Nahitaji msaada wa kusonga mbele

angelita

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2013
Posts
3,017
Reaction score
2,446
Miaka minne tangu niachane na aliyekuwa mpenzi wangu, Mwanaume ambaye nilizani ndiyo Omega wangu. Kweli mapenzi yanaumiza sana, naomba niwe mkweli Leo sababu ilifika kipindi nijiue. Mimi najua moyo hupenda mara moja tu mara mbili au tatu bahati. Mimi ni mrefu kwa kweli ila sikuwahi kutamani kudate mwanaume mfupi, hadi siku ilipotokea automatically.

Jeuri yangu na kiburi ilikwisha hapo, nilizama mazima. Ila baada ya Jamaa kujua sihemi sipumui mateso mtindo mmoja sababu anajua sichomoi. Ndipo nilipoamua kutulia kwa mume wa mtu ( si kwa kupenda kupunguza machungu) baadaye kwa sex partner hela kila kitu nilipata kwa mume wa mtu ila kuna kitu nilikosa thus why nikadate mtu mwingine.

Now niko kwa mahusiano ila sina mapenzi, Moyo bado uko kwa yule wa kwanza. Miaka minne sasa nimeshindwa kumtoa Moyoni. Nahitajimsaada niweze msahau mana nimejaribu nimeshindwa.

Wale warusha mawe tafadhari maana hapa Duniani hakuna mkamilifu
 
Sahau tu, jaribu kutembelea sehemu hospital kama wodi namba Tisa iv, utamsahau tu
 
Miaka minne bado unaumia rohoni?Kwanini ujitese kwa mtu ambaye hata hakuwazii kwa lolote?My dia unatakiwa sometimes uwe na moyo mgumu wa kukubali matokeo na kuendelea na maisha.

Hii dunia kuna mambo mengi tu ambayo unatakiwa uyatimize na sio lakubebelea machungu ndani ya moyo wako.Huo hakuwa riziki yako inabidi ukubaliane na hilo na uendelee na maisha yako.
 
Mamy pole Sana Ila nikushaur jambo kuwa Kama unaweka effort juu ya kumsahau unamsahau tu kwanza ukubali kua si wako tena labda Kama hua mnawasiliana nakujua aliposimamia now vinginevyo msahau tu miaka minne mingisana aisee na bado hujasahau kubali matokeo tu endelea na mambo yako
 
Kwani was your break up hostile ama amicable? If the former then maybe Jaribu kumtafuta uongee nae, it could be roho inauma na haijatulia because you never had closure? It's always best for one to face their demons (whatever they maybe) rather than trying to pretend they don't exists ! Plus that strategy has already failed anyway so........
 
Pole sana my sister.. As for me nakushauri kila ukiwa unamkumbuka huyo Ex usimkumbuke kwa mazuri Bali kwa mabaya aliyokutendea it probably will help you to move on . Another thing find a peace in your heart by praying ili Mungu akujaze Peace na kukusaidia Ku move on na maisha yako.

Forgive your Ex and yourself to welcome Peace .Na pia try to keep busy ,by focusing on what God is about to do for you in the next chapter that you have already started to open ... Focus on your present and future , and try to forget about your Past ..

. Na kama utaweza Siku moja ukijisikia vizuri na unayo Peace moyoni mwako after forgiving him , mtafute na umuambie that you have forgave him... This will help your burden out ... and make you free from that Cage
.. Thanks..
 
Okoka tu, mida ka hii uko busy na kanisa! After all, all 6b pipo in the globe wako na bado huyo 1 anakupetrify? Try to shun away from those reminisce, I had mine for 8guda years, we broke and thereafter it was just a humdrum kinda of relationship!

Dont get infatuated with the past, focus on ur current fetish man! Otherwise you will haunted with that memorabilia for good and its really disgusting! Anyway pole sana
 
"No longer at ease" ukijiamini unaweza Kwanzaa sema na kili moyoni kuwa si wako tena..ukikili tu soon utamsahau
 
Usijisumbue na huyo mtu, try to grow up and grow out of that cocoon. Wewe mwenyewe umesema kuwa alipojua unampenda sana, akaanza kukunyanyasa, sasa unadhani ukijirudisha now, atafanya nini?

Ukizingatia kuwa itakuwa imemthibitishia kuwa huwezi kupata mwingine kama yeye.
Wanaume wengine, confidence iko low, hawajui kupokea penzi na akipendwa akagundua tu anakuwa kama mwehu na mwanamke atakoma sana kuringa.
 
Unajua kupenda wewe, hongera. Tatizo la kushindwa kumsahau ni wewe kuingia kwenye mahusiano na watu wasioweza kukupa faraja (mume wa mtu n.k).Tafuta jukwaa Litakalokufanya upate aina ya mtu mwenye kukupa faraja. Kwa namna ilivyo umeshuka "farasi ukapanda punda", ni ngumu kumsahau.
 
DUNIA ni sehemu yenye kupendeza na kufurahisha ikiwa tu utachagua kuishi kuenenda na hali halisi na si kwa matakwa ya msukumo wa nafsi yako...mapenzi ni sehemu ndogo ya maisha yetu ya kila siku lakini mapenzi peke yake hayakimilishi maisha yetu...

.Mioyo yetu inapoanguka penzini hutuvika upofu hata tusione upande mwingine wa furaha katika maisha yetu...hutufanya tuwe watumwa ndani ya fikra zetu wenyewe kiasi cha mtu kuamini hawezi kuishi bila ya uwepo wa mtu Fulani hapa duniani.

..Lakini haya mateso huwatokea wale wote waliochagua mihemko yao kuwa ndio dira zao ziongozayo maisha yao...na wanaokataa kuishi kulingana na hali halisi ya mazingira yaliyopo sasa...Tiba pekee ni kuukubali ukweli na kuishi kuenenda na ukweli huo...na hapo ndio utakapoona dunia ikiwa kama PARADISO yenye kuvutia na kupendeza...
 
Jiulize madhalani akipatwa na umauti je bado utaendelea kumuhitaji? Jaribu kufikiria kitu kama hakipo kabisa je huwezi kuishi pia. Mi nadhani una nafasi nzuri ya kusonga mbele
 
Be honest, ni kitu gani huyo current boyfriend hana ambacho yule wa zamani alikuwa nacho? Is it money, fame, loyalty au yule wa zamani alikuwa vizuri kunako faragha kuliko huyu?
Lazima kuwe na sababu inayopelekea wewe kumkumbuka 'miaka minne'.
 
angelita

Hii stori yako imenikumbusha mbali sana!! Have you ever been at mzumbe??
 
Last edited by a moderator:
Pole waone wataalam wakufanyie cancelling. lkn kosa ulilolifanya ni kutafuta mtu wa kufutamachungu. ulitakiwa upumue kwanza kabla hujasonga mbele. nahis umekutaba na kombe la mbuz wakat pimbi alikua kombe fifa
 
Jiulize ndoto yako kubwa katika maisha yako ni ipi?

anza kuifuatilia ndoto yako ya maisha utaanza taratibu kusahau
 
angelita

Njoo tulime bustani huku, inalipa
 
Last edited by a moderator:
Nina sifa zote ulizoandika, Kama ni mimi basi nisamehe maana unajua exactly what happened between us! I am sorry lakini njoo tuyamlize japo ndio hivyo I am married.
 
Aisee we miaka NNE yote husahau?nadhani utakuwa mpaka umekonda kwa mawazo.
Pole sana
 
Pole,naelewa unapopita!!
Sikulaumu kuwa umepita huko kwa mume WA mtu,inatokea....I knw ,inacost Sana!!!

Ushauri wangu, jus accept it!!!
Yaani ukishindwa kukubali utateseka,BT once ukikubali hali halisi uta move on my dia!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…