama wote na naibu spika kuwataka kukaa chini na ndipo kulipoibuka sekeseke la wabunge hao na kuamua kususia kikao hicho cha bunge asubuhi hii na kutoka nnje huku wakiahidi kuja na tamko kali kuhusu udhalilishaji waliofanyiwa huku naibu spika tulia akifurahia tukio hilo

Souce breaking news na radio one
Tulia ilibidi awasikilize maana kweli wamedhalilishwa. Yeye ni mwanamke naye ajue kuwa huku mitaani wanasema naye ni mkumbo huo huo! Ilibidi aungane nao kukemea udhalilishaji huo!
 
Aliyesema hivyo amesahau zile nafasi za Ukuu wa wilaya ndani ya ccm? Ama kweli Tanzania kuna mambo!!!!!!! Ngonja niende nitarudi baadaye.
 
uyu Naibu spika hafai kabisa Rais naomba ujutie uamuzi wako wa kumbeba mtu asiebebeka
 
Back
Top Bottom