Naibu Spika atumia mil 20/- kumshukuru Mungu

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,502
3,483
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson ametoa Sh. milioni 20 na zawadi mbalimbali kwa jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya, ikiwemo shule ya walemavu wa mtindio wa ubongo na albino kama shukrani kwa Mungu.

Kitendo hicho cha kutoa zawadi ya zaidi ya Sh. milioni 20 kilipongezwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Zainab Mbusi, ambaye alisema amefarajika kuona mbunge huyo amefika wilayani humo na kusaidia shughuli za kijamii hasa katika shule, Kanisa na vikundi vya wajasilia mali.

Alisema katika Shule ya Msingi Mabonde alikosoma, Dk. Tulia alitoa Sh. milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa majengo na katika Shule ya Sekondari ya Loleza ya wasichana Mbeya alikosoma pia, alitoa Sh. milioni 5.

Mkuu wa Wilaya huyo alisema Naibu Spika alisaidia pia walemavu wa mtindio wa ubongo na albino Sh. milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa uzio kwenye jengo lao.

Mbusi alisema amepewa kazi ya kuhakikisha anasimamia fedha hizo ili zitumike kama zilivyokusudiwa na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa Dk. Tulia kwa kukumbuka kwao na kusaidia shughuli hizo na kupunguza changamoto zilizopo.

Katika hatua nyingine, DC huyo aliahidi kuitisha harambee kwa wadau kwa ajili ya kutafuta fedha zitakazotumika kununua madawati ili kupunguza upungufu wa madawati wilayani humo ambapo katika halmashauri ya Rungwe pekee yanahitajika 8,000.

Alisema katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, ametafuta wadau ambapo Shirika la Kimarekani la Africa Bridge limetoa madawati 2,000 huku wadau wengine akiwemo mfanyabiashara anayemiliki mabasi, Yona Sonelo wameahidi kuchangia.

Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ili kuondoa tatizo la madawati linalopelekea wanafunzi kukaa chini na kuwa nyuma kulinganisha na wilaya za mikoa ya kaskazini ambazo zimepiga hatua katika sekata ya elimu.

Chanzo: Nipashe
 
Dr.Tulia ni mlokole na tumefanya naye kazi hapa mahakamani.Ametumia kanuni ya fungu la kumi kurudisha kwa Bwana Yesu/Mungu ndo maana kafanya hayo,Wengine tuige mazuri yake,Mauza uza yake tuyaache
fungu la kumi 20m! good job mydear.
 
Kama Sh. 20 milioni ni FUNGU LA KUMI (10% ya pato lake) maana yake pato lilikuwa ni Sh. 200 milioni!! Aisee, kweli ndiyo maana watu wanauwana kwa sababu ya vyeo.
 
Kichwa cha habari kilitakiwa kuwa "naibu spika atoa misaada ya 20m kwa taasisi mbalimbali" kumshukuru Mungu ni kusali
 
Fungu la kumi la kipato chake maana yake ni nini,kama ametoa sh 20M maana yake kipatao chake ni zaidi ya sh. 200M .kwa mwaka. Ambapo sasa pasipo shaka inatupa wastani wa zaidi ya sh. 10 kwa mwezi. Je mshahara wake ni mkubwa kuliko wa Rais wake. Au, hiyo fungu la kumi linatafriliwaje. Nitashukhru kama kuna mtu atajitokeza na junifafanulia.
 
Dr.Tulia ni mlokole na tumefanya naye kazi hapa mahakamani.Ametumia kanuni ya fungu la kumi kurudisha kwa Bwana Yesu/Mungu ndo maana kafanya hayo,Wengine tuige mazuri yake,Mauza uza yake tuyaache
Kumbe? mlikole ndo anakuwa hivo? Mnawatamanisha watu kwenda motoni nyie
 
Dr.Tulia ni mlokole na tumefanya naye kazi hapa mahakamani.Ametumia kanuni ya fungu la kumi kurudisha kwa Bwana Yesu/Mungu ndo maana kafanya hayo,Wengine tuige mazuri yake,Mauza uza yake tuyaache

Mlokole? Mlokole kaingiaje chama cha wapigaji?hamna cha ulokole wala ukoloni
 
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson ametoa Sh. milioni 20 na zawadi mbalimbali kwa jamii wilayani Rungwe mkoani Mbeya, ikiwemo shule ya walemavu wa mtindio wa ubongo na albino kama shukrani kwa Mungu.

Kitendo hicho cha kutoa zawadi ya zaidi ya Sh. milioni 20 kilipongezwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Zainab Mbusi, ambaye alisema amefarajika kuona mbunge huyo amefika wilayani humo na kusaidia shughuli za kijamii hasa katika shule, Kanisa na vikundi vya wajasilia mali.

Alisema katika Shule ya Msingi Mabonde alikosoma, Dk. Tulia alitoa Sh. milioni 5 kwa ajili ya ukarabati wa majengo na katika Shule ya Sekondari ya Loleza ya wasichana Mbeya alikosoma pia, alitoa Sh. milioni 5.

Mkuu wa Wilaya huyo alisema Naibu Spika alisaidia pia walemavu wa mtindio wa ubongo na albino Sh. milioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa uzio kwenye jengo lao.

Mbusi alisema amepewa kazi ya kuhakikisha anasimamia fedha hizo ili zitumike kama zilivyokusudiwa na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa Dk. Tulia kwa kukumbuka kwao na kusaidia shughuli hizo na kupunguza changamoto zilizopo.

Katika hatua nyingine, DC huyo aliahidi kuitisha harambee kwa wadau kwa ajili ya kutafuta fedha zitakazotumika kununua madawati ili kupunguza upungufu wa madawati wilayani humo ambapo katika halmashauri ya Rungwe pekee yanahitajika 8,000.

Alisema katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa, ametafuta wadau ambapo Shirika la Kimarekani la Africa Bridge limetoa madawati 2,000 huku wadau wengine akiwemo mfanyabiashara anayemiliki mabasi, Yona Sonelo wameahidi kuchangia.

Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ili kuondoa tatizo la madawati linalopelekea wanafunzi kukaa chini na kuwa nyuma kulinganisha na wilaya za mikoa ya kaskazini ambazo zimepiga hatua katika sekata ya elimu.

Chanzo: Nipashe

Kumbe TAARIFA Imeletwa Na Gazeti La Nipashe? Sishangai! Halafu Naomba Kuwauliza Hawa Nipashe Hivi Mbona Huwa HAWAANDIKI " Taita " Wao Mr. Many Anapowachezesha Shere Nduguze Haji Manara Na Wale Wenye Nguvu Za Kifuani Sana Pale Diamond Jubilee Kila Mwaka Na Kutumia Picha Zao Kujipatia FEDHA Kutoka Kwa WAFADHILI Wake Wa Ulaya Hasa Nchini Uingereza?
 
Dr.Tulia ni mlokole na tumefanya naye kazi hapa mahakamani.Ametumia kanuni ya fungu la kumi kurudisha kwa Bwana Yesu/Mungu ndo maana kafanya hayo,Wengine tuige mazuri yake,Mauza uza yake tuyaache

Big up mlokole Dr. Tulia. Tunatarajia utamuweka mbele bwana yesu katika kutenda haki pale bungeni.
 
Dr.Tulia ni mlokole na tumefanya naye kazi hapa mahakamani.Ametumia kanuni ya fungu la kumi kurudisha kwa Bwana Yesu/Mungu ndo maana kafanya hayo,Wengine tuige mazuri yake,Mauza uza yake tuyaache
Duh
Mungu amzidishie, ikiwa ni 10% zimetoka ina maana aliingiza shs.200m, sio haba sana japo hatujui hio 200m ni kwa kipindi gani - hiki cha usipika au kaunganisha mapato yake yote tangu alipokuwa mwanasheria wa serikali au kabla. Mungu azidi kumbariki naibu spika wetu.
 
Dr.Tulia ni mlokole na tumefanya naye kazi hapa mahakamani.Ametumia kanuni ya fungu la kumi kurudisha kwa Bwana Yesu/Mungu ndo maana kafanya hayo,Wengine tuige mazuri yake,Mauza uza yake tuyaache
Kwa hiyo analipwa mil.200 siyo!!?
 
Kumbe TAARIFA Imeletwa Na Gazeti La Nipashe? Sishangai! Halafu Naomba Kuwauliza Hawa Nipashe Hivi Mbona Huwa HAWAANDIKI " Taita " Wao Mr. Many Anapowachezesha Shere Nduguze Haji Manara Na Wale Wenye Nguvu Za Kifuani Sana Pale Diamond Jubilee Kila Mwaka Na Kutumia Picha Zao Kujipatia FEDHA Kutoka Kwa WAFADHILI Wake Wa Ulaya Hasa Nchini Uingereza?
Nadhani umeingia choo cha jinsia pinzani
 
Kumbe TAARIFA Imeletwa Na Gazeti La Nipashe? Sishangai! Halafu Naomba Kuwauliza Hawa Nipashe Hivi Mbona Huwa HAWAANDIKI " Taita " Wao Mr. Many Anapowachezesha Shere Nduguze Haji Manara Na Wale Wenye Nguvu Za Kifuani Sana Pale Diamond Jubilee Kila Mwaka Na Kutumia Picha Zao Kujipatia FEDHA Kutoka Kwa WAFADHILI Wake Wa Ulaya Hasa Nchini Uingereza?
Mbona unajificha nyuma ya kalamu? Andika kwa uwazi ujulikane, oh! Mr. Many.....nduguze Haji Manara. Huu ni UHUNI kama unahisi unaogopa cyber crime ujue ulikuwa na nia ovu. Waachie wenye dhamira safi waandika maoni yao.
 
Habari inasema ametumia 20M Kama michango kwa Taasisi tajwa ila naona wachangiaji wameugeuza kama fungu la 10,kinyume cha habari,
Nadhani anajiwekea mazingira ya kuja kugombea ubunge wa Jimbo 2020.
 
fungu la kumi 20m! good job mydear.
Ndiyo Kama Mungu, Amekubariki Ml 200 Kwanini Usimpe Fungu lake la 10 Ambalo ni 20 ml? Watanzania tujufunze kumwesimu Mungu katika Kipato Chetu, ili Tuzidi kufanikiwa. Bg Up Dkt Tulia.
 
Fungu la kumi la kipato chake maana yake ni nini,kama ametoa sh 20M maana yake kipatao chake ni zaidi ya sh. 200M .kwa mwaka. Ambapo sasa pasipo shaka inatupa wastani wa zaidi ya sh. 10 kwa mwezi. Je mshahara wake ni mkubwa kuliko wa Rais wake. Au, hiyo fungu la kumi linatafriliwaje. Nitashukhru kama kuna mtu atajitokeza na junifafanulia.
Sio lazima iwe ni kutoka kwenye mshahara wake anaweza akawa na vyanzo vingine vya mapato.
 
Back
Top Bottom