Habari wadau, Naomba msaada kwa mtu yeyote anaejua wapi naweza pata watoto wa nguruwe Mwanza. Nahitaji kununua Kama 30-50 inategemea na bei Kama tutaelewana. Naomba namba au ni PM. Natanguliza shukurani
Nguruwe ni wanyama wanaoishi kifamilia. Ukiwachanganya wa makundi tofauti hupigana na kuleta vifo. Idadi ya nguruwe 5-7 kwa kila banda la mita 8 za mraba hula na kuishi vizuri. Hawaishi kama n'gombe kwenye zizi moja. Nakushauri uanze na nguruwe wachache eg 10. Nguruwe huanza kuzaa akiwa na miezi 8. Huzaa baada ya siku 93-95 na unaweza kuwaachisha baada ya siku 60. Mwezi baada ya kumwachisha anaweza kupandwa. Kwa hali hiyo ndani ya mwaka waweza kuwa na zaidi ya hamsini. Pia kuanza na wachache utapata uzoefu wa utunzaji.