Kupata pos ya NMB ni nightmare, nimefuatilia karibia mwaka toka Nov 2020, nimekuja pata mwaka jana Dec, nayo si mpya waliichukua kwa mtu alikuwa hafanyi vizuri wakamnyang'anya, imetumika sana hata baadhi ya button zimefutika.
wakati naendelea kufuatilia bank nikaona nijiongeze, nikanunua pos kwa wakala, kumbe ile pos ilikuwa imefungwa alikuwa haitumii bank waka-block huko huko , nimefanya jitahada kuifungua ila sijafanikiwa imebaki tu kama pambo, mashine ni bado mpya kabisa. Niliwapelekea bank waifungue wakasema mchakato wake ni mrefu haf wao hawatambui huo utaratibu niliotumia kuipata