Nahitaji kujua utofauti na ubora wa hizi aina mbili za biashara

olym

JF-Expert Member
Jul 25, 2019
265
449
Hello JF Members,

Natumaini wote mnaendelea vizuri, katika afya ya akili na mwili, naomba niende moja kwa moja kwenye mitizamo yangu miwili ambayo nimekua nikisoma sana threads za biashara na ujairiamali na baadhi ya tafiti ndogo ndogo za mtaani.

Nikaja na tafakari mbili ambazo kwa wingi wetu humu ndani, naweza sahihishwa vyema au kuongezewa mitizamo ilio chanya zaidi:

MOJA: BIASHARA YA KUSUBIRI MTEJA AU YA KUWAFATA WATEJA:
Kati ya hizi biashara za aina mbili, katika mtizamo wangu biashara ya kufata mteja inatija zaidi na inaruhusu mzunguko mkubwa tofauti na kusubiri mteja ambaye mara nyingi uwezi kuwa n auhakika nae, namaana kujua database ya wateja unaowasubiri ni ngumu kidogo ukilinganisha na wateja wa kuwafata ambao unajua kila mtaa nina mteja huyu na muelekeo/trend wake wa biashara ni upi,hapa natoa mifano miwili kama sio mitatu nieleweke usikute napiga pembeni.

Mfano wa kwanza, ufungue duka na phone accessories la 5M ukodi fremu uendelee kusubiri wateja, au uanze na 3M vifaa nyngne ununue usafiri km pikipiki uanze kuingia mtaani uwauzie wale wadogo wadogo wanaosumbiri wateja, chaguo la pili naona ni bora kwangu na inakupa mzunguko mkubwa na kupanuka ni rahisi ndani ya muda flani.

Mfano wa pili, Ukifungua mgahawa ukawa unasubiri wateja au kuendesha kwa mtindo wa kuwafata wateja na kuwazambazia bado naona wazo la kufata mteja alipo lina nafasi kubwa pia,
kwa hili mifano ipo mingi sana, unaweza fikiria mdau na mchangiaji wa hii mada.

MBILI: BIASHARA YA UWAKALA AU MZALISHAJI:
Pia katika mawazo yangu na maono kuna hivi vitu viwili naona kimoja kina limit ya ukuaji na ikishafika hiyo hatua unaweza kubaki hapo au utumie nguvu kubwa kuvuka maana kuna anae kunyima nafasi ya kukua kwenye kampuni, mfano wa uwakala unaweza kuwa wa huduma za kifedha, bidhaa kama bia,soda,maji, gesi za kupikia na zingine unapokua wakala wao bei unapangiwa na misingi mingi ya uendeshaji ni mipango yao na hata bei za sokoni zipo kwa ajili yao na sio wewe, kwa hili huwa naona ni ngumu kuufikia mwanja 1B US DOLLAR(Sio Ubilionea wa 1B Tsh) ukiendelea kuwa wakala wa makampuni.
Naona upande wa pili upo vizuri zaidi japo ni mgumu kwa uanzaji wake, masuala mazima ya mtaji ila una kuwa na njia nyingi za kushindana sokoni kama bei, matangazo n.k.

Bado naendelea kujifunza, maana pia ni wale wahanga wa kuanzisha biashara na kufa ila usimamizi umekua changamoto maana nipo kwenye ajira nashindwa kuchomoka kwa wakati ila njia yangu napenda sana iwe ya biashara, kwenye huu uzi ukinipa idea ya biashara kwa 3M kuna zawadi nono..Location Dar.

Karibuni magwiji wa mtaa kwenye masuala mazima ya utafutaji, mnitoe tongotongo kijana wenu.
 
Okay.....!!!

Idea mbona hii hapa umeandika.Ni suala la kuiboresha tu.

I assure you, it's one of the best overlooked idea you can ever imagine.

Pro Tip: FMCG(s) product (s)+ Branding and convenience.
 
FMCG(s) ni nini?
 
Back
Top Bottom