Nahitaji kufahamu bei ya pumba ya mahindi

Nahitaji kufahamu bei ya pumba ya mahindi

Mkuu kwa shinyanga kwa sasa kilo 100 inaenda 24K .sijajua maeneo yako
 
Alafu hilo neno PUMBA nililisoma vibaya aisee!

Sasa mkuu bei siinategemea wewe upo maeneo gani?
 
Wakuu naomba kujua bei ya pumba ya mahindi kwa gunia au kwa tani.
ni kweli utakuwa umehitaji KUJUA/KUFAHAMU maana Tanzania ni kubwa na ina mahitaji mengi tofauti. bila wewe kutaja unakopatikana utaambiwa bei za Tanga, Dar, Mara, Bukoba, Songwe na sijui kama itakuwa imekusaidia kufanta chaguo sahihi.

nawashukuru waumini wa JF sio wachoyo wamekumegea lau ukate kiu yako.

ongezea na hii:
-bei ya pumba ya mahindi haiwezi kufanana kote nchini, itategemea na mkoa, wilaya au kitongoji
-upatikanaji wa pumba unategemea kiwango cha mavuno ya mahindi kwa msimu huo
-bei ya mashineni (yanakokobolewa mahindi) ni ndogo zaidi kuliko wafanyabiashara mitaani/vibandani maana hawa huongeza bei kupata faida NA mashineni vijana/watumishi huiuza kama 'dili' yao kudokoa kwa maboss wao kabla ya hesabu
-msimu huu (msimu wa mavuno ya mahindi) watu wengi hukoboa ba hivyo pumba ni nyingi na bei iko chini kuliko miezi ya 9-12 na January.


JF walipata kunena, "AKILI ZA KUAMBIWA, CHANGANYA NA ZAKO"
 
Back
Top Bottom