Nahitaji ushauri wenu

Wa kusoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Posts
3,454
Reaction score
2,984
Jamani mm nataka kwenda Angaza lkn nashindwa nianzie wapi. Tatizo ni kwamba zamani nilikuwa siugui kabisa lkn kwa sasa homa na mwili kukosa nguvu ni kawaida. Nawaza sana khs kwenda kupima afya tangu 2007 lkn naogopa. Nifanyeje jamani na nitamwambiaje mpenzi wangu?
 
Hehehehe dogo hujambo?
Tulia ukiwa tayari kifikra utaenda
 
Tuulize habari ya kupokea majibu! Kupima haina shida!
 
Kupima simpo sana, tatizo ni kupokea majibu. Unapaswa kuwa mshauri nasaha wa nafsi yako kwa maana ya kujikubali na kuwa na utayari, na uwe tayari kwa outcome. Kuna time I was kijump way nikaenda kupima, majibu palichimbika. Good luck it was NEG.
 
woga ni fikra tu uliyoipa kipaumbele akilini mwako...jitahidi uwe na mawazo chanya juu ya maisha yako pasipo kujali aina yoyote ya majibu utakayopokea.
 
Hakuna kitu kizuri kama kujua afya yako, sasa kama unaogopa majibu, subiria uumwe ule usio na dawa na dunia yote itakutambua, maana dhoruba yake lazima ikulaze si chini ya mwaka ndo afya irudi, bora upime wakati una afya yako hata kama unaumwa ,unaanza kunywa dawa taratibu

nina ndugu yangu kaishi kwa wasiwasi kama wako miaka kama saba tangu mumewe afariki, only to find out last month kwamba hana ugonjwa huo hajaamini,kaenda hospital kama tatu, lakini sasa ungemwona kabla,alikuwa tayari kadhoofu,hana raha ,kaacha shule njiani,sababu alijua anakufa,pima ujijue ndugu yangu
 
Hospitalini huwa siendi na hata kama nikiugua homa naanza kuhofia nakuwa na wasiwasi kweli jamani, kuna siku nilijihisi nina malaria nilivyoenda Dispensary wakasema sina malaria kidogo nizimie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…