Nahitaji msaada wenu

Mpaka nimefikia hatua hii ya kuandika uzi huu ni kwamba nimekwama sina jinsi siwezi kukopa kwani sina uhakika wa kulipa pesa nahitaji wanangu na mama yao wapate kula. Kazi kupata ni ngumu na vibarua vimekuwa mtihani. Kwa atakaewsza nisaidia naomba tuwasiliane Pm. I really need your help.
 
Mkuu samahani? Hela ya Bando umeitoa wapi? kwa nini Usingeiacha nyumbani? au Umeazima simu ya Mtu? Samahani lakini kuuliza siyo ujinga
 
pole sana kwa unayopitia yanamwisho. ila swali ushafikiria hata kufanya kazi nje ya taaluma kama kuendesha bodaboda na zinginezo?
 
Mkuu samahani? Hela ya Bando umeitoa wapi? kwa nini Usingeiacha nyumbani? au Umeazima simu ya Mtu? Samahani lakini kuuliza siyo ujinga
mkuu natumia free basics. Hiyo pesa ya kununu MB ingetosha zaidi kuwaachia nyumbani wakapata hata maandazi asubuhi ikapita tukajuwa ya mchana mkuu.
 
Mkuu samahaniHuwezi fungua hata Tution Centre mahala ulipo Mkuu Samahani lakini mimi ni mdadisi tu kidogo
Mkuu haina haja ya kusema samahani nashukuru kwa hili pia nilishafanya tuition japo haikiwa na mafanikio, mazingira niliyopo muamko wa elimu ni mdogo sana nilipata watoto watatu ambao nilikuwa ninawafundisha na ukizingatia masomo niliyochukuwa si yenye uhitaji sana wa tuition kwa ngazi ya o level.
 
pole sana kwa unayopitia yanamwisho. ila swali ushafikiria hata kufanya kazi nje ya taaluma kama kuendesha bodaboda na zinginezo?
sina ujuzi wa kuendesha pikipiki mkuu na kusema ukweli sikulifikiria hili. Shukran kwa wazo mkuu
 
Alafu mkuu hayo mawazo ya kujiua tupa kule,
Shida yako ni ndogo sana,stand as a man..mwanaume ni kupambana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,ungekuwa na dar kuna mtu ningekuunganisha nae mpambane pamoja,tanga parefu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu maisha popote na mwanaume ni kupambana bado sijakata tamaa mkuu nitakutafuta mkuu ili niipate hiyo connection. Wacha kwa leo mkuu nipambanie ugali wa watoto mkuu. Shukran sana
 
Alafu mkuu hayo mawazo ya kujiua tupa kule,
Shida yako ni ndogo sana,stand as a man..mwanaume ni kupambana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafight sana though sometimes mambo yanakuwa hayaendi kama hivi kichwa knapata moto mkuu wanangu bado wadogo. Can you imagine bro mpak kula inakuwa mtihani. Mpaka nafikia hatua ya kuanzisha uzi ili nipate msaada. Nafight mkuu. Shukran sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…