Nahitaji ushauri na hekima zenu

FUTURE HUNTER

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
2,112
Reaction score
2,822
Kuna binti mmoja tulipendana huko miaka ya nyuma around 2013.Ni binti smart na wife material mno though binafsi nilijikuta moyo baadae hauridhiki na mwonekano wake.
Basi kama mjuavyo moyo usiporidhika utafanya namna ya kujikomboa ikatokea kutokuelewana basi mm nikamwacha.Alilia sana na laifanya juhudi mwaka mzima kurudi kwangu lakini sikugeuza shingo.
Sasa tatzo ni huyu binti ananipenda mno kiasi cha kwamba anai ni block na kufuta namba zangu lakin kichwani zinabaki na akijaribu relationship mpya huishia kuvunjwa moyo na analia sana.Mwishowe hunitafuta na kusema maisha yake hayana thamani.
Kazi haziendi,yaani anakata tamaa na ananililia sana mimi maana huenda ndio mwanzilishi wa haya yote.
Mpaka familia yake inabd wamtembelee kumfariji maana anakuwa kama anaumwa.
Naombeni ushuri na mawazo nimshauri vipi huyu ndugu aweze ku move on.mm bahat mbaya nina realationship mpya sasa najikuta naumia pia kwa hili.
Nisaidieni ushauri ndugu zangu.
 
Futa mawasiliano nae like badili namba yako ya simu ili asiweze kukupata tena,hizo relationship zake hazidumu coz still anakuwaza wewe na si ajabu sababu za hizo relation zake kutokudumu ni yeye mwenyewe,

Ulikosea sana "kumpenda" kisha ukamwaga eti hukuridhika na muonekano wake! kwani hukuliona hilo toka mwanzo? bila shaka hata wewe ulianza kumcheat na kua na mwingine ndio maana ukamcompare na huyo aliyekua mpenzi wako na ukaona hana muonekano,kujua kizuri na kibaya ni lazima utakua umefanya comparison.
 
Kwani mwanzo wakati unamtongoza hukumuona km hakufai mpk umvue chupi mtoto wa watu ndo uone kasoro.... Yaan hiyo ni laana unaitafuta mkuu
 
Ni kweli mkuu kosa nililifanya toka awali nile man ship tu.
Mawasiliano yake mm huwa sinaga yeye ndio anayo tena kichwan.
Kubadili namba n changamoto nimeitumia katika taasisi muhimu kama namba yangu official
 
Hajakubaliana na hali kwwmba ameachwa nashida kua ni wewe pia bado wamu entertain

Kama mtu humtaki unaanzaje kuumia kwa hali yake mwache alie aumwe mapenzi hayalazimishwi

Unapomuacha mtu muache kweli kweli we ukipigiwa unapokea na kusikiliza anavyolia mwisho useme uumie

Hakuna linalodumu kuna siku ataweza kwenda mbele akitaka sasa hivi bado hajataka na inashauriwa kama unaachwa ulie kweli kweli utoe huo uchungo kwa hiyo msaidie badili namba hata akikutafta asikupate
 
This is what gonna happen next.

Atakusahau kabisa, na akisha kusahau na wewe ndio utaanza kumkumbuka na kumpenda.

And guess what, kipindi icho atakua na mtu wake wala hatakuelewa tena.

Hayo ndo mapenzi mkuu, its a circle.

Source: My experience.
 
Wewe mpotezee moja kwa moja.
Hamna namna unayoweza kumsaidia.
Maana hauwezi kurudiana naye kwa sababu tayari una mtu wako.
Ukiachana na mtu songa mbele , usirudi nyuma.
Unaweza ukaona anakulilia kumbe anataka revenge.
 
Aisee nashukuru madame S mm huwa namba zake sinna but yeye kila akinitafuta basi ni kilio namba zangu haziwezi kumtoka kichwani anazo.
Kubadili namba changamoto n kuwa sehemu nyingi za kiofisi hii namba ndio natumia
 
Du
 
Wewe mpotezee moja kwa moja.
Hamna namna unayoweza kumsaidia.
Maana hauwezi kurudiana naye kwa sababu tayari una mtu wako.
Ukiachana na mtu songa mbele , usirudi nyuma.
Unaweza ukaona anakulilia kumbe anataka revenge.
Mimi nisha move on kitambo sana lakin tabu n hapo kwa mwenzangu yaan kama sasa it has been a year toka alinitafuta last time akiwa na furaha sana kuwa 2020 ataolewa nikampongeza na kumuombea heri.
Kanitafuta tena karibuni ikiwa n vilio na majonzi kiasi cha hata kushindwa kazin mpaka majirn imebed waite wazazi wake waje kumshauri.
Inaniuma na mm pia kuona hali hyo ndio maana natafuta namna bora nimshauri vipi ili aweze kuaonga mbele vzur
 
Kwani mwanzo wakati unamtongoza hukumuona km hakufai mpk umvue chupi mtoto wa watu ndo uone kasoro.... Yaan hiyo ni laana unaitafuta mkuu
Hapana mkuu kuna mda hivi vitu vinatokea.Najutia kumuumiza pia lakin najisikia vibaya yeye kila anapopatwa na msuko msuko analia sana na kuvunjika moyo na huishia kunitafuta akilia na kudai mm ndio chanzo cha yote maana ndio nilikuwa first love wake.
 
Mrudie mkaishi huyo ndiye anayekupenda kuliko michepuko yako yote,
Huyo ndiye atakayevumilia shida zako zote,
Huyo ndiye atakayekufanya uwe na karibu na Mungu,
Huyo ndiye atakayefanya uwe na mafanikio kimaisha,
Huyo ndiye huenda ikawa chaguo lako.
Na huyo ndiye anaweza kukucare kwa kila namna couse anajua thamani na nafasi yako kama mwanaume.
Pia huyo ndiye atakayefanya ufurahie maisha yako yote na watoto wako, usiendelee kumwumiza muite mwambie yamekwisha!

Mwisho kabisa; ni bora kupendwa kuliko kupenda.
 
Dah pole mkuu watu km hao nishakutana nao ila sometimes inabid umove on bila huruma unaeza ukajikuta unavunja relationship yako mpya kisa huruma so kaa nae mbali vaa sura ya mbuzi tu
Hapana mkuu kuna mda hivi vitu vinatokea.Najutia kumuumiza pia lakin najisikia vibaya yeye kila anapopatwa na msuko msuko analia sana na kuvunjika moyo na huishia kunitafuta akilia na kudai mm ndio chanzo cha yote maana ndio nilikuwa first love wake.
 
Ni kweli ndugu ana sifa zote hizo ila sasa mimi tayar nina mtu mwingine na tuna mipango ya kuoana.
Kwa hali anayopitia ningeweza rudisha moyo nimuoe tu abaki hata wife home though deeply sijakubali full.lakin sasa nina mtu mwingine tayar
 
Usidanganyike na vilio vya mtu.
Sio kila kilio ni kilio vingine unafki tuu ili unase kwenye mitego yake.
Hamna unachoweza msaidia zaidi ya kumpotezea mkuu.
 
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…