aimi lyatuu
JF-Expert Member
- Dec 7, 2015
- 765
- 848
Hapana ni wazo la hovyo kabisa...kumbuka umeshaweka Alama za vidole kwenye hilo Pochi...... Na Kama ni kweli ikitokea aliyelipoteza aliuwawa kwa Alama hizo wewe nawe utahusishwa na tukio hilo na kukupata ni rahisi Kuna kitu Kama Kitambulisho cha Taifa, usajili wa Laini za simu Alama zako za vidole zipo.......Wakuu nimesoma coment zote hizi jibu ni moja nililo lipata kwamba kutokana na "intelijensia" ya nchi yetu hili swala laweza kuwa dogo machoni kwangu ila baada ya kulifanya naweza nikajiachia alama ya kutosha katika maisha yangu yote.
Naitupa usiku kwa wale wafagia barabara kijanja!!
Asanteni wakuu!!
Tanzania ni nchi mbaya sana kuishi. Nchi nyingine, hapo unampigia simu mwenye pochi, anachukuwa pochi yake ikiwa na kadi na pesa zake kabisa. Ama unaipeleka polisi kama mwenye pochi hapatikani. Akikupa zawadi unaikataa kwa vile hata wewe pia ungeweza kupoteza kitu akakiokota yeye na akakupa bila malipo. Hata polisi hawaaminiki. Eti kisiwa cha amani! Maoni yaliyokwishatolewa yanasikitisha sana. Utaokotaje passport za wenzako halafu unakwenda kuzitupa? Ubinadamu uko wapi? Mungu wetu ataamua mengi siku ya hukumu!
Hapana ni wazo la hovyo kabisa...kumbuka umeshaweka Alama za vidole kwenye hilo Pochi...... Na Kama ni kweli ikitokea aliyelipoteza aliuwawa kwa Alama hizo wewe nawe utahusishwa na tukio hilo na kukupata ni rahisi Kuna kitu Kama Kitambulisho cha Taifa, usajili wa Laini za simu Alama zako za vidole zipo.......
Mimi nakushauri ni Bora Mara 10 nenda polisi waeleze nadhani watakuelewa......
Siku nyingine ukiona kitu kama hicho usikimbilie kushika peleka taarifa Polisi.......
Wachaga bhanaa.......!!!!!
Umefanya vizuri kuomba ushauri, achana na hao wanaokuambia nenda katupe kwani Dunia ina mengi unaweza kuona uko peke yako sehemu Kumbe kuna mtu anashuhudia unachofanya na ikitokea ameenda kutoa taarifa polisi na kukutaja wewe hiyo itakula kwako hitakuwa na cha kusema.......ndipo hapo utakapohusishwa na tukio lolote lililompata Mwenye hiyo pochi......Ila mkuu mpaka muda huu nimepitia viama mbalimbali pia nimeshuhudia watu waliopitia moto kwangu hiyo ni kitaaolojia...na kweli nimelisachi vya kutosha kama ni alama ya vidole nimeacha kwa kila kitu kilichomo mule kwenye pochi na hili ndilo limenifanya niombe ushauri hapa jamvini