Nahitaji Software inayobadili sauti kuwa maneno

Natafuta matibabu

JF-Expert Member
Aug 1, 2020
262
301
Salamu kwa wana JF wote, husika na kichwa cha Habari.

Nina uhitaji wa SOFTWARE ambayo inabadili sauti kuwa maneno. Hii software inatakiwa iwe ni ya ku Install kwenye Computer au Kishikwambi. Iwe na vifaa kama Microphone ambayo mzungumzaji atakuwa anaivaa mithili ya zile ndogo za Makocha wa Mpira, kifaa cha kupeleka signal kwenye Computer kama kile cha Mouse zisizokuwa na wire.

Mzungumzaji akiongea signal za Sauti zipelekwe kwenye Computer kwa mtindo nilioueleza halafu zikabadilishwe kuwa maneno kwenye Microsoft word ambayo utakuwa umeifungua kwa muda ule au system yeyote ambayo hii software itakuwa inaitumia.

Jinsi Technology inavyozidi kuchanja mbuga siamini kama kitu hiki hakipo ingawa sijasikia bado.

Wanajamvi naombeni muongozo kuhusu hili.

Asanteni!
 
Moderator nimewaomba uzi ubaki jukwa la Habari mchanganyiko ili utembelewe haraka.

Mkaukimbiza huku, ona sasa zimepita dk 52, uzi una view 23 tu.

Anyway, ndio majukumu yenu hayo, ngoja niendelee kupambana na hizi view chache naweza kusaidika
 
Ipo, ila usitegemee ikafanya kazi kwenye kiswahili
Nimejaribu kupita mtandaoni nimeona zipo kama vile google speech detector, ni kweli kwenye kiswahili haifanyi kazi ila kwenye kiingereza inafanya kazi lakini iwe ni maneno yaliyonyooka, yaani yaliyotamkwa vizuri kama yanavyostahili ndio yataweza kubadilishwa.

Sasa nimefikiri labda naweza kupata ambayo inafanya kazi vizuri ndio nikamua kuulizia huku
 
Zipo nyingi ila Kwa Kiswahili ni shida mkuu. Najua unafanya transcribing so the best way ni kurecord sauti then wape watu wafanye transcribing
 
Unacho hitaji wewe ni "Speech to text" Software, Programu ya AI inayobadili sauti kuwa maneno

Hizi zipo, lakini kuipata inayoelewa lugha yako ya kiswahili ni ngumu, kwa sababu moja kuu,

Kampuni na developers wanaounda na kuboresha programu za namna hii wanatokea kwenye nchi zinazo zungumza kingereza

Developers wa hapa ni aidha hawana interest au computing power na data za kutengeneza programu za namna hio.
 
Zipo nyingi ila Kwa Kiswahili ni shida mkuu. Najua unafanya transcribing so the best way ni kurecord sauti then wape watu wafanye transcribing
Ni kweli nataka kufanya transcribing hasa kwenye matukio muhimu ambapo mzungumzaji anakuwa mmoja, hata pia nikitaka kuzungumza na mtu ishu muhimu niweze kumuwekea kifaa halafu mimi niangalie computer.

Ipo kwenye computer kupitia Microsoft word nimeijaribu ila hakuna ufanisi maana inataka maneno yatamkwe ipasavyo kwa kiingereza jambo ambalo linakuwa gumu kutokana na lafudhi tofauti.

Kwa kiswahili haiwezi kunasa maneno kabisa inaiishia kuandika kwa kingereza tu neno lolote inalohisi ndio lenyewe.

Hii fursa kwa Madeveloper wakijipinda wataweza kufanya jambo, hii technology inaweza kuwa msaada kwa wanaosikia kidogo halafu wanaweza kusoma, kwani hadi sasa hamna vifaa vyenye ufanisi vinavyosaidia kusikia.
 
Unacho hitaji wewe ni "Speech to text" Software, Programu ya AI inayobadili sauti kuwa maneno

Hizi zipo, lakini kuipata inayoelewa lugha yako ya kiswahili ni ngumu, kwa sababu moja kuu,

Kampuni na developers wanaounda na kuboresha programu za namna hii wanatokea kwenye nchi zinazo zungumza kingereza

Developers wa hapa ni aidha hawana interest au computing power na data za kutengeneza programu za namna hio.
Developer wa Kiswahili wakiamua wanaeweza kufanya jambo la muhimu ila bado hawajatambua hii fursa
 
Changamoto ni kwamba inashndwa kubaini maneno ipasavyo labda yatamkwe vizuri kwa lugha ya kiingereza, kiswahili haiwezi
Kazi yako itakuwa kuEdit yakae sawa, ila si kwamba haifanyi kazi. Ni kama ukichukua document ukataka Google translator ikutafsirie kwa kiswahili, itafanya ila itabidi uiweke sawa ieleweke.
 
Back
Top Bottom