Habari wakuu. Kuna sehemu hapa bongo wanauza Hifi (High Fidelity) speakers? Nahitaji spika ndogo za kuweka juu ya kabati ( Wazungu wanaita bookshelf speakers) au speaker za kusimamisha ndani ya nyumba.
Sitaki hizi speakers za Wachina zilizozagaa kila duka. Nahitaji Real Hi fi. Iwe Used au mpya. SPeaker kama za Bose, B&W, JBL, NHT, Wharfedale, Audio Engine, Polk Audio, Klipsch, Acaustic Energy, Boston Accaustics au kampuni yoyote iliyobobea kwenye utengenezaji wa music systems.
Na hitaji small speaker but with big power, deep and tight bass.
Naombeni msaada wenu.